Wahandisi (contractors): Msaada tafadhali

JATELO1

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,230
301
WANA-JF;
Naomba kujua kuhusu mtaji (capital) unaohitajiwa na contractors Registration Board (CRB) ili kuweza kusajili kampuni ya ujenzi kwenye madaraja yake tofauti tofauti. Nimejaribu kutafuta taarifa hii kwenye website ya CRB lkn sijafanikiwa kuiona popote. Nimefanikiwa kuona tu kiwango cha contract amount ambao madaraja ya makampuni (class 7-class 1) haya yanaruhusiwa kufanya.

Pia nimeona taarifa ili kampuni iweze ku-upgrade toka daraja moja kwenda daraja la juu, ni lazima iwe na an improved capital, lkn haiko wazi ni kutoka kwenye kiwango gani ambao ulikuwa initial na ni kwa kiasi au kwa asilimia ngapi?

Hivyo naomba wale wenye uelewa katika hili wanisaidie tafadhali, kwani hii taarifa nahitaji sana. Naomba ufafanuzi ulenge haya yafuatayo;

1. Je, kampuni mpya ya ujenzi (civil works, building works, au civil and building works) inapoomba usajili kwa mara ya kwanza (mfano class 7) inatakiwa kuwa na capital-mtaji (hapa namaanisha pesa tu bila kuhusisha plants and equipments) kiasi gani?

2. Je, kama kampuni inahitaji ku-upgrade toka class moja kwenda class ya juu (mfano class 7 kwenda class 6) je inatakiwa kuwe na improved mtaji wa pesa (capital) kwa kiasi gani au kwa asilimia ngapi ya mtaji wa awali?

3. Je, inawezekana kwa mara ya kwanza ukasajili kampuni ya ujenzi kwenye class 6, 5, 4, 3, 2 au 1 badala ya kuanzia class 7? kama ndiyo je, upande wa mtaji (pesa) inatakiwa pia iwe kiasi gani? AU usajili wa kampuni ya ujenzi ni lazima ufuate mlolongo wa class 7, then class 6, then class 5, n.k?

NB: Naomba maelezo yazingatie tu

1.Usajili na upgrading ya makampuni ya wazawa (local contractors) tu na siyo makampuni ya kigeni.

2. Mtaji (capital) hapa iwe ni pesa inayohitajika kwa usajili au upgrading pale CRB na siyo assets zingine za kampuni.

Natanguliza shukrani.
TELO.
 
Kama ulivyoeleza hapo juu CRB ndiyo chombo kinachoshughulika na usajili ya makandarasi. Wao wako kwenye nafasi nzuri zaidi ya kujibu maswali yako. Tembelea ofisi zao ziko kila pende ya Tanganyika.(Tanzania Bara)
 
WANA-JF;
Naomba kujua kuhusu mtaji (capital) unaohitajiwa na contractors Registration Board (CRB) ili kuweza kusajili kampuni ya ujenzi kwenye madaraja yake tofauti tofauti. Nimejaribu kutafuta taarifa hii kwenye website ya CRB lkn sijafanikiwa kuiona popote. Nimefanikiwa kuona tu kiwango cha contract amount ambao madaraja ya makampuni (class 7-class 1) haya yanaruhusiwa kufanya.

Pia nimeona taarifa ili kampuni iweze ku-upgrade toka daraja moja kwenda daraja la juu, ni lazima iwe na an improved capital, lkn haiko wazi ni kutoka kwenye kiwango gani ambao ulikuwa initial na ni kwa kiasi au kwa asilimia ngapi?

Hivyo naomba wale wenye uelewa katika hili wanisaidie tafadhali, kwani hii taarifa nahitaji sana. Naomba ufafanuzi ulenge haya yafuatayo;

1. Je, kampuni mpya ya ujenzi (civil works, building works, au civil and building works) inapoomba usajili kwa mara ya kwanza (mfano class 7) inatakiwa kuwa na capital-mtaji (hapa namaanisha pesa tu bila kuhusisha plants and equipments) kiasi gani?

Kimsingi hakuna exactly amount amount ambayo kampuni inaweza kumention as Capital to start with,ilawaweza jikadilia kwamba incase unapewa project ya kwanza na unatakiwa kwa mwanzo mpaka utakapolipwa Advance it means kwa jengo labda uweze kuanza Foundation then ndo upewe Advance so Kadiria mwenyewe walau 30-50milion inaweza kuwa start-up capital.

2. Je, kama kampuni inahitaji ku-upgrade toka class moja kwenda class ya juu (mfano class 7 kwenda class 6) je inatakiwa kuwe na improved mtaji wa pesa (capital) kwa kiasi gani au kwa asilimia ngapi ya mtaji wa awali?

Utakapokuwa member utapata majawabu ya haya yote kwakuwa si pesa tu huwa ni kigezo cha wewe kuwa upgraded but kazi ulizofanya katika daraja ulilopo na kiwango(standard) cha kazi hizo na namna ulivyokuwa appreciated i.e kazi za serikali hutoa certificates of appreciation na kimsingi utafahamu zaidi once you are in the field.

3. Je, inawezekana kwa mara ya kwanza ukasajili kampuni ya ujenzi kwenye class 6, 5, 4, 3, 2 au 1 badala ya kuanzia class 7? kama ndiyo je, upande wa mtaji (pesa) inatakiwa pia iwe kiasi gani? AU usajili wa kampuni ya ujenzi ni lazima ufuate mlolongo wa class 7, then class 6, then class 5, n.k?

Unaweza hata kuanza na Class one ila ukidhi vigezo tajwa katika maelezo yao na Mtaji uwe ni hakika unajua huweza kumiliki crane na kuwa engineers as per uhitaji wa bodi na mengineyo halafu ukose let say 20bil just mfano,So ushauri wangu soma vizuri maelezo katika form zao na ujipime una nguvu za kuanzia Class gani na huwa ni nzuri zaidi pia kama na wewe ni mtaalam katika fani husika za ujenzi.

NB: Naomba maelezo yazingatie tu

1.Usajili na upgrading ya makampuni ya wazawa (local contractors) tu na siyo makampuni ya kigeni.

2. Mtaji (capital) hapa iwe ni pesa inayohitajika kwa usajili au upgrading pale CRB na siyo assets zingine za kampuni.

Natanguliza shukrani.
TELO.

kama vifaa tajwa kwa class husika unavyo tazama uwezo wako kuanzia 30 nakuendelea you will be considered bro.Ila mi si from board ila ni mdau ktk ujenzi.Karibu!
 
Correction,wahandisi ni engineers na wakandarasi ni contractors,kwani upo mbali na board kama unaweza kufika na kuongea nayo inakuwa rahisi,mi nilikuwa najua hyo ya contract sum na equipments ila pia kukua kwa daraja inategemea aina za kazi ulizofanya na experience
 
ahsante ndugu yangu kwa marekebisho. Ni kweli nilimaanisha Wakandarasi (Contractors). Tatizo ni kwamba niko nje ya nchi kwasasa, hivyo sitaweza kufika kwenye ofisi zao ndiyo maana nimeomba msaada kwa mwenye taarifa hizo. Pia sina mpango wa kuanzisha kampuni, bali kuna study nafanya katika eneo hilo ndiyo maana nahitaji hizo taarifa hasa za mitaji (pesa) ya Wakandarasi wazawa.
 
Back
Top Bottom