Wahariri wa Vyombo Vya Habari wafukuzwa Malaika Hotel Mwanza?

Nao wahariri walikubali kuondoka? kama waliondoka na hawatofungua kesi ya anti-discrimination wanastahili kufukuzwa mahali popote ambapo kuna uwezekano wa Ridhiwani kupita.

Nakubaliana nawe Mkuu, ilibidi wagome kufukuzwa mpaka kieleweke. Ridhwan hana haki zaidi ya kufikia hotel hiyo ukilinganisha na hao wahariri.
 
MAANA YA KUJENGWA IKULU KILA MKOA NI NINI?? huyo RIZMK.WERE ni KIMA KM VIMA WNGN HASTAIL KUPEWA HESHIMA KUBWA KIASI HICHO.
 
Nao wahariri walikubali kuondoka? kama waliondoka na hawatofungua kesi ya anti-discrimination wanastahili kufukuzwa mahali popote ambapo kuna uwezekano wa Ridhiwani kupita.
MMKJ hebu watu wachunguze jee hiyo Malaika Resort kweli ni ya yule Muasia Manooj Mehta? Naamini watu watapigwa butwaa watakapoujua ukweli.
 
Nawapongeza uongozi wa hotel pamoja na polisi kwa kuhakikisha riziwani anakuwa salama.

Watanzania wanamchukia huyu jamaa bila sababu ya msingi. Wanaweza hata kumdhuru.
 
Ni jambo geni lenye kuleta taswira isiyo na majibu sahihi. Pamoja na kwamba familia ya mkuu wa nchi hulindwa lakini si kwa kiwango hiki. Mtoto wa mkuu wa nchi hana kiwango cha kuchukua hoteli yote na kufukuza wabapangaji wengine, tofauti na mkuu wa nchi ambaye huwa na msafara mkubwa.

Kwa kawaida safari zenye kuhitaji uangalizi wa pekee hupangwa mapema, kama hoteli atakayofikia inaandaliwa mapema na hivyo uongozi wa hotel kutoa udhuru kwamba hoteli imekuwa over booked. Sasa hii ya kuwatimua watu waliokwisha chukua vyumba na kulipia eti kwa vile Ridhiwan anafikia hoteli hiyo ni kitu cha kushtusha, na kinajenga dhana ya Ridhiwani mwenyewe anavyojiweka mbele ya jamii kwa kutumia kivuli cha baba yake.

Tumeshakuwa na marais kadhaa nchini, na hata siku moja sijawahi kuona kiroja kama anavyojitokeza Ridhiwani mbele ya Umma wa Watanzania. Watu tumekuja kumfahamu mtoto wa mwinyi siku hizi, watoto wa Mkapa sijawahi kuona hata picha zao na shughuli zao, kwani ni mambo ya familia yao. Watoto wa Nyerere ndo kabisa, kuna siku pale dar nilishangaa kumwona dada mmoja akija kuniomba ushauri wa mambo ya uandishi wa vitabu, sikumjua mpaka mwenyeji wake aliponitambulisha kwamba ni mtoto wa Nyerere, yuko very simple na hana ulinzi wo wote na alikuwa kama tu nilivyo mimi na ninyi wenzangu.

Sasa huyu Ridhiwani nini mbele ya Watanzania kama si kujikweza kusiko hadhi yake. Nakubaliana na tamko la Kiongozi mmoja wa Umoja wa Vijana Arusha. Thats too much.
 
Nakubaliana nawe Mkuu, ilibidi wagome kufukuzwa mpaka kieleweke. Ridhwan hana haki zaidi ya kufikia hotel hiyo ukilinganisha na hao wahariri.

hawakufukuzwa bali walihamishwa kwasababu za kiusalama.
 
mkuu vyovyote vile lakini habari hii huwezi kumlaumu Ridhiwani...
mwenye hoteli alikuwa na mamlaka ya kukataa ugeni wa Ridhiwani na kutetea wateja wake wengine
tusikimbilie kulaumu watu tu.Kama yeye Ridhiwani yuko convinced anahitaji security
ya uhakika kwa maisha yake sisi wengine tunaweza vipi kusema hakuna haja ya hilo??????

wanaosema Ridhiwani ni nani ni wapumbavu, hata watoto wa Obama wanapewa security...
muhimu ni kuzingatia hiyo security iko vipi, cost zake,na ni vipi haitakuwa kero kwa wengine
kwa hili aliesababisha kero sio Ridhiwani ni wamiliki wa hoteli
Mkuu umenena vyema. mwanza kuna hotel kibao kama wanaona wamedhalilishwa si waisusie hiyo hotel!
 
Nawapongeza uongozi wa hotel pamoja na polisi kwa kuhakikisha riziwani anakuwa salama.

Watanzania wanamchukia huyu jamaa bila sababu ya msingi. Wanaweza hata kumdhuru.

Hakuna anayemchukia Ridhwan ila watu hawapendi kuona akitaka kutumia wadhifa wa Baba yake kama vile naye anashare katika wadhifa ule kwa kuingilia mambo mbali mbali ambayo hastahili kuyaingilia kama vile ya ndani ya chama cha magamba na pia kutumia wadhifa huo kufanya ufisadi wa kujilimbikizia mali.

Kama utakumbuka alitishia kufungua kesi dhidi ya Dr Slaa na Mtikila kwa kudai kuwa ana pesa nyingi ambazo hazijulikani amezipataje katika muda mfupi tangu amalize masomo yake, lakini hatujui kesi hiyo imeishia wapi.

Wahariri wa vyombo vya habari kamwe hawawezi kuwa na nia ya kumdhuru Ridhwan (Wamdhuru Ridhwan ili iweje!?) na ulinzi ulipo pale Malaika Hotel unatosha kabisa Ridhwan na wahariri kulala katika Hotel ile bila matatizo, kama management ya Malaika Hotel ingeona kuna sababu ya kuongeza ulinzi basi ingeweza kufanya hivyo bila ya kuwafukuza wahariri wa vyombo vya habari.
 
quote_icon.png
By The Boss
mkuu vyovyote vile lakini habari hii huwezi kumlaumu Ridhiwani...
mwenye hoteli alikuwa na mamlaka ya kukataa ugeni wa Ridhiwani na kutetea wateja wake wengine
tusikimbilie kulaumu watu tu.Kama yeye Ridhiwani yuko convinced anahitaji security
ya uhakika kwa maisha yake sisi wengine tunaweza vipi kusema hakuna haja ya hilo??????

wanaosema Ridhiwani ni nani ni wapumbavu, hata watoto wa Obama wanapewa security...
muhimu ni kuzingatia hiyo security iko vipi, cost zake,na ni vipi haitakuwa kero kwa wengine
kwa hili aliesababisha kero sio Ridhiwani ni wamiliki wa hoteli

Tusidanganyane hivyo, hawa watu wanakuja na full authority na kwa kupitia vyombo vya usalama kama ilivyotokea huko arusha, mwenye hotel ana ubavu wa kuwakataza? Don't blame hotel management.
 
Hakuna anayemchukia Ridhwan ila watu hawapendi kuona akitaka kutumia wadhifa wa Baba yake kama vile naye anashare katika wadhifa ule kwa kuingilia mambo mbali mbali ambayo hastahili kuyaingilia kama vile ya ndani ya chama cha magamba na pia kutumia wadhifa huo kufanya ufisadi wa kujilimbikizia mali.

Kama utakumbuka alitishia kufungua kesi dhidi ya Dr Slaa na Mtikila kwa kudai kuwa ana pesa nyingi ambazo hazijulikani amezipataje katika muda mfupi tangu amalize masomo yake. Wahariri wa vyombo vya habari kamwe hawawezi kuwa na nia ya kumdhuru Ridhwan (Wamdhuru Ridhwan ili iweje!?) na ulinzi ulipo pale Malaika Hotel unatosha kabisa Ridhwan na wahariri kulala katika Hotel ile bila matatizo, kama management ya Malaika Hotel ingeona kuna sababu ya kuongeza ulinzi basi ingeweza kufanya hivyo bila ya kuwafukuza wahariri wa vyombo vya habari.
Urais ni suala la kifamilia. mtoto wa mfalme naye ni mfalme. Alikuja hapa Chelsea Clinton watu wakafukuzwa hotelin hatukusema leo kwa Ridhwan imekuwa nongwa
 
Urais ni suala la kifamilia. mtoto wa mfalme naye ni mfalme. Alikuja hapa Chelsea Clinton watu wakafukuzwa hotelin hatukusema leo kwa Ridhwan imekuwa nongwa

Mbona Watoto wa Mwalimu walikuwa hawajikwezi kama huyu!? Kufukuza watu mahotelini eti kwa usalama wao!?
 
hawakufukuzwa bali walihamishwa kwasababu za kiusalama.

Je, walipewa option ya kuamua kubaki hotelini hapo au kuhama? Kama hawakuwa na hiyo option basi walifukuzwa, hata kama management inataka kulemba na ili ionekane kama walihamishwa.
 
Tusidanganyane hivyo, hawa watu wanakuja na full authority na kwa kupitia vyombo vya usalama kama ilivyotokea huko arusha, mwenye hotel ana ubavu wa kuwakataza? Don't blame hotel management.

sidhani kama mwenye hoteli naweza kulazimishwa 'ugeni huo 'kwenye hoteli yake
 
Sina hakika kama huyu kijana anaelewa maana ya haya matendo yake.

Kama ningeweza kumwona ningemuuliza swali rahisi sana. Ningemuuza kwamba,..."hivi ndugu Ridhiwani, unapanga kuishi nchi gani baada ya 2015?"!!!!
Labda lingenisaida kuelewa kwa nini anafanya hivi au kama anazushiwa tu!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Familia ya rais ni lazima ipewe ulinzi fikilia kama kuna baya lolote likimpata member wa familia ya rais lazima rais ataathilika ktk utendaji wake wa kazi labda kama tulalamike mambo aliyotoka kufanya huko alikotoka lkn ulinzi ni lazima

kwani sasa kaathiliwa na nn mbona utendaji wake unalalamikiwa hata waliokaribu naye. anyway hivo ndivo walivo watawala wa afrika. m7 alitoa ndege ya rais na waliz kumpeleka bint yake kujifungua majuu
 
Back
Top Bottom