Wahindi walazimisha kuuziwa nyumba za Upanga

Mi naona wangepewa tu bure,maana ni wapangaji wa muda mrefu.TUWE WAZALENDO ZAIDI.
 
Habari zako za kinafik nafik. Hao wahindi hizo pesa walizitowa wapi? Au wao wanauwezo wa kuzitafuta zaidi yako? Majumba ya Upanga yalijengwa na wahindi na yakadhulumiwa na nyerere na wapangaji ambao si wahindi huziuza kwa shida zao za pesa.

Au hujui kuwa wengi wetu hata tukifiwa Dar basi hata kama kuuza flat tutauza ili tusafirishe maiti Kilimanjaro au Kagera au Mbeya? Au hujuwi kuwa wengi wetu tukiwa na kipaimara basi hata flat tutauza ili tukifanye cha nguvu? Au hujuwi kuwa wengi wetu tukimcheza mwari tutauza hata flat?

Ujinga wetu ndio maradhi yetu.

Wahindi ni wachapa kazi, wametoka walikotoka wakaanza kuuza bajia, chachamawa, kachori lakini tazama baada ya muda wako wapi? Na hausikii wanamcheza mtoto, wanakipaimara, wana harusi za kifahari, wana maziko ya kuleweshana. Wao kazi, kazi, kazi. Ndio maana unawaona wao ndio wana mafanikio. Wahindi huanza kula maraha wakishajijenga kimaisha na si kabla.

Tusitake kuwalaumu wahindi kwa uzembe wetu.

Ni kweli kabisa, watz tumezidi kwa uzembe na kutojituma ktk kazi, maendeleo tutabaki kuyaona kwa wageni ndani ya nchi.

Ila kwa vile wahindi wana uwezo kimaisha kwanini wasipewe maeneo mengine yaliyowazi kama vile mapori yaliyoko Singida waakachenga kwa makubaliano maalumu ili nchi ikapendeza!!
 
Msechu ni mtu mwenye mshikamano na wahindi toka anafanya kazi bank , kwa hiyo mara alipokabidhiwa NHC basi ni wakati wake wa kulipa fadhila kwa wahindi jinsi walivyokuwa nae toka zamani. Huyu mtu badala ya kupandisha kodi ya nyumba za UPANGA yeye anaziuza. cha msingi ilikuwa kuzipandisha nyumba hizi bei ili shirika lipate fedha nyingi
 
Correction hapo... anaitwa Nehemiah Mchechu... Ameanza na kasi kubwa...
 
Huyo Mchechu sijui Msechu MD wa NHC naye keshaanza kuingiwa na tamaa na uroho kama Magufuri eeh!,yaani hajamaliza hata mwaka tayari keshaishiwa plans? Sometimes I feel sorry to these elite brothers like him,na ndio maana Mkapa aliwaleta Netgroup Solution kukusanya madeni ya Tanesco kwani Wabongo wakipewa high profile jobs performance becomes worse.
 
Hivi hawa wahindi wanatutafuta nini?
Ubaya ni kwamba wanawatumia watanzania wenye uroho wa fedha kutuhujumu.
Yani daktari wa muhimbili anaishi kiluvya wakati muhindi ananing'iniza miguu na kula pariki pale upanga,halafu tunajiuliza vifo vya kina mama na watoto vitapungua vipi.
Nchi hii?!!

lakini mkuu tukiangalia upande wapili wa shilingi zile nyumba nyingi utaona zemejengwa miaka ya 50`s kwa juu ina ajina.. zilikuwa za kwao kabla nyerere hajawapokonya ..
 
Wahindi wamo lakini pia nyuma yao kluna kundi la mafisadi, sasa wanataka kunyonya kila kitu mapaka nyumba. Haiwezekani Pro. Tibaijuka anapaswa kuonesha misuli, siyo kuogopana tena.
 
lakini mkuu tukiangalia upande wapili wa shilingi zile nyumba nyingi utaona zemejengwa miaka ya 50`s kwa juu ina ajina.. zilikuwa za kwao kabla nyerere hajawapokonya ..
ukiangalia vizuri serikali inaendeshwa na kodi zetu
 
kwa hatuna haja ya kuwalaumu wahindi haya yote ni ujinga wetu tusitafute mchawi kwa kuwalaumu wahindi.
 
Tuongee mengine tusongelee UBAGUZI- wao huo wanaujua na wanauabudu wana wahindi wenzao wanaowaita OUT CASTES na UNTOUCHABLES sasa hiyo iko wapi hapa. Kama wanweza kuwaita wahindi wenzao kwa majina haya na hawataki mjadala kuhusu hilo unafikiri wewe waatakuita nani. Tuongee mengine tuache hayo ya ubaguzi
 
Wewe ni nani alikukataza kuishi katikati ya jiji? Au gharama zimekushinda?

mimi ninaishi katikati ya mji,mdogo wangu anaishi msoga umeshawahi kuona muhindi anayeishi msoga au kijiji kinachofanana nacho?ukienda longido kuna wazungu,hawa wahindi wamerundikana upanga tu.
 
Habari zako za kinafik nafik. Hao wahindi hizo pesa walizitowa wapi? Au wao wanauwezo wa kuzitafuta zaidi yako? Majumba ya Upanga yalijengwa na wahindi na yakadhulumiwa na nyerere na wapangaji ambao si wahindi huziuza kwa shida zao za pesa.

Au hujui kuwa wengi wetu hata tukifiwa Dar basi hata kama kuuza flat tutauza ili tusafirishe maiti Kilimanjaro au Kagera au Mbeya? Au hujuwi kuwa wengi wetu tukiwa na kipaimara basi hata flat tutauza ili tukifanye cha nguvu? Au hujuwi kuwa wengi wetu tukimcheza mwari tutauza hata flat?

Ujinga wetu ndio maradhi yetu.

Wahindi ni wachapa kazi, wametoka walikotoka wakaanza kuuza bajia, chachamawa, kachori lakini tazama baada ya muda wako wapi? Na hausikii wanamcheza mtoto, wanakipaimara, wana harusi za kifahari, wana maziko ya kuleweshana. Wao kazi, kazi, kazi. Ndio maana unawaona wao ndio wana mafanikio. Wahindi huanza kula maraha wakishajijenga kimaisha na si kabla.

Tusitake kuwalaumu wahindi kwa uzembe wetu.

kama ni wachapa kazi si wangetusaidia sana na hii sera yetu ya kilimo kwanza?waende vijijini wakejenge uchumi, upanga wawaachie watumishi wa umma kama madaktari na watumishi wa wizara.

Mchapakazi hanenepi kama walivyo wahindi acha dhihaka wewe!
 
lakini mkuu tukiangalia upande wapili wa shilingi zile nyumba nyingi utaona zemejengwa miaka ya 50`s kwa juu ina ajina.. zilikuwa za kwao kabla nyerere hajawapokonya ..

kama walinyanganywa mbona mpaka leo wapo?
 
FaizaFoxy said:
Wahindi ni wachapa kazi, wametoka walikotoka wakaanza kuuza bajia, chachamawa, kachori lakini tazama baada ya muda wako wapi? Na hausikii wanamcheza mtoto, wanakipaimara, wana harusi za kifahari, wana maziko ya kuleweshana. Wao kazi, kazi, kazi. Ndio maana unawaona wao ndio wana mafanikio. Wahindi huanza kula maraha wakishajijenga kimaisha na si kabla.

FaizaFoxy,

..ulioleza ni kweli, but not the whole story.

..mafanikio ya kibiashara kwa kiasi fulani yanachangiwa na muendelezo wa colonial legacy.

..wakati wa ukoloni kulikuwa na sheria ya kuwazuia wazawa/native kupata mikopo kwenye mabenki au mahali popote.

..sheria ilikuwa inaelekeza kwamba ukimkopesha mzawa na akashindwa kulipa basi sheria haitakusaidia kwasababu mzawa/native ni mtu dhalili asiyekuwa na umakini kulingana na sheria za wakati huo.

..kwa msingi huo wakati wa ukoloni Mzungu alikuwa ni mtawala, Mhindi na Muarabu wakaachiwa watambe kwenye biashara, na sisi wazawa tukabakia kuhangaika kutafuta kodi ya kichwa na kuishi kwa kuchumia tumbo.

..in 1967, miaka 6 baada ya uhuru, Mwalimu Nyerere alileta azimio la Arusha ambalo naweza kusema lilikuwa pigo lingine kwa mzawa yeyote yule aliyejaribu kujiingiza ktk shughuli za biashara.

..kuna mambo ya KIHISTORIA na KISOSHOLOJIA ambayo inabidi kuyaangalia ili kuweza kuelewa kwanini WAZAWA tumeachwa nyuma ktk umiliki wa BIASHARA kubwakubwa.
 
Msechu ni mtu mwenye mshikamano na wahindi toka anafanya kazi bank , kwa hiyo mara alipokabidhiwa NHC basi ni wakati wake wa kulipa fadhila kwa wahindi jinsi walivyokuwa nae toka zamani. Huyu mtu badala ya kupandisha kodi ya nyumba za UPANGA yeye anaziuza. cha msingi ilikuwa kuzipandisha nyumba hizi bei ili shirika lipate fedha nyingi

Kama huna habari nyumba zote za NHC zimepanda bei na kila mkataba unapoisha zinazidi kupanda, uko wapi wewe?
 
FaizaFoxy,

..ulioleza ni kweli, but not the whole story.

..mafanikio ya kibiashara kwa kiasi fulani yanachangiwa na muendelezo wa colonial legacy.

..wakati wa ukoloni kulikuwa na sheria ya kuwazuia wazawa/native kupata mikopo kwenye mabenki au mahali popote.

..sheria ilikuwa inaelekeza kwamba ukimkopesha mzawa na akashindwa kulipa basi sheria haitakusaidia kwasababu mzawa/native ni mtu dhalili asiyekuwa na umakini kulingana na sheria za wakati huo.

..kwa msingi huo wakati wa ukoloni Mzungu alikuwa ni mtawala, Mhindi na Muarabu wakaachiwa watambe kwenye biashara, na sisi wazawa tukabakia kuhangaika kutafuta kodi ya kichwa na kuishi kwa kuchumia tumbo.

..in 1967, miaka 6 baada ya uhuru, Mwalimu Nyerere alileta azimio la Arusha ambalo naweza kusema lilikuwa pigo lingine kwa mzawa yeyote yule aliyejaribu kujiingiza ktk shughuli za biashara.

..kuna mambo ya KIHISTORIA na KISOSHOLOJIA ambayo inabidi kuyaangalia ili kuweza kuelewa kwanini WAZAWA tumeachwa nyuma ktk umiliki wa BIASHARA kubwakubwa.

Hizo sheria unazosema na huko kubanwa inawezekana kabisa ikawa ni hivyo wala sikata, kumbuka, Muingereza kaendesha hii nchi kwa kutubana kwa miaka mingapi? 40? na sisi toka tumejifunguwa katika huko kubanwa miaka mingapi? 49? wapi na wapi?
 
mimi ninaishi katikati ya mji,mdogo wangu anaishi msoga umeshawahi kuona muhindi anayeishi msoga au kijiji kinachofanana nacho?ukienda longido kuna wazungu,hawa wahindi wamerundikana upanga tu.

Hap ndipo uliponowa.
 
kama ni wachapa kazi si wangetusaidia sana na hii sera yetu ya kilimo kwanza?waende vijijini wakejenge uchumi, upanga wawaachie watumishi wa umma kama madaktari na watumishi wa wizara.

Mchapakazi hanenepi kama walivyo wahindi acha dhihaka wewe!

Wapo huko na mashamba yao utakaa kimya ukiyaona. Uliza uambiwe. Watumishi wa umma ndio waliowauzia wahindi hizo nyumba za NHC.

Kuna mmoja alinihadithia kisa kilichompata mara baada ya "kuikwaa" flat, mimi mwenyewe ilibidi nicheke, anasema alitembelewa na bibi yake kutoka kijijini, na siku ya tatu toka afike ikabidi amuulize mjukuu wake, "baba huku hamuendi chooni?, maana hii nyumba sioni choo", mjukuu akashangaa, akamuonesha yule bibi choo, bibi akamwabia "makubwa haya, mimi siku zote nilidhani kisima cha maji, na hayo maji ndio nilikuwa nayatumia kwa kunywa maana haya mnayoweka juu ya meza yabaridi sana yanaumiza meno".
 
Habari zako za kinafik nafik.

Au hujui kuwa wengi wetu hata tukifiwa Dar basi hata kama kuuza flat tutauza ili tusafirishe maiti Kilimanjaro au Kagera au Mbeya? Au hujuwi kuwa wengi wetu tukiwa na kipaimara basi hata flat tutauza ili tukifanye cha nguvu? Au hujuwi kuwa wengi wetu tukimcheza mwari tutauza hata flat?

Wahindi ni wachapa kazi, wametoka walikotoka wakaanza kuuza bajia, chachamawa, kachori lakini tazama baada ya muda wako wapi?

Ujinga wetu ndio maradhi yetu.

Tusitake kuwalaumu wahindi kwa uzembe wetu.

Kwenye red:
1. Kwa utafiti wako huo ni watu wangapi wameuza flat ili kusafirisha maiti Kilimanjaro, Kagera au Mbeya?
2. Ni watu wangapi wameuza flat ili kufanya sherehe za kipaimara?
3. Ni watu wangapi wameuza flat ili kumcheza mwana?

Kwenye blue:
4. Ni wahindi wangapi au ni muhindi yupi hasa aliyepata utajari kwa kuuza bajia, chachamawa, kachori?
5. Kuna uwezekano utajiri wa kutosha wa wahindi wengi haukupatikana kwa kuuza bajia, chachamawa au kachori? kama jibu ndiyo - ni biashara gani hiyo iliyowapa 'mapato' makubwa hivyo kuweza kufikia hapo walipo? Kama jibu ni hapana - basi rudia tena swali no 4.

It will be Interesting to hear your research findings!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom