Wahenga wetu na upeo wao

majorbanks

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
228
66
Wakuu
Nadhani neno wahenga wetu si geni sana miongoni mwetu na wengi wetu tumeshuhudia ukweli uliomo kwenye maono yao kupitia misemo,nahau,methali na mengine mengi.
Kuna wakati najiuliza,je hawa watu waliexist kwenye nchi yetu hii?
Na kama kweli walikuwa ni miongoni mwa Watanganyika,iweje leo hii nchi yetu imeshindwa kuwa na kizazi chenye chembechembe za upeo kama wao?
Upeo wao ni wa hali ya juu sana kiasi kwamba kulikuwa na nafasi ya nchi yetu kuwa mbali na hapa tulipo!!
 
Mkuu, majorbanks.
Uzalendo ni kitu muhimu sana kwa kila taifa duniani, ndio maana utaona baadhi ya viongozi wa mataifa au wanamichezo mathalani wakiimba wimbo wa Taifa wanatokwa na machozi, ule ni ujumbe tosha. Sasa hapa kwetu hatujui kuenzi vyakwetu angalia haya maneno mazito kwenye wimbo wetu wa Taifa, HEKIMA, UMOJA, NA AMANI. Kila mtoto wa miaka 5 na kuendelea angetakiwa awe anayajua kama sala, hapo hata kuwaenzi wahenga ingekua sio tatizo.
 
Back
Top Bottom