Wahuni wamchoma sindano ya sumu kada wa CCM

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
5,023
2,553
Aliekuwa mgombea wa udiwani kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 Bwana Celisi Mosha kwa tiketi ya cmm tarafa ya Vunjo (kilema kati) amejeruhiwa na watu wasiojulikana kwa kumkata sehemu kubwa ya mwili wake pamoja na kumchoma sindano yenye sumu usiku wa kuamkiableo.Bwana Mosha ni mjasiriamali na alikuwa anaelekea mnadani kwa ajili ya ununuzi wa ngombe .Hivyo basi ukiwa kama mwana Vunjo unaombwa mchango wako ili kuweza kufanikisha ujenzi wa kituo cha polisi ambacho kitakuwa kinatoa huduma kwa wanavunjo wote bila kujali itakadi zetu.Zinahitajika takribani shilingi milioni hamsini ili kuweza kamalizi ujenzi wa hiki kituo cha polisi pale kilema kati karibia na hospitali teule ya Vunjo.Mwanavunjo yoyote mwenye hamasa ya kutaka kuchangia anaombwa kuwasilisha mchango wake kupitia account number 0550124315 Benki ya Akiba commercial Bank ( Kilema Division Develipment Trust Fund)
 
Mbona hueleweki unataka mchango wa kituo cha policcm au unatupa habar ya mtu kucharangwa mapanga hata hivyo hiyo michango ya ujenzi wa kituo mchangishane magamba kwani cdm hatuwezi kuwachangia wauaji hao
 
Makupa umekunywa nini mchana huu?

mkuu swala la usalama wa wazazi wetu na ndugu zetu kule Vunjo si la kufanyia mchezo hata kidogo .Embu fikiria kuwa ni ndugu yako ndie aliejeruhiwa
 
Kituo cha Polisi?
Ikifikia hapo tunasikilizana lakini wananchi tukiongea mengine tunaambiwa yako Mahakamani.. Mengine tunaambiwa Hakuna ushahidi wa kuwapeleka mahakamani mafisadi.. Zaidi tukipeleka ushahidi tunageuziwa kibao!.. Ya mabwepande bado yanatokota!.. Ebu niacheni!
 
Nieleweke: Serikali haitusikilizi wananchi ndiyo maana inakosa fedha za kujengea kituo cha polisi.
 
mkuu swala la usalama wa wazazi wetu na ndugu zetu kule Vunjo si la kufanyia mchezo hata kidogo .Embu fikiria kuwa ni ndugu yako ndie aliejeruhiwa

na wewe fikiria wale polisi waliomuua yuje muuza magazeti kule moro, angekua ndugu yako?.. alafu uwape mchango??
 
Hata kama polisi wako cm 10 toka kwako hawawezi kuja kukuokoa ukivamiwa na majambazi.Majambazi wakipora na kuondoka na wao ndo wanakuja wakijidai wako bize kuwasaka.Si shauri watu kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi.Ingekuwa ujenzi wa shule au hospitali hapo angalau ingekuja akilini.Ujenge kituo cha polisi halaf aje akupige risasi za moto au akubambikizie kesi wapi na wapi
 
ni daktari gani aliyekupa ripoti kuwa kachomwa sindano ya sumu? kuwa makini na thread yako coz kuna siku utisaidia mahakama ushahidi.
 
Makupa wewe ni gamba tena lililokomaa,hizi habari peleka kwa magamba wenzio waambie kuna trilioni 12 zipo uswiss mkazichukue mjenge nazo vituo vyenu vya policcmagamba...sitaki hata kuwaona wauwaji hawa!!!hawana msaada wowote kwetu.
 
Tutolee upuuzi wako hapa, wamiliki wa sindano za sumu ni polisi na usalama wa taifa, sasa kama wameua mtu tuwachangie tena?
 
Nieleweke: Serikali haitusikilizi wananchi ndiyo maana inakosa fedha za kujengea kituo cha polisi.

Mkuu nasikia 2015 unataka kugombea ubunge Moshi Vijijini kwa tiketi ya CHADEMA. Vipi kuhusu kukubalika ? Na je umefikia muafaka na Komu au umeamua kivyako LIWALO NA LIWE?
 
mkuu swala la usalama wa wazazi wetu na ndugu zetu kule Vunjo si la kufanyia mchezo hata kidogo .Embu fikiria kuwa ni ndugu yako ndie aliejeruhiwa

mbona unajibu tofauti na swali uliloulizwa!?? Kiswahili kigumu au hakieleweki?
 
Back
Top Bottom