Wahusika wa mwendokasi (UDART) tufahamisheni hili la Kimara

Wabesa

Member
Jan 7, 2016
78
56
Habari wakuu,

Natumai humu ndani wapo au watasoma wahusika wa UDART.

Nikiwa natoka Kariakoo/Posta naunga kwenda Mbezi, namiliki kadi nikifika pale Kimara nakwangua kadi sehemu mbili.
*Pa kupita kuelekea liliko bus.
*Ndani ya bus.

Je, nakatwa vipi hapo ili ije total Tshs 150?
 
Unatakiwa ukatwe 150 tsh kimara,sababu Gerezani wameshachukua 650tsh
Sawa kabisa kwa maelezo yako.

Ila pale Kimara tuna scratch sehemu mbili....

Je,au pale pa kupita kuelekea kwenye bus HUKATWI??

Kisha hiyo 150 inakatwa ndani ya gari?

Mind you,hiki king'amuzi cha gari ndicho kinachokata 400 unapopanda Mbezi.

Hili limekaaje??

Kama kuna button za kubadilishwa na dereva pindi gari inapofika Kimara tuelezwe,nje na hapo pesa za KADI zitakua na sintofahamu.
 
Isije nauli ikaja hivi 650+650+150=????
Napata shaka sana.

Kama si hivyo yawezekana;

*650+ 400+400

*650+400+150

*650+ 400

Yawezekana ndiyo maana IDADI ya Safari na Makato inatusumbua ktk kadi na kua na SINTOFAHAMU kubwa.

Hopeful watakuja kutueleza .
 
Napata shaka sana.

Kama si hivyo yawezekana;

*650+ 400+400

*650+400+150


*650+ 400


Yawezekana ndiyo maana IDADI ya Safari na
Makato inatusumbua ktk kadi na kua na
SINTOFAHAMU kubwa.
Hopeful watakuja kutueleza .
Udhulumati tu,kwanza walisemaga unaweza tumia nauli yako kabla ya lisaa limoja Kama sikosei,mfano Labda umeenda kariako fasta na ukageuza fastaa hilo Naona halifanyiki ktk Giner wala kadi zaoo...ukichanjaa tu maana yake unakatwaaaa
 
Mbezi-kimara 400,kimara kwenda popote 650 jumla 1050,Bei elekezi ya Sumatra ilitakiwa ukitoke Mbezi kwenda Gerezani, kivukoni, Morroco iwe 800,Udart watuibia
 
Siyo kwamba Serikali,SUMATRA,UDART hawaoni hilo tatizo isipokuwa ni kama vile wanafurahia adha sisi abiria tunayoipata.
 
ukitoka mbezi kwenda kimara wanakata 400 ukiunganisha wanakata 400 total800 ukitoka posta,kkoo 650 ukiunga wanakata 150 total 800 mimi niliweka 1000 tu kwenye akaunti yangu ya dart ili nijaribu ikakubali
 
Back
Top Bottom