Jidulamabambase
Member
- Nov 28, 2010
- 31
- 5
BATAMIKI kufanya dua ikiwa CHADEMA haitaomba radhi
Kauli CHADEMA kuwatuhumu masheikh kuwa wanatumika kuipa ushindi CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, zimechukua hatua mpya baada ya Baraza la Taasisi za Mikutano ya Kiislamu (BATAMIKI) kuipa CHADEMA siku tatu kuomba radhi kwa kuwahusisha viongozi hao kwenye masuala ya siasa na harakati za kuwania ubunge jimboni humo.
BATAMIKI imesema iwapo CHADEMA haitafanya hivyo katika kipindi kilichotolewa, litafanya dua maalumu ya siku saba kumwomba Mwenyezi Mungu awadhalilishe viongozi wa chama hicho na kuwaondoa katika nyadhifa walizonazo.
Awali, uongozi wa CHADEMA ulipewa wiki moja kuomba radhi kwa Watanzania na Waislamu kutokana na kitendo cha wabunge na wafuasi wake jimboni humo kumdhalilisha Mkuu wa wilaya hiyo, Fatma Kimario na kumvua hijabu. Hata hivyo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Profesa Abdallah Safari, alidai Fatma hakuwa amevaa hijabu bali mtandio na kwamba, chama chake kinaamini masheikh wanatumiwa na CCM katika uchaguzi huo ili kuipa ushindi.
Profesa Safari, ambaye awali alikuwa CUF na alijiunga CHADEMA baada ya kuangushwa katika uchaguzi wa mwenyekiti wa chama hicho na Profesa Ibrahim Lipumba, alidai masheikh walipaswa kuwa na subira.
Katibu Mkuu wa BATAMIKI, Sheikh Sadiq Godigodi, alisema jana kuwa, dua itafanyika kutokana na uongozi wa CHADEMA kushindwa kuwaomba radhi Watanzania na Waislamu.
"CHADEMA kutoa tamko kupitia Profesa Safari kuwa masheikh wanatumika kuipa ushindi CCM, si la kweli.
"Sheikh ni kiongozi wa Kiislamu ana mamlaka ya kutoa tamko kuhusu tendo lolote baya analoliona linafanyika kinyume cha utaratibu, ikiwemo kudhalilishwa kwa Uislamu,'' alisema.
Alisema suala la masheikh kukemea si la kisiasa, bali lipo katika misingi ya heshima na kuutukuza utu wa Mwislamu.
"DC amedhalilishwa, viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuomba radhi na si kutoa majibu yasiyokuwa na mantiki, huku wakipotosha maana kuhusu hijabu,'' alisema.
Kwa mujibu wa Sheikh Godigodi, Kuruani inaeleza hijabu kama vazi la staha na linalotambulisha heshima ya mtu mbele ya jamii.
Alisema Sura ya 33 aya ya 59 katika Kuruani inasema: "Ewe mtume waambie wake zako na mabinti zako wote wa Kiislamu wajiteremshie vizuri shungi zao mpaka kifuani mwao kufanya hivyo kutawafanya wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe.''
Kutokana na hilo, alisema BATAMIKI inamtaka Profesa Safari asitumike kwenye jambo lolote linalohusu dini ya Kiislamu, kwa kuwa viongozi wake wamekwishakosea na wanachotakiwa kukifanya ni kuwaomba radhi Waislamu.
Akizungumzia dua maalumu, Sheikh Godigodi alisema itasomwa kuanzia Jumanne na masheikh kutoka Uganda, Kenya na Tanzania.
"Endapo hadi Ijumaa CHADEMA hawatakuwa wameomba radhi Jumanne ijayo dua itasomwa kwa mikoa ya Tanga na Dar es Salaam na Zanzibar,'' alisema.
Aliwataja masheikh watakaosoma dua hiyo kuwa Idrisa Adamu Waridi (Mombasa, Kenya), Mohamed Ismai (Lamu, Kenya), Mahmoud Lugaia (Uganda) na Rajabu Amran (Tanzania).
Katika hatua nyingine, CHADEMA imeanza kumshutumu mbunge wa Singida Kaskazini Tundu Lissu, kwa kushindwa kuomba msamaha kwa Waislamu kuhusu Fatma kuvuliwa hijabu.
Habari kutoka ndani ya CHADEMA zinasema katika kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika hivi karibuni mjini Tabora, iliamuliwa Lissu alimalize hilo kwa kuwaomba msamaha Waislamu.
"Unajua suala hili limefika hapa kutokana na baadhi ya viongozi kuwa wabishi na kuendeshwa chama katika misingi ya ubabaishaji. Wajumbe tulishakubaliana kwa kuwa tulishakosea tulipaswa kuomba radhi na kutoa sababu ambazo nahisi zingeeleweka kwa jamii na si kama ilivyo sasa,'' kilisema chanzo hicho.
Alisema hatua iliyofikiwa ni matokeo ya ubishi wa Lissu na kuona CHADEMA inaonewa wakati mambo mengine sisi wenyewe ndio tunaojitakia.
Source: Wavuti - Habari
My take, Mtajulikana na kila mtu kuwa hamna mwelekeo, mmepotoka na mtaliangamiza taifa hili, mnataka wakristo pia watoe tamko ili mpate pa kusemea kuwa CHADEMA ni chama cha kikrsto! Mlachemshije!