Wahadhiri vyuo vikuu vya umma kugoma

Jamani leo ni tarehe 27/4 ambayo wahadhiri waliahidi kugoma wamefanya hivyo? au zilikuwa kelele za mlango, mwenye taarifa zaidi atujuvye au mtu yeyote aliye karibu na vyuo hivyo atupe taarifa nini kinaendelea.
 
Mkuu, wamegoma, kwamba wameonewa vyakutosha, wamenyonywa vya kutosha, sasa wanataka mapinduzi!

Hayo waliyasema baada ya Jaji warioba ambaye ni mwenyekiti wa kanseli ya chuo kuja kuwasihi wasitishe mgomo! ambao baadhi pia walidai ushauri wake umechelewa ni sawa na kuokoa mtoto aliye kwisha fariki kwa kuzama!

Kikubwa hasa, kwamba waziri kiongozi kasema swala hilo la mafao ni la kisera ambalo linahitaji uamuzi wa baraza la mawaziri ambao haijulikani watakaa lini?

Kwa mtaji huo wamekubaliana kugoma mpaka hapo serikali itakapo pata nafasi ya kukaa kuwapa ufumbuzi wa madai yao.

Hii ndiyo habari!
 
Kama ni kweli basi wameandika historia! wasomi wetu wakati mwingine wamekuwa waoga na makuwadi wakubwa! Nawapongeza sana pamoja mnaweza msiogope vitisho nyie ni learned minority wengine tutawafuata
 
Kama ni kweli basi wameandika historia! wasomi wetu wakati mwingine wamekuwa waoga na makuwadi wakubwa! Nawapongeza sana pamoja mnaweza msiogope vitisho nyie ni learned minority wengine tutawafuata

Kweli mkuu. Hawa jamaa wametia aibu kwa muda mrefu. Ngoja tuone kama watamudu kasheshe za mgomo. Kama wao wameumbwa kwa kuta za mayai basi hapa kitaeleweka.
 
Ulie tu. Aliyebadili ni William Ngereja, ngosha mzembe aliyebanwa kama mjusi kwenye mlango hapo juzi mjengoni. Hakuwa na jinsi ya kujitetea wala kuomba utetezi kwa Kikwete kwa sababu Kikwete alikuwa kakwama na moshi wa Volcano Ulaya. Natamani ule moshi uanze tena siku akisafiri na udumu hadi uchaguzi uishe. Kukosekana kwake siku chache tu, kumeleta sheria nzuri ya madini. Akikosekana milele itakuwaje?

Mkapa kama si uwezekaji wa kijinga na kuuza mashirika na pia WIZI wake alioufanya mwisho, sasa hivi angelikuwa na heshima kubwa kama NYERERE. Wote wasubiri siku watakuja kuanza kupanda kizimbani kama walivyowapandisha wenzao akina Mramba. CCM oyeeee, Kiwete oyeeee, moshi wa volcano oyeeee.....

NB: Mbona unawachukia sana Wakatoliki? Ehhh, kuna Padri alikufanyia kale kamchezo nini? Wahi na wewe uombe Mamilioni kwa PAPA wa Kijerumani. Unaweza kuambulia walau ki-VX 6 kipya :)

Mkapa ujinga wake mkubwa alikuwa akiwasikiliza wezi wenzake kutoka kanisani..

NB: Mbona unawatetea sana Wakatoliki? ehhh na kuwasifia wewe ni chakula ya maaskofu na mapdre nini? endelea kuwatetea maana wanakufanyia kale -kamchezo kachafu pole.
 
Mkuu, wamegoma, kwamba wameonewa vyakutosha, wamenyonywa vya kutosha, sasa wanataka mapinduzi!

Hayo waliyasema baada ya Jaji warioba ambaye ni mwenyekiti wa kanseli ya chuo kuja kuwasihi wasitishe mgomo! ambao baadhi pia walidai ushauri wake umechelewa ni sawa na kuokoa mtoto aliye kwisha fariki kwa kuzama!

Kikubwa hasa, kwamba waziri kiongozi kasema swala hilo la mafao ni la kisera ambalo linahitaji uamuzi wa baraza la mawaziri ambao haijulikani watakaa lini?

Kwa mtaji huo wamekubaliana kugoma mpaka hapo serikali itakapo pata nafasi ya kukaa kuwapa ufumbuzi wa madai yao.

Hii ndiyo habari!
Thanks Rwabugiri tusubiri kama serikali itawapelekea FFU kama inavyowafanyia wanafunzi wanapogoma
 
Mkapa ujinga wake mkubwa alikuwa akiwasikiliza wezi wenzake kutoka kanisani..

NB: Mbona unawatetea sana Wakatoliki? ehhh na kuwasifia wewe ni chakula ya maaskofu na mapdre nini? endelea kuwatetea maana wanakufanyia kale -kamchezo kachafu pole.

Wacha kuharibu thread na nyinyi na udini wenu,

Hapa tunaongelea swala nyeti, la wasomi waliobobea nchini kuamua kugoma kuwafundisha vijana wetu ambao ndo tegemeo la taifa siku za usoni. Hawa wasomi wanaelewa fika madhara makubwa yatakayo tokea kwa kuacha kwao kufundisha., lakini longolongo la ahadi hewa zinazotolewa kisiasa kwa zaidi ya myaka kumi zimewafikisha hapa!

Leteni hoja za kusaidia kuondoa hili tatizo badala ya kuendekeza udiniiiiii kila mahali, kila jambo liwe na wakati wake please!
 
Mkuu, wamegoma, kwamba wameonewa vyakutosha, wamenyonywa vya kutosha, sasa wanataka mapinduzi!

Hayo waliyasema baada ya Jaji warioba ambaye ni mwenyekiti wa kanseli ya chuo kuja kuwasihi wasitishe mgomo! ambao baadhi pia walidai ushauri wake umechelewa ni sawa na kuokoa mtoto aliye kwisha fariki kwa kuzama!

Kikubwa hasa, kwamba waziri kiongozi kasema swala hilo la mafao ni la kisera ambalo linahitaji uamuzi wa baraza la mawaziri ambao haijulikani watakaa lini?

Kwa mtaji huo wamekubaliana kugoma mpaka hapo serikali itakapo pata nafasi ya kukaa kuwapa ufumbuzi wa madai yao.

Hii ndiyo habari!

Hongera zao...TUCTA jamani nanyi fanyeni kweli.
 
safi sanaaaaaaaaaa wahadhiri!watakuwa wametusaidia sisi wote wananchama wa hiyo mifuko ya kiubabe na kitapeli.nina hakika mafao yakiboreshwa yataangalia scales za mishahara na si wahadhiri pekeee,bravoooooooooooooooo!tunasubiri tarehe tano ya TUKTA.
 
Wahadhiri wamtilia ngumu Warioba, wasisitiza kugomaTuesday, 27 April 2010 21:14

WAHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana walimshambulia mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, Jaji Joseph Warioba alipotaka kuwatuliza ili wasisitishe mgomo walioupanga.

Wahadhiri hao, wakionekana kuwa na jazba, walikataa ushauri wa Jaji Warioba na kusema kuwa maneno yake ni mepesi na hayana uzito wowote.

Wahadhiri hao wameamua kugoma baada ya kuona serikali imeshindwa kushughulikia madai yao ya kutaka kuboreshwa kwa mafao ya wastaafu ambayo yanatolewa na Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma (PPF) na ule wa wafanyakazi waandamizi (Senior Staff Superannuation Scheme, SSS).

Pia wanataka menejimenti za vyuo vikuu ziwaruhusu waajiriwa wapya kujiunga na mifuko mingine ya pensheni wanayoitaka kama LAPF.

Jana Jaji Warioba alikwenda kwenye mkutano wa wahadhiri hao wa vyuo vikuu ulioitishwa kwenye ukumbi wa Cafeteria 1 ulio UDSM ili kutoa taarifa ya kura za maoni kuhusu mpango wa mgomo huo na akatumia fursa aliyepewa kuwashauri wasomi hao wasitishe kutekeleza azma yao ya kugoma na kuwaelezea athari zake.

“Tunakubali kuwa suala hili limechukua muda mrefu kushughulikiwa, lakini kwa jinsi katibu mkuu kiongozi alivyolishughulikia katika miezi minne na nusu tu hadi kufikia kupeleka waraka kwa Baraza la Mawaziri, tunaamini halitachukua muda mrefu tena kuamuliwa,” alisema Warioba.

“Wanataaluma wanatakiwa kuwa na subira; kama mmeweza kusubiri kwa miaka takribani kumi, msikate tamaa bali mvute subira kwa miezi miwili, mitatu ijayo ili serikali ikamilishe azma yake.”

Baada ya Jaji Warioba kutoa maoni yake kuhusu mgomo huo aliomba kuondoka bila kusikiliza maoni ya wahadhiri hao huku mwenyekiti wa Chama cha Wahadhiri wa UDSM (Udasa) akimuomba asikilize maoni ya wajumbe.

Lakini Warioba hakutaka kuendelea na kikao hicho na badala yake akaomba ashirikishwe kwa kupewa taarifa za kikao iwapo watapanga kukutana.

Baada ya Jaji Warioba kuondoka kwenye ukumbi huo, wahadhiri hao waliendelea na kikao ndipo mwenyekiti wa Udasa, Dk Damas Nyaoro alipotoa fursa kwa wajumbe kuchangia ushauri wa waziri mkuu huyo wa zamani.

“Maneno ya Warioba yote ni mepesi, hayana uzito wowote. Kama wameshindwa kutoa suluhisho la tatizo ndani ya miaka kumi itakuwaje katika miezi miwili? Sisi si watoto wadogo,” alisema mmoja wa wahadhiri.

Alisema wamesikitishwa na kitendo cha Warioba kuondoka kabla ya kusikiliza maoni yao kwa sababu walihitaji awepo apo ili wampe maneno yao.

“Ningefurahi sana kama Jaji Warioba angekuwepo hapa ili asikilize maoni, ila naomba mfikishie sisi tutagoma kama tulivyopanga hii ni kutokana na makubaliano ya vyuo vyote,” alisisitiza mmoja wa wahadhiri hao.

Wahadhiri hao walisema suala lao lisiwekwe kisiasa bali wanachohitaji ni utekelezaji na siyo ahadi hewa.

“Serikali imechelewa sana, pia haina nia njema na wanataaluma na anayetaka kuahirisha mgomo, aahirishe kichwani mwake na si kuwashauri wajumbe,” alisema mhadhiri mwingine.

Akitoa taarifa za mpango wa mgomo huo, Dk Nyaoro alisema wahadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (Duce) wameazimia kugoma kwa asilimia 100, Chuo Kikuu Cha Dodoma (Udomasa, 98%) na Udasa asilimia 95.

Alitaja vyuo vingine kuwa ni Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (Sua) 95%, Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Mkwawa (Mkwawa) 92%, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara Moshi (Mucobs) 89%, Chuo Kikuu cha Ardhi (Arisa) 85% na Chuo Kikuu cha Mzumbe 75%.

Alisema kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Out) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) havikuweza kuwasilisha mapendekezo kuhusu mgomo huo.

Dk Nyaoro alisema mgomo huo, ambao ulianza rasmi jana, unashinikiza madai mbalimbali ya wahadhiri baada ya kuchoshwa na ahadi hewa zinazotolewa na serikali kuhusu malipo hayo.

“Aprili 9 mwaka huu tulikutana baadhi ya wanataaluma wa vyuo mbalimbali vya umma na katika mkutano huo tulifikia uamuzi wa kufanya mgomo, lakini kwa kuzingatia kutokuwepo kwa baadhi ya wahadhiri tuliamua viongozi wao wapeleke uamuzi huo ili waweze kushirikishwa,” alisema Dk.Nyaoro.

Alifafanua kuwa mgomo huo utakuwa wa kusitisha kufundisha pekee lakini kazi nyingine za kiofisi zitaendelea kama kawaida.
 
Hongereni sana Wahadhiri. Hii bila shaka itawapa nguvu TUKTA kuendeleza mgomo wao pia. Na hatimaye labda wananchi wanaweza kujifunza kwamba haki zao haziwezi kuja kwa kulalamika tuuuu. Katika mfumo wa kifisadi kama uliopo TZ, hatua madhubuti kama hizi ndiyo zitatuokoa.
 
Kama ni wasomi wenye credentials zilizokamilika kwa nini wasitafute ajira kwingine? Kuna haja gani ya kuikamua nchi ambayo haina hata kipato cha kuwanunulia watoto wa shule madawati ? Ubinafsi umeota mizizi sana tz

Sometimes don't be cynic!
Mtanzania yeyote ana haki ya kudai haki yake badala ya kukimbilia kwingine.

Maoni yangu ktk hili nadhani serikali yetu ni kama club ya walevi wanaoamua hata kuimba matusi kwa pamoja.

Mifuko hii ya hifadhi ya jamii (hasa PPF) imelalamikiwa na watumishi kwa muda mrefu sana bila majibu. Ni mifuko ya hifadhi ya jamii, ni mingi kwa nini PPF tu ndo ionyeshe upuuzi kama huo na iachwe hivyo hivyo?

Pamoja na kwamba ni mgomo wa vyuo vikuu, hapo Tanzania kila aliye na uhusianao wa pensheni na PPF ni kilio tu. Ina maana watumishi wote wa mashirika ya umma.

Yasemekana PPF wanaitegemea serikali iwasaidie mgogoro huu kwa sababu hawana pesa. Pesa nyingi zimechukuliwa na serikali kujenga majengo ya kifahari bila hata mikataba (ref. Mh Zitto). Bahati mbaya zaidi hata palipo na mikataba bado serikali hailipi madeni kwa kuamini ilichukuwa toka chombo cha serikali. Haioni sababu za kulipa madeni ya mifuko hii.

Niliwahi kuambiwa mifuko hii ni kama mfuko chakavu wa vikao vya harusi hapo Bongo. Wanachukua pesa kila wakijisikia kufanya hivyo. Lakini ktk yote haya wastaafu wanapunjwa bila sababu za msingi tena kwa nguvu na vitisho.

Naamini mgomo huu ni hatua ya mwisho baada ya kukosa mbinu mbadala. Huyo anayeitwa Rais yabidi pia aambiwe kwamba maisha bora siyo kwa wanasiasa tu!
 
Mkuu hapo umeliweka vyema, manake inaonekana kuwa mwana siasa bongo ndo kila kitu. Fani zingine zooote hazithaminiwi isipokuwa wana siasa, ambao wao kuijiongezea masurufu haaiitaji kubadili sera za nchi, kwa wengine ukigusa tu, unaambiwa sera, sera mbona kwa wana siasa hazifanyi kazi?

Nashangaa awamu ilo pita wabunge walilipwa mil 25, awamu hii nasikia zimeongeza hadi kuwa 45, hiyo mbona hatukusikia ikihitaji kusubili sera?

Nadhani kuna umuhimu wa watanzania wote kuamuka kudai haki zetu toka kwa wanyonyaji "wanasiasa" Lazima masurufu ya wastaafu wote, wawe wanasiasa kuanzia wabunge, mawaziri, ama watendaji wa serikali ama wafanyakazi wowote wale yawe na uwiano, kiwepo chombo maalumu cha kupanga na kuratibu huu mfumo! Hii ya wanasiasa kujipangia wanavo taka wao ni unyonyaji na kudhalilisha fani zingine zote nchini ilihali ndizo mihili mikuu!
 
Aibu nyingine hii, kama wasomi wameshindwa kugoma sababu ya ubinafsi je hao walala hoi wataweza? Tanzania kuwa huru bado sana!!
 
Thursday, 29 April 2010 21:30 0diggsdigg

Mussa Mkama na Ummy Muya

MGOMO wa wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma na vishiriki, umeyeyuka.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mgomo huo umeyeyuka kutokana na mvutano ulioibuka baina yao na kutengeneza makundi yanayovutana, moja likiubeza na jingine likiunga mkono.

Jana wahadhiri hao walilazimika kupiga kura ili ya kupata maoni mapya kuhusu mgomo huo matokeo na matokeo yalionyesha kuwa wahadhiri 161 walitaka mgomo usitishwe, wakati wengine 69 walitaka uwepo na mtu mmoja hakuegemea upande wowote.

Katika kikao kilichofanyika usiku wa kuamkia jana, katibu mkuu wa Menejimenti ya Utumishi ya Umma, George Yambesi alisema hakuna sababu za wahadhiri kugoma kwa sababu mgomo huo ni batili kutokana na kutokufata kanuni na taratibu za kutatua tatizo lao.

Alisema kama ni lazima wahame katika mpango wa mafao duni na mfuko wa wafanyakazi waandamizi (Senior Staff Superannuation Scheme, SSS) na kujiunga na mfuko mwingine, serikali ni lazima itafute fedha kwanza kisha ziingizwe katika mfumo wa bajeti ya serikali.

“Lazima serikali itafute fedha kwanza kasha ziingizwe katika mfumo wa bajeti ndipo utatuzi upatikane,” alisema Yambesi.

Uamuzi wa kufanya mgomo ulioshindikana jana, ulifikiwa katika kikao cha wahadhiri kadhaa wa vyuo vikuu vya umma kilichofanyika Aprili 9 mwaka huu jijini Dar es salaam ambako wadhiri 415 waliunga mkono mgomo dhidi ya 22 ambao hawakuafiki.

Kuwepo kwa makundi miongoni mwao ndiyo kulilopelekea mgomo huo kuwa na mvutano wa chini kwa chini uliosababisha mwenyekiti wa Udasa, Dk Damas Nyaoro kuonekana mchochezi wa mgomo huo.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema kuwa hatua ya kupiga kura ilichukuliwa baada ya Dk Nyaoro kushutumiwa na baadhi ya wahadhiri kuwa ndiyo anayechochea mgomo, jambo ambalo alipingana nalo akisema kuwa uamuzi huo ulichukuliwa na wahadhiri wote na akataka kujivua madaraka, lakini baadaye akakubali maombi ya wajumbe na ikabidi zipigwe kura.

Habari hizo zinasema kikao hicho kiliitishwa na Dk Nyaoro ili atangaze kujiuzulu wadhifa huo baada ya kusikia tuhuma dhidi yake kuwa anachoichea mgomo.

Wahadhiri walifikia uamuzi wa kutangaza mgomo kutokana na kile walichoeleza kuwa wachoshwa na ahadi hewa zinazotolewa na serikali kuhusu malipo ya madai yao.

Hii ni mara ya pili kwa wahadhiri hao kutishia kufanya mgomo ili kuishinikiza serikali itekeleze madai yao. Mara ya kwanza walitishia kugoma Oktoba mwaka jana.

Wahadhiri walioazimia kugoma ni kutoka Chuo cha Sayansi ya Afya na Tiba cha Muhimbili, Chuo cha Ualimu Chang’ombe (Duce), Mkwawa (Muce), Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua), Chuo Kikuu cha Mzumbe (Mu) na Chuo cha Ushirika Moshi.

My comments:
Habari nyepesi nyepesi kutoka Mlimani zinasema Deans ndio "wachawi" wa mgomo huo maana tangu mwanzo waliwatisha wahadhiri na kudai kwamba mgomo ni batili na wanapaswa kuendelea na kazi.
 
Kugoma kwa ajili ya maslahi yako binafsi sio jambo la kiungwana wala kishujaa, these people are self centred.

Watanzania wangapi hawana uhakika wa kula, watanzania wangapi wanakosa matibabu kwa ajili hawana pesa za kulipia matibabu, watanzania wangapi hawana ajira, watanzania wangapi wanashidwa kuwalipia school fees+uniforms watoto wao. Sasa hawa wasomi wenye mishahara mizuri na wengi wao wamesomeshwa bure na Watanzania hawa masikini bado wanagoma eti pension zao ziboreshwe ndio watafanya kazi(kazi ya kulipwa sio bure).

Mimi nilitegemea hawa wasomi wange goma siku nyingi hasa wakati serikali inaondoa sera ya free education kwenye higher institutions. Hawa wasomi nilitegemea wangeweza kubuni mikakati kabambe ya kuondoa umasikini uliokithiri kwenye nchi yetu na kugoma kama serikali ingeshindwa kuitekeleza, sasa hawa tunaotegemea wasaidie Taifa hili nao wanagoma tena kwa ajili ya manufaa yao binafsi. Hii ni hatri kubwa.
 
Wahadhiri wamefarakana kuna makundi, naambiwa kuna waliogoma na wengine wamekumbuka wake zao na watoto wameamua kususia mgomo! Kumbukeni hao ni wasomi wanatoa chicken reasoning! Wasomi wa Tanzania na wafanyakazi wa reli (TRC) ama wale wa Jumuiya ya Africa Mashariki hakuna tofauti?
 
Mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma uliodumu kwa takribani wiki nzima sasa umekwisha rasmi leo, na hivyo basi kuanzia jumatatu wahadhiri hao wataanza kuingia madarasani na kufundisha kama kawaida. Kwa habari za kuaminika ni kuwa wahadhiri wamesitisha mgomo huo baada ya Waziri mkuu Pinda kuwahakikishia kuwa madai yao yanashughulikiwa na serikali na watapata majibu kabla ya bunge kuvunjwa rasmi mwezi wa saba!
 
Kilembwe,

Tuamnini kuwa madai ya Wahadhiri wetu yatashughulikiwa kabla ya Bunge kuahirishwa. Sioni kwanini Inapofika kwenye haki ya msingi inashindikana kujadiliana kwa misingi ya Sheria tuliyojiwekea.

Nawapongeza Wahadhiri kwa hatua yao ya kijasiri, nadhani sasa kweli saa ya ukombozi imekaribia hapa tulipofika. Haina mantiki gratuity ya Wabunge, inakuwa tayari siku Bunge inapoahirishwa, wakati wazee wetu na watumishi wengine lazima wahangaike mpaka soli zinaisha. Wahadhiri wamekuwa kimya wakati wa saga za wenzao, naamini nao pia wataunganisha nguvu na jamii nzima ili kuunganisha nguvu.

Tukumbuke haki hizi ni maisha na ni uhai, hivyo hakuna sababu ya kuzitazama kwa msingi wa kiitikadi. tushikamane kutafuta tatizo liko wapi na kwanini haki hizi ambazo ziko wazi zinashindikana kupatikana kwa njia za kawaida? Wahadhiri wangelitusaidia sana hapa kufanya analysis siyo ya kwao tu, lakini hasa kutafuta tulipokosea ni wapi ili kila kada ipate haki zake inazostahili.
 
Back
Top Bottom