anasumbuliwa na usimba/uyanga. safari hii naona kaita wavuta ganja wenzake. mia
Simba wa sasa na wale legion timu ina kama 12 hivi.mkuu huo u simba na u yanga unaoongelea hapo ni upi umefuatilia selection yake kwa makini kwa maoni yangu nadhan utakuwa umekosea kidogo, kama cjakosea yanga wanawachezaji wawili tu(nurdin na kado) na anayecheza ni nurdin kwan kado hana tofauti na mtazamaji. Inshort labda uzungumzie kitu kingine na uyanga au usimba
TFF sijui walikuwa usingizini,Julio?mimi alipotangazwa tuu julio ........nilianza kuikataaaa!!! the same timu ingekuwa chini ya kocha mwengine ningeikubali sana!!!
hahahahahaa, hiyo ni timu ya kocha mmojawapo kati ya walioteuliwa kuiongoza kili statz (Julio), nimeshangaa zaidi kitendo cha kumuita Said Maulid kwenye kambi, huyu mtu si ameshaanza kuzeeka kisoka, sasa wanamwita ili iweje......kwa nini basi wasingeita walau wachezaji kadhaa wa timu ya vijana ili kuwapa uzoefu?........ hao ndio makocha wetu wazawa...ngoja tuone kitakachotokea.
Unazi na pia ameshaover take Mkwasa,maana yeye ndio msemaji mpanga timu na mpiga porojo mkuu.kusema ukweli mimi ni moja kati ya wanaopinga kuendekezwa kwa makocha wa kigeni, na kama ingetokea kocha mzawa akapewa timu, ningempendekeza Jamhuri kwa kigezo cha uzoefu na uwezo wa kuwajengea ari wachezaji. Ila kwa mwendo anaoenda nao kwenye Challenge plus tuhma za kuleta unazi kwenye kuunda timu, nimepungukiwa na imani kabisa!
Wamenifurahisha kwa kumleta Boban na kuachana na kasumba za makocha wazungu...na amini chini ya Julio timu itakuwa na hamasa maana hii kazi ya kuamasisha anaiweza sana....
Puli hilo,teja teja tu.huu ushabiki wa kijinga ndio unatupeleka kuteua timu mbovu mbovu! BOBAN! BOBAN! Mbona hakuonyesha cha ajabu siku na Rwanda????????? TENA alikuwa CHOKI Mbaya!
Hata Kazimoto hana match fitness,alikuwa majeruhi kwa muda mrefu.Julio mjinga sana kajaza simba hata uwezo hawana,eti Juma Jabu wa kumzidi Oscar Joshua? Kapombe wa kumnyima namba Taita? Cpingi uwezo wa Kazimoto,Kaseja na Nyoso..
Jionee haya kwenye Kili Stars:Mkwasa na Julio nao... Mkongwe Saidi Maulidi wangemuacha, muda wake umekwisha. Afadhali badala yake wangemchukua John Boko kwa manufaa ya sasa na ya baadaye. Nadhani kuna kujuana hapo...
Thomas Ulimwengu naye aache uchoyo na tamaa.
Inakuwaje Coastal Union inatoa wachezaji 3 wakati wako mkiani mwa ligi ilhali timu kama Oljoro JKT haina hana mmoja?
Kwa mchezaji ambae timu yake iko mkiani,tegemea kwamba udhaifu wa timu hiyo umechangiwa na wachezaji,hivyo kwa viwango vyao hawafai kuchezea timu ya taifa.Kocha anamteua mchezaji kwa kutumia vigezo mbali mbali kimojawapo kikiwa ni kumfahamu mchezaji uwezo wake uwanjani. Na hili linawezekana sana akimuona mwenyewe mchezaji akifanya mazoezi na kucheza katika mechi za kimashindano. Coastal kuwa mkiani haimaanishi kuwa wachezaji woote hawana uwezo wa kuchezea timu ya Taifa ya Tanzania Bara/Tanganyika(Kilimanjaro Stars). Kwani wachezaji watatu tu ndio wanoichezea Coastal union! Pempua zaidi mkuu. Pili shaurini makocha kuhusu wachezaji wanaofaa kuchezea timu mzipendazo kwa kufuata utaratibu(huku mkitoa vigezo vinavyoeleweka kulingana na wakati uliopo).
Kwa mchezaji ambae timu yake iko mkiani,tegemea kwamba udhaifu wa timu hiyo umechangiwa na wachezaji,hivyo viwangio vyao hawafai kuchezea taifa.
Hoja yako(kwangu mimi) inakuwa na uzito, endapo ligi ambayo Coastal Union inashiriki ingekuwa inaendeshwa kwa "fair play" ndani ya uwanja na nje ya uwanja. Mara ngapi tumesikia malalamiko ya Timu zenye vipato vidogo inkiwemo Coastal (katika ligi ya Tanzania bara/Tanganyika) kulalamika kuwa zinaonewa na marefa (kwa marefa kuzibeba timu kubwa Simba na Yanga n.k baada ya kula rushwa i.e najua issue ya refa Kazi unaikumbuka). Hoja yako ni 'ideal' katika ligi za nyumbani(Vodacom league) .