Waislam (batamiki) kuisalia dua chadema

Subir muone na hao wanaotukana uislamu humu jf mungu atawalaan inshallah
labda km wanafanya Dua kwa majini, lakni Mungu hasikilizi Dua zisizo sababu. Na kama wanaomba kwa majini, basi majini ni shetani, na shetani hana nguvu km Mungu tunaemwabudu. Yeye ni Mungu anatenda haki, na hiyo Dua itawarudia hao hao.
 
BATAMIKI kufanya dua ikiwa CHADEMA haitaomba radhi

Kauli CHADEMA kuwatuhumu masheikh kuwa wanatumika kuipa ushindi CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, zimechukua hatua mpya baada ya Baraza la Taasisi za Mikutano ya Kiislamu (BATAMIKI) kuipa CHADEMA siku tatu kuomba radhi kwa kuwahusisha viongozi hao kwenye masuala ya siasa na harakati za kuwania ubunge jimboni humo.

BATAMIKI imesema iwapo CHADEMA haitafanya hivyo katika kipindi kilichotolewa, litafanya dua maalumu ya siku saba kumwomba Mwenyezi Mungu awadhalilishe viongozi wa chama hicho na kuwaondoa katika nyadhifa walizonazo.

Awali, uongozi wa CHADEMA ulipewa wiki moja kuomba radhi kwa Watanzania na Waislamu kutokana na kitendo cha wabunge na wafuasi wake jimboni humo kumdhalilisha Mkuu wa wilaya hiyo, Fatma Kimario na kumvua hijabu. Hata hivyo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Profesa Abdallah Safari, alidai Fatma hakuwa amevaa hijabu bali mtandio na kwamba, chama chake kinaamini masheikh wanatumiwa na CCM katika uchaguzi huo ili kuipa ushindi.

Profesa Safari, ambaye awali alikuwa CUF na alijiunga CHADEMA baada ya kuangushwa katika uchaguzi wa mwenyekiti wa chama hicho na Profesa Ibrahim Lipumba, alidai masheikh walipaswa kuwa na subira.

Katibu Mkuu wa BATAMIKI, Sheikh Sadiq Godigodi, alisema jana kuwa, dua itafanyika kutokana na uongozi wa CHADEMA kushindwa kuwaomba radhi Watanzania na Waislamu.

“CHADEMA kutoa tamko kupitia Profesa Safari kuwa masheikh wanatumika kuipa ushindi CCM, si la kweli.

“Sheikh ni kiongozi wa Kiislamu ana mamlaka ya kutoa tamko kuhusu tendo lolote baya analoliona linafanyika kinyume cha utaratibu, ikiwemo kudhalilishwa kwa Uislamu,’’ alisema.

Alisema suala la masheikh kukemea si la kisiasa, bali lipo katika misingi ya heshima na kuutukuza utu wa Mwislamu.

“DC amedhalilishwa, viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuomba radhi na si kutoa majibu yasiyokuwa na mantiki, huku wakipotosha maana kuhusu hijabu,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Sheikh Godigodi, Kuruani inaeleza hijabu kama vazi la staha na linalotambulisha heshima ya mtu mbele ya jamii.

Alisema Sura ya 33 aya ya 59 katika Kuruani inasema: “Ewe mtume waambie wake zako na mabinti zako wote wa Kiislamu wajiteremshie vizuri shungi zao mpaka kifuani mwao kufanya hivyo kutawafanya wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe.’’

Kutokana na hilo, alisema BATAMIKI inamtaka Profesa Safari asitumike kwenye jambo lolote linalohusu dini ya Kiislamu, kwa kuwa viongozi wake wamekwishakosea na wanachotakiwa kukifanya ni kuwaomba radhi Waislamu.

Akizungumzia dua maalumu, Sheikh Godigodi alisema itasomwa kuanzia Jumanne na masheikh kutoka Uganda, Kenya na Tanzania.

“Endapo hadi Ijumaa CHADEMA hawatakuwa wameomba radhi Jumanne ijayo dua itasomwa kwa mikoa ya Tanga na Dar es Salaam na Zanzibar,’’ alisema.

Aliwataja masheikh watakaosoma dua hiyo kuwa Idrisa Adamu Waridi (Mombasa, Kenya), Mohamed Ismai (Lamu, Kenya), Mahmoud Lugaia (Uganda) na Rajabu Amran (Tanzania).

Katika hatua nyingine, CHADEMA imeanza kumshutumu mbunge wa Singida Kaskazini Tundu Lissu, kwa kushindwa kuomba msamaha kwa Waislamu kuhusu Fatma kuvuliwa hijabu.

Habari kutoka ndani ya CHADEMA zinasema katika kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika hivi karibuni mjini Tabora, iliamuliwa Lissu alimalize hilo kwa kuwaomba msamaha Waislamu.

“Unajua suala hili limefika hapa kutokana na baadhi ya viongozi kuwa wabishi na kuendeshwa chama katika misingi ya ubabaishaji. Wajumbe tulishakubaliana kwa kuwa tulishakosea tulipaswa kuomba radhi na kutoa sababu ambazo nahisi zingeeleweka kwa jamii na si kama ilivyo sasa,’’ kilisema chanzo hicho.

Alisema hatua iliyofikiwa ni matokeo ya ubishi wa Lissu na kuona CHADEMA inaonewa wakati mambo mengine sisi wenyewe ndio tunaojitakia.

Source:
Wavuti - Habari

My take, Mtajulikana na kila mtu kuwa hamna mwelekeo, mmepotoka na mtaliangamiza taifa hili, mnataka wakristo pia watoe tamko ili mpate pa kusemea kuwa CHADEMA ni chama cha kikrsto! Mlachemshije!
Hayo maswala ya dua wamuulize shehe wa Magomeni yuko wapi, aliyesema atamuwekea mkuu ulinzi wa majini???????????? Hivyo vitisho labda mungu wa kuzimu avifanyie kazi, lakini Mungu Baba ni wa haki wala haongwi na sala za unafiki!!!!!!!!! Majibu ya hizo dua mtazipata wenyewe, subiri mfanye huo mkakati mtamjua Mungu wa kweli ni nani!!!!!!!!!!
 
Wanatumia reverse psychology yote hiyo ni kutengeneza mazingira ya kusaidia CCM waibe kura lakini nadhani wamegonga mwamba nadhani Mrema na Mtikila na Mkapa wangeshaudead mpaka sasa,wangemwombea kikwete anayefanya watu kunywa chai ni jambo la anasa
Wanatumia kila mbinu kutishia eti CCM ishande Igunga basi. Vitisho vya ajabu ajabu, hivi wanalipwa na nani na fedha ngapi???????? Hapo wamegonga mwamba la kuvunda halina ubani CCM kwishiney by by kwaheri Igunga!!!!!!!!!
 
Hiyo dua mtasoma wenyewe masheikh njaa lakini sisi waumini tunao taabika na ccm hatuji someni natuone,hakika mungu hamfichi mnafiki nyinyi wanafiki tu,unajua huku warabuni ukisikia sheikh sio kwa sbb kasoma dini laa,kuna sheikh kutokana na umaarufu wke tu anaitwa sheikha,wengne kwa sbb ya pesa kama wale viongozi wa uae emirate wote ni masheikh lkn ndio wafadhili wa timu ya man city ya uk,sasa uislam na ligi kuu ya england wapi na wapi?

Sasa hawa wanaojiita masheikh wala hawatutishi,cdm msiombe radhi kabisa mm ni muislam lkn hawa maustadh njaa siwaogopi kabisa,wangekuwa wanauwezo wakuomba hizo dua nawaombe mvua ije umeme uwake masaa 24 mtera ijae maji,hyo danganya toto kwanza muislam gani mjinga kama wao ataekwenda kukunja miguu kwa kuomba dua ya kinafiki?
 
BATAMIKI kufanya dua ikiwa CHADEMA haitaomba radhi

Kauli CHADEMA kuwatuhumu masheikh kuwa wanatumika kuipa ushindi CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, zimechukua hatua mpya baada ya Baraza la Taasisi za Mikutano ya Kiislamu (BATAMIKI) kuipa CHADEMA siku tatu kuomba radhi kwa kuwahusisha viongozi hao kwenye masuala ya siasa na harakati za kuwania ubunge jimboni humo.

BATAMIKI imesema iwapo CHADEMA haitafanya hivyo katika kipindi kilichotolewa, litafanya dua maalumu ya siku saba kumwomba Mwenyezi Mungu awadhalilishe viongozi wa chama hicho na kuwaondoa katika nyadhifa walizonazo.

Awali, uongozi wa CHADEMA ulipewa wiki moja kuomba radhi kwa Watanzania na Waislamu kutokana na kitendo cha wabunge na wafuasi wake jimboni humo kumdhalilisha Mkuu wa wilaya hiyo, Fatma Kimario na kumvua hijabu. Hata hivyo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Profesa Abdallah Safari, alidai Fatma hakuwa amevaa hijabu bali mtandio na kwamba, chama chake kinaamini masheikh wanatumiwa na CCM katika uchaguzi huo ili kuipa ushindi.

Profesa Safari, ambaye awali alikuwa CUF na alijiunga CHADEMA baada ya kuangushwa katika uchaguzi wa mwenyekiti wa chama hicho na Profesa Ibrahim Lipumba, alidai masheikh walipaswa kuwa na subira.

Katibu Mkuu wa BATAMIKI, Sheikh Sadiq Godigodi, alisema jana kuwa, dua itafanyika kutokana na uongozi wa CHADEMA kushindwa kuwaomba radhi Watanzania na Waislamu.

"CHADEMA kutoa tamko kupitia Profesa Safari kuwa masheikh wanatumika kuipa ushindi CCM, si la kweli.

"Sheikh ni kiongozi wa Kiislamu ana mamlaka ya kutoa tamko kuhusu tendo lolote baya analoliona linafanyika kinyume cha utaratibu, ikiwemo kudhalilishwa kwa Uislamu,'' alisema.

Alisema suala la masheikh kukemea si la kisiasa, bali lipo katika misingi ya heshima na kuutukuza utu wa Mwislamu.

"DC amedhalilishwa, viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuomba radhi na si kutoa majibu yasiyokuwa na mantiki, huku wakipotosha maana kuhusu hijabu,'' alisema.

Kwa mujibu wa Sheikh Godigodi, Kuruani inaeleza hijabu kama vazi la staha na linalotambulisha heshima ya mtu mbele ya jamii.

Alisema Sura ya 33 aya ya 59 katika Kuruani inasema: "Ewe mtume waambie wake zako na mabinti zako wote wa Kiislamu wajiteremshie vizuri shungi zao mpaka kifuani mwao kufanya hivyo kutawafanya wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe.''

Kutokana na hilo, alisema BATAMIKI inamtaka Profesa Safari asitumike kwenye jambo lolote linalohusu dini ya Kiislamu, kwa kuwa viongozi wake wamekwishakosea na wanachotakiwa kukifanya ni kuwaomba radhi Waislamu.

Akizungumzia dua maalumu, Sheikh Godigodi alisema itasomwa kuanzia Jumanne na masheikh kutoka Uganda, Kenya na Tanzania.

"Endapo hadi Ijumaa CHADEMA hawatakuwa wameomba radhi Jumanne ijayo dua itasomwa kwa mikoa ya Tanga na Dar es Salaam na Zanzibar,'' alisema.

Aliwataja masheikh watakaosoma dua hiyo kuwa Idrisa Adamu Waridi (Mombasa, Kenya), Mohamed Ismai (Lamu, Kenya), Mahmoud Lugaia (Uganda) na Rajabu Amran (Tanzania).

Katika hatua nyingine, CHADEMA imeanza kumshutumu mbunge wa Singida Kaskazini Tundu Lissu, kwa kushindwa kuomba msamaha kwa Waislamu kuhusu Fatma kuvuliwa hijabu.

Habari kutoka ndani ya CHADEMA zinasema katika kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika hivi karibuni mjini Tabora, iliamuliwa Lissu alimalize hilo kwa kuwaomba msamaha Waislamu.

"Unajua suala hili limefika hapa kutokana na baadhi ya viongozi kuwa wabishi na kuendeshwa chama katika misingi ya ubabaishaji. Wajumbe tulishakubaliana kwa kuwa tulishakosea tulipaswa kuomba radhi na kutoa sababu ambazo nahisi zingeeleweka kwa jamii na si kama ilivyo sasa,'' kilisema chanzo hicho.

Alisema hatua iliyofikiwa ni matokeo ya ubishi wa Lissu na kuona CHADEMA inaonewa wakati mambo mengine sisi wenyewe ndio tunaojitakia.

Source:
Wavuti - Habari

My take, Mtajulikana na kila mtu kuwa hamna mwelekeo, mmepotoka na mtaliangamiza taifa hili, mnataka wakristo pia watoe tamko ili mpate pa kusemea kuwa CHADEMA ni chama cha kikrsto! Mlachemshije!

The way God judges things is different from the way humans judge! Ni upuuzi mtupu huu! Hakuna mtu yeyote mahali popote anayeweza kumwombea mtu mwenzake mabaya kwa Mumgu halafu Mungu naye awe mjinga kiasi hicho na kuikubali sala au dua ya namna hiyo! Mungu anafundisha kulingana na mafundisho ya dini ya Kikristo, "ukienda kutoa sadaka (kuomba dua, kusali nk) na kisha kukumbuka kuwa una kitu na jirani yako (ndugu, jamaa, rafiki, jirani, mtu mwenzako) acha dua yako kwanza, nenda upatane naye na mkiisha patana, ndipo nenda ukatoe hiyo dua yako."

Kwa maneno mengine, Mungu anasikiliza sala iliyo nyoofu - iisiyo na kinyongo (isiyo ya kumwombea mtu mwingine mabaya). Wanaodai wanawalaani wenzao kwa nia ya kuwaangamiza Mungu hakubali sala ya aina hiyo! Kusali/kuomba dua ina maana unajiweka mnyofu mbele ya Mungu na watu wengine (kusamehe mabaya yao). Pia Yesu alifundisha kusamehe hata maadui. Kama Chadema wamekuwa maadui kwa mtazamo wa hawa vipofu wa imani, wanatakiwa wasamehewe (ingawa sioni wapi walikosea!).

Hao masheikh ndio wanaopaswa waombe radhi kwa Chadema kwa kusema uwongo maana picha waliyopeleka kwa Watanzania hasa wale ambao hawasomi magazeti wala kuangalia TV ni kwamba huyo DC alivuliwa nguo na kubaki uchi kitu ambacho siyo kweli. Pia kwenye picha hapakuonesha kuwa alivuliwa hijab bali ilikuwa katika kumdhibiti huyo DC na mtandio wake kuvulika maana haukuwa umefungwa kwa pini au 'shazia'. Hawa watu ni kweli wanatumika vibaya kwa maslahi ya chama tawala!
 
Kama hawa mashehe na wengine wanaoamini nia yao kuwa ni njema wanataka kuishi pamoja na wasio waislamu, ni vema wakakubali kuwa dini yao haitapewa nafasi kubwa na watu wengine, kama wao wasivozipa nafasi imani nyingine. Hijabu ni swala la kiislamu na si swala la mwanamke yeyote au wote!!! Tusilazimishwe kuiona jamii katika kioo cha kiislamu!!

Dunia hii si ya imani ya kiislamu tu. Ni ya kila binadamu na kwa utashi wake. Kama vipi, wamuombe mungu awahamishie sayari nyingine!! Tanzania ni ya watu wote na si ya imani fulani au dini fulani.
 
Mashekhe au Makada wa Magamba? wanadhalilisha dini yetu kwa ubwabwa wa CCM mungu atawaalani na dua lao. Alisomewa Nyerere na Shekhe Kassim bin Jumaa, mungu awarehemu na haikumdhuru Nyerere ije kuwa Chadema kisa Mfuga Kiti moto amevuliwa ushungi. Wakwende zao kama wana njaa mimi nitawaalika kwenye Karamu ya Mdingi wangu
 
Hawa kamwe siyo waislam ni watu walio vaa kanzu,baragashia,ushungi na wametailiwa miskitini basi wakajiita ni waislam ambao wanampinga Mungu mmoja bali wana amini S.A.W na Mungu wa pili na watatu mwezi. Kwakweli BATA MAKI mmafanya masiala na Mungu kabisa yaani mnaleta mambo ya shirki kwenye imani...hawa wote wangekuwa waislam wasingefanya wala kutamka mambo hayo ya ajabu.Sijui ata madrasa wamesoma wapi? Kama kuna serikali hapo tziidii basi hainabudi kukemea mambo kama haya kwani gharama yake kubwa kuliko tunavyo fikilia.. Hivi hakuna waislam wakweli ambao wanaweza kemekea kabisa haya madudu au wote mmeshikwa masikio?
makae wakielewa wakristo ni robo 3 ya watanzania wt hata kama watatumia uislam wan kuinyima kura cdm wajue tayari wamepanda mbegu ya udini na hahtang'oka milele
 
kwa mara ya kwanza ndio napata hasira kutokana masuala ya udini, Nitarudi baadaye maana kichwa kimeanza kuniuma.

kiongozi wa dini - utashi = mdini.
kiongozi mdini
= UDINI.
1. BAADA YA HLI JAMBO, NAONA NGUVU HALISI YA DUA ITAKUWA NEGLIGIBLE.
2. UTATOKEA MTAFARUKU MKUBWA SANA NDANI YA DINI YA KIISLAMU(kana baadhi ya waisilamu pure wataanza kuupinga huu uongozi wa sasa wa waislamu)
 
ah ah ah ah wanacheza hao viongozi wa chadema wapo kwa matakwa ya MUNGU siyo mtu mwingine na hizo dua zao ngoja tuone kama zitawafanya kitu hizo ni jaa zinawasumbua
 
kwa mantiki hii watakuwa wamelaani (au kuroga kama wengine mnavyoweza tamka) waislamu watatu na si uislamu kama dini...tuweke mipaka wa shutuma zetu, japo tunaweza laumu kwa matumizi mabaya ya dini na vyama vyetu kwa maslahi binafsi
 
viongozi wa dini yangu ndio wanaosababisha dini yangu idharauliwe kutokana na ufahamu wao mdogo
 
Nasikia kichefuchefu nikiona baadhi ya watu bado wanapenda ligi za kipumbavui humu ndani hasa zihusuvo mambo ya dini. Kwani kuna ulazima gani wa kumlazimisha mtu kuwa ni mwisilamu wakati alishauacha miaka kadhaa iliyopita!?
 
Huyo Mungu wao wa ajaaabu, yaani mungu gani unamuomba amfanyie mwenzio baya? Badala ya kumwomba mungu amsaidi asirudie na aache uovu we unamwombe majanga. Ahh! Kwani uongo kuwa baadhi ya masheikh wanaitetea CCM? Nani asiyejua maovu yao na udini hapa nchini. Wajirekebishe bhana.
 
CCM inawatumia vibaya hawa ndugu zetu waislamu lilianza saga la DC na CDM, Bakwata wakaingia kichwa matokeo yake wameufyata na hawa BATAMIKi nao wamekubali kuingia kwenye mkenge tuone itakuwaje, halafu dua zote zinasomwa maeneo ya pwani. Mh...
Nasubiri movie hii iendelee
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom