WAUMINI wa dini ya Kiislamu mkoani Dodoma, wamewataka Watanzania kupuuza uvumi kuhusu mgogoro wa Libya, badala yake, wametaka kuungana na kumuombea kiongozi huyo adumu madarakani.
Wito huo ulitolewa juzi na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabaan, ambaye alisema hakuna machafuko nchini Libya bali kinachotokea ni kikundi kidogo alichokiita cha kihuni kinachopanga kumuondoa, Kanali Muammar Gaddafi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Sheikh Shaaban alisema tamko la Waislam wa Mkoa wa Dodoma ni kuwataka wenzao nchini na duniani, kuhakikisha hawaungi mkono kikundi hicho cha kihuni.
Sheikh Shaaban alisema kinachofanyika ni baadhi ya watu ambao wanapenda kunywa pombe na kutumia dawa za kulevya, walioko mpakani mwa nchi hiyo na Misri ndio walioanzisha fukuto hilo.
Mimi ni nina shahada ya sheria ambayo niliipata Libya, nina ufahamu mzuri wa uongozi wa Gadaffi, ni mtu wa upendo kwa watu wake na nimekuwa nawasiliana na wenzangu huko wanasema machafuko ni ya mji mmoja tu, sio nchi nzima, alisema Sheikh Shaaban.
Kiongozi huyo alisema licha ya kuongoza nchi yake vizuri kwa kwa muda mrefu, Kanali Gaddafi amekuwa na mchango mkubwa kwa mataifa mbalimbali.
Kanali Gaddafi amejenga msikiti mkubwa mjini Dodoma na nchini Uganda. Pia, alifadhili ujenzi wa msikiti wa Butiama, baada ya Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere kumuomba.
Source: Mwananchi