Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,220
mwache ajipe moyo tu.
sio kujipa moyo.... Ndio ukweli huo. Nimeangalia future na nikapata ushauri kwa mtu anayefanya kazi ya Archaeology Arusha.
mwache ajipe moyo tu.
sio kujipa moyo.... Ndio ukweli huo. Nimeangalia future na nikaisoma vizuri. Nikimaliza degree naunganisha Masters.
teh teh teh,kweli wewe hujui haya mambo yanaendaje mkuu!!ebu maliza kwanza hyo masuala yako ndo akili itafunguka..
Serikali yetu haina mpango maalumu wa kutengeneza nafasi za ajira ingawa kuna wizara ya Kazi na Ajira.Kabla ya kujiunga na chuo hapa Tanzania ni vema mhusika akafanya japo utafiti kidogo ili kujua sekta zinazotoa ajira. Ajira binafsi ni ngumu kwa sababu mitaala yetu haiwaandai vijana wetu kujiajiri pia mitaji ni tatizo kwani mpaka uwe na hati ya nyumba, shamba, nk. Nchi hii ngumu ati!
hah sasa kama msomi kama wewe cju dugrui holder au diploma unataka serikali ikupe ajira au uwajiliwe elimu yako imekusaidia nini?Hapo darasa la saba,form 4 na six wasemeje?Umesoma tena kwa kutumia kama sikosei kodi ya wananchi na bado unataka wakuajiri na kukulipa kutumia kodi zetu badala ya wewe kuwaajiri wao!UWO NI WIZI.!!Jiajiri na uwajiri wengine bwana.
utashangaa, lakini nimemwona aliyefanya hivyo. Cha msingi ni kupiga kitabu, na kuondoka na GPA za maana. Maana ninataka hata nje ya nchi nikasome. So...ni mipango tu.
inaonesha uko 1st year mkuu?
Dude mbona niliwahi kukuambia kuwa nipo first year?
hah sasa kama msomi kama wewe cju dugrui holder au diploma unataka serikali ikupe ajira au uwajiliwe elimu yako imekusaidia nini?Hapo darasa la saba,form 4 na six wasemeje?Umesoma tena kwa kutumia kama sikosei kodi ya wananchi na bado unataka wakuajiri na kukulipa kutumia kodi zetu badala ya wewe kuwaajiri wao!UWO NI WIZI.!!Jiajiri na uwajiri wengine bwana.
Serikali imewasaidia kwa kuwasomesha bure sasa mnataka nini tena.!Eti mtu anamaliza chuo hawezi kuyatumia mazingira anakoishi kuanzisha ajira yake binafsi.Nimeshangaa mwana Jf mmoja anasema utaanzishaje kampuni kama hauna mtaji!Hivi kwanini mnawaza kuanza na makubwa hivyo badara ya kuanza na madogo ndo yaje yawe makubwa ndo maana mkipata kazi mnaiba mijizi tu.
ok,uko wap nikutafute baadae unitoe hata mamsosi?
Nchini Tanzania inaaminika kuwa kuna wasomi wachache,kwa tatizo ili la wasomi wachache basi hao waliopo wangekuwa wanatumika kwa fujo sana katika maeneo mbalimbali yanayoitaji taaluma.
Sasa cha kushangaza kwanini nchi yenye wasomi wachache, kati ya hao wachache wengi wanasemekana hawana ajira maalumu(wanafanya kazi kwenye sekta isiyo rasmi).Tatizo ni nini la kutokuajiri wasomi? Au wanachosoma hakina maana kwa taifa?
inawezekana nchi yetu ina wasomi wachache ukilinganisha na nchi nyingine. lakini kuwa na idadi ndogo ya wasomi haimaanishi kuwa wasomi wote watapata kazi. kazi hupatikana ikiwa kuna shghuli nyingi za uzalishaji. kama tuna zalisha manake tuhitaji watu wengi wa kufanya kazi ktk kampuni za uzalishaji. kwa sasa nchi yetu haizalishi inategemea kuingiza mali toka nje , sasa kazi haziwezi kupatikana. kwa mfano kufa kwa viwanda vya nguo kumepoteza ajira nyingi sana, kila kiwanda kinatakiwa kiwe na wanasheria, wahasibu, nk. lakini leo tuna vaa mitumba na nguo toka china manake kazi zimepotea hapa. hatuna viwanda vya kusindika madawa kwa mfano, manake tusitarajie ajira kwa wataalamu wa madawa , na hata hao wa fani nyingine ambazo zitasaidia kuendesha hivyo viwanda.
kwahiyo tatizo si idadi ya wasomi, tatizo ni kazi zenyewe hazipo kutokana na kukosekana shughuli za uzalishaji
Dogo ukimaliza nitafute nikupe shavunipo mabibo block E. #231
nipo mabibo block E. #231