Wagombea udiwani CCM wabwagwa

Msongoru

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
306
24
na Anna Makange, Tanga

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepata pigo baada ya wagombea wake wawili waliokuwa wakiwania udiwani katika Kata ya Ngamiani Kati na Chongoleani, wilayani hapa kubwagwa kwenye uchaguzi mdogo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi, Chama cha Wananchi (CUF) kilipata ushindi kwa wagombea wake kuongoza katika kata zote mbili.

Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana kuhusiana na uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya ya Tanga, Paul Baruti, alisema mgombea aliyeshinda ni Nabahan Habib wa CUF aliyepata kura 634, akifuatiwa na Mohamed Thabit wa CCM aliyepata kura 391 na Aziz Mahadh wa CHADEMA aliyepata kura 112.

Alisema waliokuwa wamejiandkisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Ngamiani Kati ni watu 4,070, waliojitokeza kupiga kura walikuwa 1,145 wakati kura halali zilikuwa 1,138 na saba ziliharibika.

Kwa upande wa Kata ya Chongoleani alisema mgombea Ali Ng'anzi wa CUF alishinda kwa kupata kura 567 kati ya kura halali 1,121 zilizopigwa na kumshinda Hamis Jasho wa CCM aliyepata kura 454.

Uchaguzi huo mdogo umefanyika ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na aliyekuwa diwani wa Ngamiani Kati, Salimu Akida (CUF) aliyehamia nchini Marekani mwaka 2006.

Uchaguzi katika Kata ya Chongoleani ulifanyika baada
 
na Anna Makange, Tanga

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepata pigo baada ya wagombea wake wawili waliokuwa wakiwania udiwani katika Kata ya Ngamiani Kati na Chongoleani, wilayani hapa kubwagwa kwenye uchaguzi mdogo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi, Chama cha Wananchi (CUF) kilipata ushindi kwa wagombea wake kuongoza katika kata zote mbili.

Alisema waliokuwa wamejiandkisha kwa ajili ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Ngamiani Kati ni watu 4,070, waliojitokeza kupiga kura walikuwa 1,145 wakati kura halali zilikuwa 1,138 na saba ziliharibika.

Kwa upande wa Kata ya Chongoleani alisema mgombea Ali Ng'anzi wa CUF alishinda kwa kupata kura 567 kati ya kura halali 1,121 zilizopigwa na kumshinda Hamis Jasho wa CCM aliyepata kura 454.

Uchaguzi huo mdogo umefanyika ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na aliyekuwa diwani wa Ngamiani Kati, Salimu Akida (CUF) aliyehamia nchini Marekani mwaka 2006.

Uchaguzi katika Kata ya Chongoleani ulifanyika baada

mwanzo wa safari hatua, taratibu macho ya wadanganyika yameanza fumbuka tutafika siku moja kujinasua mikononi mwa mafisadi. Bravo wana tanga
 
hizi ni habari nzema kwa watu wote wenye kulitakia mema taifa hili,kuwa sasa watnganyika wameelewa kuwa nchi hii imawezekana kabisa tukawa na mitazamo tofauti katika kulijenga taifa letu
 
Hili ni jambo jema lakini kama upinzani unataka kupata ushindi wa kuwatosha 2010 ni lazima washikamane ukweli kweli sio kuwe na mgombea kutoka kila chama hatutafika kwa style hii kusanyeni nguvu zenu muone matunda yake hasa kwenye viti vya ubunge na udiwani
 
Uchaguzi huo mdogo umefanyika ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na aliyekuwa diwani wa Ngamiani Kati, Salimu Akida (CUF) aliyehamia nchini Marekani mwaka 2006.
Huyu Salimu alikuwa na nia ya kweli ya kugombea udiwani au alikuwa anatafuta nauli tu.... hii inaweza kuwa aina nyingine ya ufisadi
 
CUF wapo makini hawa ndio wapinzani wa kweli hao Chadema bosheni tuu....
 
Hapo umekosea, nilitegemea useme kuwa CUF na CHADEMA ndio vyama makini na CCM lazima iondoke. Kwa nini sisi kwa sisi tunashambuliana? kama tuna nia ya ukombozi kweli ni lazima tukubali kwa kauli kuwa tunaye adui mmoja naye ni CCM, of course na vibaraka wake kama Mtikila. Pongezi CUF na pongezi CHADEMA ma-champion wa vita dhidi ya ufisadi.
 
Wewe na nani?
 
Tanga wameshajua kinachoendelea sasa.
Hongera watu watanga pamoja na mimi ;-)
 
Back
Top Bottom