Wahamiaji haramu -Tanzania

Mayolela

JF-Expert Member
Sep 21, 2009
384
6
Hii ni kero yangu,naomba wahusika wahifuatilie.Wapo Wakenya,wamalawi ,wachina wengi sana hapa Dar,wakifanya kazi bila kuwa na permit yoyote zaidi ya kuwa na line ya safaricom na vodacom ili kuwasiliana na ndugu zao huko makwao.
Waziri Masha futilia jambo hili.taarifa tunapeleka ofisi ya Uhamiaji makao makuu ,hata ofisi ya mkoa opp. na shoprite lakini baada ya siku 2 watuhumiwa uwachiwa baada ya kutoa mlungula mzito.
Hebu watoe taarifa ya wageni waliopo nchini na wanafanya kazi bila vibali.
Waondoeni hii ni nchi yetu -warudi kwao,tena basi ni watu wenye roho tofauti na sie watanzania.
Naomba niwasilishe.
 
Ni aibu kubwa sana kuona watanzania tumesahau utu na utanzania wetu ambao mwalimu aliujenga kwa kupiga vita vitu kama rushwa na leo hii tunauharibu kwa kukumbatia rushwa.Hili soma la kuwa rushwa ni adui wa haki na maendeleo naona bado halijaeleweka.
Tunatakiwa tujichunguze ni wapi tumetoka,tulipo na ni wapi tunaeleke?
 
Back
Top Bottom