Wahanga hawa wako wengi-Mama, mtoto wafia mapokezi ya hospitali kwa kukataliwa huduma

Unajua
inakuwa karaha sana mtu unapoambiwa ukweli vivyo hivyo kwa serikali yetu kutufu. kwa wale ambao ni wahanga wa kadhia hii wanajua uchungu wake na wanaamua kusimama front kulalama ili sauti isikike.

Kwa kuwa watawala wetu hawatibiwi hapa nchini hata kwa kagonjwa ka mafua tu, hivyo wala hawatishiki na kelele zetu.. sana sana wanatuonya tusiwasumbue wakati wanakula au la .........!!!!!!
 
Jamani Ya Hospitali Nyinyi Acha Tu. Hizi Hospitali Zetu Hasa Za Sirikali Wakati Mwingine Ni Machinjio. Shida Ni Sirikali Nzima Imeoza Hakuna Anayejari Afya Ya Mwenziwe Mradi Anajua 'nikiumwa Nakwenda Zangu India Au Uk Kwani Shida Iko Wapi?'
Huduma Katika Awamu Hii Ni Mbovu Sana Huko. Madaktari Sijui Ni Wachache Au Vipi Lakini Wala Hawaonekani Hata Opd.
Kwa Mfano Kule Bukoba Baba Yangu Ambaye Huwa Ana Attend Clinic Ya Sukari Kila Mwezi Mara Moja Aliniambia Huwa Wanapata Shida Sana Wale. Wakienda Pale Wanasubiri Daktari Wakati Mwingine Mpaka Saa 9 Jioni Kabla Hawajapata Huduma Wale.
Kwa Wale Wanaofahamu Taratibu Za Matibabu Ya Wagonjwa Hawa, Huwa Wana Fast Kwa Masaa Kadhaa Kabla Ya Kupimwa Na Kuonana Na Daktari Wake. Sasa Ebu Fikiri Mtu Mwenye Adha Hii Ya Ugonjwa Wa Sukari Na Anashinda Njaa Mpaka Saa 9 Ajala. Kweli Anakuwa Ametendewa Haki?
Wakiuliza Oh Mara Madaktari Wako Wodini, Oh Madaktari Ni Wachache, Oh Madaktari Wako Theater! Ili Mradi Kisingizio Hakikosi.
Sasa Ukisikia Kuna Mtu Kafa Kabla Ya Kuonana Na Daktari, Hiyo Si Hoja. Na Nakwambia Amini Usiamini Hakuna Anayejali. Ufe Shauri Yako.
Nimeambiwa Hata Daktari Wa Upasuaji Hayupo Pale Na Operations Zao Ni Za Mashaka Mashaka. Yupo Mmoja Walimfanyia Operation Ya Enia Na Wakasahau Kuziba Mshipa Mmoja Damu Ikawa Inavujia Ndani Ya Testacle, Na Hakuna Aliyekuwa Akijali. Fikiri Operation Ilifanyika Saa 8 mchana, Na Alilala Damu Ikitoka Sehemu Za Siri Mpaka Asubuhi tena akiwa na maumivu makali. Hakuna Aliyekuwa Akijali Maisha Ya Ndugu Huyu. Alipona Kwa Bahati Tu.
Lakini Ngoja Hawa Mafisadi Wanaojifanya Watawasaidia Hawa Wananchi Wakiumwa Homa Tu, Analipiwa Airticket Kwenda India.
Halllo Comeon Wizara Ya Afya, Hizo Pesa Mnazowalipia Hao Mafisadi Si Ndiyo Mgeboreshea Huduma Mahospitalini? Nakwambia Msicheze Hata Nyie Mtakufa Vibaya Kama Wanavyokufa Hawa Walioweka Imani Yao Kwenu Walaghai.
 
Wakubwa nimempoteza kichanga wangu kwa uzembe wa wauguzi, news kama hii inagusa sana moyo wangu... ninaomba kwa Mungu afanye mabadiliko makubwa ktk vichwa vya wauguzi na waganga

Waziri wa Afya proudly anataja orodha ya watoto na kina mama wanaokufa kwa matatizo ya uzazi halafu hafanyo juhudi zozote kuokoa hali hii.

AFYA NI HAKI YETU YA KIKATIBA LAZIMA TUIDAI

Mkuu kwanza pole sana,

Pili nimefurahi sana kuona unatambua haki zako za kikatiba, na napenda kusema kwamba chamsingi ni kumshinikiza Waziri wa Afya na Naibu wake wajue jinsi gani wananchi wanavyoona juu ya ufuatiliaji wa Afya za wananchi na matukio yanayotokea kwa uzembe wa ofisi zilizo chini ya wizara yao na utendaji wao kwa ujumla.

Mimi nafikiri sasa hivi cha msingi tukianza na jambo forum tuweke wazi haya kwa wananchi wote na pengine Magazetini kwa wale wenzetu waandishi waweke wazi HAKI ZA WATANZANIA KWENYE HUDUMA ZA AFYA NA HUDUMA NYINGI nafikiri itakuwa njia moja wapo ya kutoa elimu kwa kila mtu mpk vijijjini waweze kujua tunakwenda wapi.

Haiwezekani tuwe na watu wasomi wengi nchini wasiokuwa na msaada kwa jamii yetu hasa kwenye kutoa elimu bure kwa wananchi juu ya haki zao za msingi.

Narudi tena pole sana mkuu, ila sasa umefikia wakati WANANCHI WAJUE HAKI ZAO ZA MSINGI halafu uone mabadiliko yatakayotokea. Mimi naamini maisha bora nchi hii yanawezekana hasa kama mtu anajua haki zake za msingi za kikatiba.
 
Hi mentality ya "fulani must go" haitatufikisha popote.

Tuna systemic problem, tunahitaji a systemic solution.

CCM must go is more like it.Mwakyusa as a person may not be the problem and may actually be better than many a possible replacements, but what do you do when the entire system is plagued? You start an overhaul of the entire system, you do not change nuts and bolts.


Sawa kabisa tuna system problem maana CCM imeshindwa kubadilika ama kuboresha huduma. Huduma katika hospitali za serikali ni mbaya na kila mtu anajua hilo na hiyo hali haijatokea kwa bahati mbaya bali ni picha halisi ya UDUNI wa utendaji na ufanisi wa serikali yetu ya CCM. Serikali ya CCM haijafinikiwa kupanga. kusimamia vema na kuhakikisha matibabu kwa raia wake yanapatikana. Bila usimamizi wa CCM ambayo ipo madarakani sasa nani atasimamia ama nani atalaumiwa. TZ ni kama haina mwenyewe.
 
mie ninachojiuliza ingekua nchi nyingine waziri kweli na serikali nzimaa ingekua so silent abt haya??au ndo kwa sababu hamna mwanafamily wao yeyote anaweza face such things as wakiugua hata mafua wanago nje kutibiwa?
 
Jamani hata hakuna tamko lolote so far toka serikalini au ndio serikali ime freeze sababu sullivan??
 
Hi mentality ya "fulani must go" haitatufikisha popote.

Tuna systemic problem, tunahitaji a systemic solution.

CCM must go is more like it.Mwakyusa as a person may not be the problem and may actually be better than many a possible replacements, but what do you do when the entire system is plagued? You start an overhaul of the entire system, you do not change nuts and bolts.

Mkuu naona unataka kumtofautisha waziri wa afya na mfumo unaouzungumzia. mimi naamini kuwa yeye kama waziri wa afya anauwezo wakufanya mabadiliko hayo unayoyasema lakini mpaka sasa hajayafanya atwambie tatizo ni nini? Kwa taaluma yeye ni daktari hivyo shida na taabu za madaktari na manesi anazijua kwanini hafanyi hiyo "overhaul of the entire system"????
 
msikimbilie kusema hizi kazi ni wito wito tu,hivi kwenye pesa wapi pameandikwa wito??kila kazi ni wito mazee..
wewe unafikiri mtu atajitoaje kimasomaso kama kapesa anakopata ni ka duchu hakawezi kumtoa hata kwa wiki 2?Mbunge anapiga porojo bungeni anaondoka na lundo la fwedha,iweje watu muhimu kama hawa serikali haiwajali?Kama mpiga deki wa TRL analipwa mshahara mkubwa kuliko daktari aliyesota more than 5 years kula shule ngumu na katika mazingira magumu,huu wito utatoka wapi hapa?
Pale muhimbili kuna mpaka ma surgeon hawawezi hata ku afford ka mark 2 wanakwenda kazini kwa daladala,sasa hebu jiulize huyu mtu atakuwa na morali ya kazi kweli wakati anamuona jirani yake labba yuko tigo tu ana sukuma mashine.
msikimbilie kulaumu tu ndugu zangu

Mtarajiwa nakubaliana na wewe lakini pia naomba nitofautine na wewe, ina maana kama huridhiki na mshahara wako ndio usiijali kazi yako??? hii mimi hainiingi akilini kama mshahara haukutoshi unatafuta mahala pengine ambapo unaona pana maslahi zaidi lakini sio kusababisha vifo kwa watu wasionahatia kabisa.
 
Serikali ipo ktk fungate la uhuru hivyo masuala kama haya hayaistui.....
Ila wataongeza orodha ktk takwimu zao za vifo vya akina mama na watoto
 
Serikali ipo ktk fungate la uhuru hivyo masuala kama haya hayaistui.....
Ila wataongeza orodha ktk takwimu zao za vifo vya akina mama na watoto

unanikumbusha kitabu cha Mohammed Seif Khatib lenye jina hilo
 
Hivi mpaka iundwe task force ya kufuatilia haya mauaji ya kimya kimya ktk hospitali zetu???? Ni hospitali za serikali na private na ninamini kuwa kuna faida wanayopata kutokana na vifo vyetu....
 
Jamani hata hakuna tamko lolote so far toka serikalini au ndio serikali ime freeze sababu sullivan??

Hawana pressure maana aliyekufa aliwapa kura moja tu so kafa hawana kazi naye wanawafuata ndugu waliobakia kwa kofia ama tisheti then kura wanangoja mwingine afe .
 
Hawana pressure maana aliyekufa aliwapa kura moja tu so kafa hawana kazi naye wanawafuata ndugu waliobakia kwa kofia ama tisheti then kura wanangoja mwingine afe .

weee Lunyungu ohooo mie simo...

enewei nimefurahi kuandika hii post yangu ya 1,000 kwenye thread muhimu inayohusu uhai wangu na wako mchangiaji mwenzangu.

Jamani tusipofanya kitu tutaendelea kuuawa kimyakimya na wanaafya wanaolipwa kwa kodi zetu.....
 
Msanii hongera kwa bandiko 1000 mie sijakufikia kaka ama nimesha fika sijui.Ila hili la Serikali kuendelea na Sullivana na madaktari kusema hawaamini kwamba kuna uzembe ulifanyika inatisha sana unaweza kuchukua panga na kuwafuata na kuwamaliza LIVE .Ni dhuluma ya hali ya juu na kiburi .
 
Kuna ule usemi maarufu wanaoutumia hospitalini "waache madaktari wafanye kazi yao" ambapo uzembe wa kuchezea maisha ya walipa kodi unafanyika kwa kigezo cha nani katoa kitu kidogo....

Hivi hawa walumendago hawajui kuwa ahera hamna takrima???

Mkuu Lunyungu ktk post zako sijafika hata nusu yake
 
Back
Top Bottom