Wahitimu wa Fani mbalimbali nchini wafaidika na Huduma Mpya ya Nafasi za Kazi

justdoit

Member
Sep 2, 2009
63
4
Kutokana na Urahisi wa Huduma hii ya Nafasi za Kazi wahitimu wa fani mbalimbali Tanzania wamejikuta wakichangamkia nafasi za kazi zinazotanganzwa na makampuni kabla hata ya kutangazwa kwenye magazeti. Hali inayowafanya kuwa mbele ya mda katika soko la ajira lenye ushindani mkubwa.



Kujiunga ni Rahisi Sana !

Unatakiwa kuandika neno KAZI( acha nafasi) ikifuatiwa na aina ya kazi unayotafuta halafu utume kwenda 15522.

Mfano: Kama unatafuta kazi ya MARKETING andika KAZI MARKETING na utume kwenda namba 15522.

Punde utaanza kupokea nafasi za kazi uliyoomba. Kujitoa Andika neno KAZI(acha nafasi) ikifuatiwa na neno ONDOA na utume kwenda 15556.

Ukitaka kupata kazi bila kujiunga andika neno KAZI(acha nafasi) ikifuatiwa na herufi S (acha nafasi) ikifuatiwa na aina ya kazi unayotaka na utume kwenda 15522. Mfano: KAZI S MARKETING na kutuma kwenda namba 15522.

Gharama ya kujiunga(ambayo hutozwa mara moja) ni shilingi 250 tu pamoja na VAT, na kila kazi utakayotumiwa utachajiwa shilingi 150 tu pamoja na vati.

Masharti na vigezo kuzingatiwa.


Baadhi ya Nafasi za Kazi zilizopo:

Accountant
HR
Public Relations
Journalism
Business Administration
Social Science
Cashier
Finance
Banking
Graphic Design
Nursing
Doctor
Clinical Officer
Electrical Engineer
Electrical Technician
Electrician
Auto Electrical
Mechanical Engineer
Mechanical Technician
Auto Mechanics
Civil Engineer
ICT
Chemical and Processing Engineer
Driver
Secretary
Typist
Office Attendant
Receptionist/Customer Care
Sales and Marketing
Administration
Public Administration
Teacher
Sociology
Social Work
Printer

Na nyingine nyingi.
 
Watangazaji wa huduma za kazi ingefaa walipwe na makampuni yanayohitaji hao wafanyakazi, sio watafuta kazi.

Tutajuaje kwamba kuna kazi za kutosha kuhalalisha malipo haya? vipi kama kuna kazi mbili kwa siku zinatoka na wateja 10,000 wanatumia huduma hii kwa siku? Hili litakuwa sawa? Hii itakuwa biashara au kanyaboya?

Tunataka huduma zenye kusaidia watafuta kazi na waajiri, sio ujanja ujanja wa kujitengenezea fedha haraka bila kufanya kazi.
 
Huu ni uwizi wa kisasa...matangazo ya aina hii yapo mengi hapa mjini tafadhali serikali tunaomba muingilie kati na kuchukua hatua.
 
Tanzania tunahitaji some sort of "Better Business Bureau".

"Better Business Bureau"! Hapa inabidi ufafanue kinaganaga, kuna watu wa aina mbalimbali kwenye jukwaa hili, hata wasukuma wanaosoma kiswahili kwa shida sana kama "a-li-ku-ja" wamo, ila inabidi nao wakuelewe sababu yaweza kuwa watoto wao wamesoma wanasigina soli ya kiatu mtaani mda huu!
 
Sidhani kama ni kweli fursa za ajira Tz leo zinapatikana kwa njia hiyo. Nafikiri ako ni kamradi ka mtu tu. Ajira bongo sasa hv depends on who u knw na co kwa kutumia...!
 
Hivi mnadhani mtu kuwa ma-critics ndo maendeleo au uelewa? Hata kama Idea ni nzuri huwa mnatoa mawazo ya kui-discourage...
Just yesterday tumepokea testimony kwa watu watatu wamepata kazi kwa kutumia huduma hii...mnaona hiyo TZS 150 mtu anachajiwa ni kubwa sana na tunafaidi kuliko kazi atakayopata. Hamuoni hizo kamari zinazochezwa kwenye simu kila siku na watu wanapoteza maelfu ya shilingi bila mafanikio? Just yesterday we received three testimonies kutoka kwa watu ambao wamepata kazi kwa kutumia huduma hii.

Badilikeni... This service is not politics or gambling. It's legal business that's why you subcribe to it if you are impressed and you can unsubscribe anytime you wish to.
 
KAZImobile:
Hakuna kazi mpya kwa sasa ,utatumiwa ujumbe wa nafasi za kazi ya ICT ndani ya muda mfupi.

kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaa!:confused2:
 
mimi naona huo ni kama wizi,hiyo huduma nimewahi kutumia hakuna lolote,tufike sehemu tuache kuibiana.
 
Ooooooo!!!!!!! Kweli huu ni Usaniii babkubwa.Lakini it is Ok,Jamaa hawa siyo wavivu wa kufikiri,maisha ni mapambano,nao wanapambana kihivyo.
 
KAZImobile:
Hakuna kazi mpya kwa sasa ,utatumiwa ujumbe wa nafasi za kazi ya ICT ndani ya muda mfupi.

kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaa!:confused2:
Ic jamaa wamenitumia nafasi za kazi...guys changamkeni ,inasaidia kimtindo!
 
Back
Top Bottom