Wahisani:Bajeti tuliyopewa ni tofauti na ile iliyosomwa Bungeni

Matunda ya wizi wa mitihani sasa yanaanza kulipa.Mtakumbuka kuwa wahitimu wetu katika level mbalimbali wamekuwa wakiibuka kufaulu kwa kuiba mitihani, maana yake uwezo wao wa kujenga hoja za kitaalam unakuwa finyu matokeo yake wanatimiza majukumu yao kwa njia ya udanganyifu kama wao walivyofaulu.Matunda haya yatarigharimu sana taifa kwani tayari hata sector zingine ujinga kama huu umeanza kujitokeza.Niwakumbushe wana JF kuwa mwaka juzi kuna Doctor muhimbili alimfanyia mgonjwa wa kichwa operation ya goti na mgonjwa wa goti akafanyiwa operation ya kichwa.Maajabu kweli kweli, kwa uongo huu tutaweza hata ku-compete kwenye jumuiya ya A.Mashariki.

Tusubiri tuone
 
kwa hili mkulo ajiuzulu , mtu mzima kudanganya c issue ila ukibainika ni noma , ajiuzulu c ni yeye aliyeiwasilisha imf na bungeni . Ila kabla ya kutwambia ameonewa sana amefadhaika sana atuambie ipi original na ipi kanyaboya .
 
kwa hili mkulo ajiuzulu , mtu mzima kudanganya c issue ila ukibainika ni noma , ajiuzulu c ni yeye aliyeiwasilisha imf na bungeni . Ila kabla ya kutwambia ameonewa sana amefadhaika sana atuambie ipi original na ipi kanyaboya .
Hili la kujiuzulu unaliona likitokea? Nani atashinikiza Mkulo ajing'atue? Mwajiri wake? wahisani? Wananchi?
 
Serikali ya SISIEMU sasa hii imezidi, mnachakachua mpaka bajeti !? Bajeti ni mojawapo ya nyenzo za kutuongoza katika kuamua vipaumbele gani tuvigharamie na pia kuwa na nidhamu ya matumizi ya kodi za Watanzania na wahisani wetu.

Sasa ikiwa serikali ya SISIEMU haioni umuhimu ya bajeti kuleta nidhamu ya matumizi ya pesa, kwa kweli tumekwisha!

Halafu Mh. Mustafa Mkulo(MB) Waziri wa Fedha anasema IMF imewasifia na kuwa Tanzania inafaa kukopeshwa? Labda IMF imeona kwa vile vitabu vya mahesabu ya serikali ya Tanzania na bajeti yake ni shagalabaga, hivyo IMF itapa interest kubwa kwa mikopo yake kwa Tanzania! Kweli ukiona unasifiwa na IMF basi ujue umeliwa!
 
Si mara yake ya kwanza kudanganya mwaka 2008 Mkullo alikuja na bajeti ya uongo akakurupushwa na Mh.Cheyo wakishirikiana na Dr.Slaa ikabidi akafanye marekebisho kabla ya bajeti kupitishwa na bunge.Safari hii kaingia CHOO CHA KIKE.
 
Kumbe ndio mchezo wao ati!!!!! Basi mchezo kama huu utakuwa unachezwa sehemu nyingi kuanzia sector za chini wanaposubmit budget zao wizarani.
 
Si mara yake ya kwanza kudanganya mwaka 2008 Mkullo alikuja na bajeti ya uongo akakurupushwa na Mh.Cheyo wakishirikiana na Dr.Slaa ikabidi akafanye marekebisho kabla ya bajeti kupitishwa na bunge.Safari hii kaingia CHOO CHA KIKE.
Ni kwa kurejea bajeti ile ya 2008 nilisema hii si mara ya kwanza kwa Mkulo kufoji bajeti. Nadhani aliona kwa ngazi ile amemaliza sasa achakachue kwa ngazi ya kimataifa.
Huu mchezo mchafu ninashawishika kusema unaaznzia ngazi za halmashauri/manispaa mpaka huko kwa Mkulo.
 
Mkullo kwa wahisani hana sifa nzuri, mwaka jana pia alifuja mamilioni ya pesa za waathirika wa mafuriko Kilosa zilizotolewa na EU, ni baada ya wahisani kupewa taarifa na wananchi kwamba nyumba za dharura zilizotakiwa kujengwa ili wajihifadhi waathirika hakufanya hivyo.Na hata JK alipewa taarifa hizo za kifisadi na alikwenda mwenyewe kujionea kutotekelezwa huko, cha ajabu hakuchukua hatua na bado kamrudishia kitumbua chake aendelee kuji-savia.
Lakini kumbe ni kweli kwamba za mwizi ni arobaini.
 
Hii nchi sehemu gani inafanya kazi seriously? Haya mambo ya aina hii si aibu tupu.
 
Ndiyo maana tunasema JK SI RAIS MAKINI.Tusitegemee kuona mabadiliko ya kiuchumi, hata kuchaguliwa kwa kina Magufuri na Mwakyembe hakutatusaidi kwani mgawaji wa mishiko ya nchi (Waziri wa fedha ndo huyo).Gabbage in gabbage out
 
This is absolutely more than shame. Our leaders have completely gone insane

I hooe this is done to serve some purpose not intended to benefit Tanzanians but a certain group of people.

Its shame, shame, shame beyond doubt
 
Hao wahisani nao ni wanafiki wakutupwa. Ni kila mwaka wanagundua madudu ya kila namna lakini bado hawachukui hatua mathubuti. Ni kweli pesa nyingi hata zile zilizoanishwa kwa miradi ya maendeleo zinaishia tumboni mwa wachache!! Nawashauri hawa wahisani sasa wawekeze kwenye elimu ya uraia ili kule vijijini wapate kufahamu kuwa tunahitaji serikali mpya tofauti na ile ya CCM ili kubadili hali. Keshokutwa tunasheherekea mika 49 ya mateso na umaskini uliokithiri kwa zaidi ya asilimia 75 ya wananchi. Kweli bado tunahitaji serikali ya namna hii? Hebu tufanye mabadiliko tukianzia na katiba yetu ili basi 2015 kieleweke. So shameful!!
 
Mkullo kwa wahisani hana sifa nzuri, mwaka jana pia alifuja mamilioni ya pesa za waathirika wa mafuriko Kilosa zilizotolewa na EU, ni baada ya wahisani kupewa taarifa na wananchi kwamba nyumba za dharura zilizotakiwa kujengwa ili wajihifadhi waathirika hakufanya hivyo.Na hata JK alipewa taarifa hizo za kifisadi na alikwenda mwenyewe kujionea kutotekelezwa huko, cha ajabu hakuchukua hatua na bado kamrudishia kitumbua chake aendelee kuji-savia.
Lakini kumbe ni kweli kwamba za mwizi ni arobaini.

Mkubwa nataka uelewe tu kwamba kiongozi yeyote anayeingia madarakani kuna taasisi nyeti ambazo ni lazima aweke watu ambao watamlinda!! Sehemu/taasisi hizo ni kama Usalama wa Taifa, Fedha, Ulinzi, Mambo ya Ndani, Mahakama, Bunge, Mwanasheria Mkuu, etc, etc. Heads wa units/institutions hizi oooooooh sitaki kusema. Kwa mantiki hiyo. Mkulo is also doing the needful to his master au!!!!! Kila mbuyu na.......hivyo basi hata mngepiga baragumu hakuna kitu hapo!!!

 
Nina chefuka na uhuni huu. Watakuwa wanatengeneza nakala hata zaidi ya tatu. Moja wanapeleka uarabuni, nyingine ulaya nk. Ile inayopitishwa mjengoni, inatunzwa ofisi ya spika. teh teh
 
Namshukuru Mungu kwa kuwa siku zote nimekuwa na hisia kuwa budget inayopelekwa bungeni ni fake. Tazama tangu 2006 budget inaongezeka lakini maendeleo hakuna yaani hata hizo fedha za maendeleo hakuna. Mara nyingi najiuliza je, Bunge likisha pitisha budget je, upata fulsa kupitia utekelezaji wake au ndo imetoka mpaka report ya CAG. Je, kunamid year review. Kwa nchi kama yetu aingii akilini unaposikia kunafungu limebaki halikutumika wakati Rorya, Katavi hakuna barabara ya lami. Ni kweli wanapika ulizia jinsi hazina walivyohaha na budget hii utacheka. Nchi inajengwa kaskazini mwa Tanzania na kubomolewa mashariki mwa Tanzania.
 
Hizi ni karata njema kwa upinzani kujijenga na kuonyesha kuwa mambo ya nchi siyo ya kufanyia mchezo. Yaani nasema kuwa upinzani wakiweza kumsukuma mkulo ajiuzulu yatakuwa mafanikio makubwa sana kwao na kwa taifa. Wakifanya utafiti watagundua kuwa kuna barabara na miradi mingi tu inaendelea nchini na haikutengewa fedha na bunge na ile iliyotengewa fedha imetulia tu wala hakuna kazi yoyote inayoendelea huko.

Hapa ndipo mahali pa kupelekea miswada binafsi ili wabunge wa CCM wasipounga mkono watanzania wawatengee adhabu yao

Rsp.
 
Back
Top Bottom