Elections 2010 Wagombea hawaruhusiwi kuwa mashahidi katika kuhesabu kura?

Masauni

JF-Expert Member
Aug 15, 2010
386
58
Kama tunavyojua ni ukweli usiopingika kuwa CCM itatumia mbinu nyingi kutaka kuiba kura ili ionekane imeshinda. Nakumbuka mwaka 1995 wakati Balozi paul ndobo akigombea jimbo la musoma kupitia NCCR-Mageuzi. CCM walipoona kwamba Paul ndobo ameshinda walienda katika kituo cha kuhesabia kura na kutaka kubadilisha matokeo. Thank God Paul ndobo mwenyewe alikuwepo pale kituoni na baada ya mabishano makubwa paul ndobo aliwaambia CCM atakaye taka kubadilisha matokeo ya kura kinyume na yalivyo nitampiga risasi hapahapa!! na ccm walipoona mzee ndobo hatanii walikubaliana matokeo yawe kama yalivyo na hapo ndobo akatangazwa mshindi. Waungwana ebu naomba mnifahamishe sasa utaratibu huu wa wagombea kuwepo katika vituo ulishafutwa? Pia jambo jingine naomba tutoe ushauri kwa chadema jinsi gani watalinda kura zao!
 
Jimbo la Musoma liliwahi kuchukuliwa na upinzani??? Naomba tukumbushane plz....
 
Hili na mimi linanipa wasiwasi. Nimemsikia Dr. Slaa akisema mwaka huu tutalinda kura zetu haitapotea hata moja. Lakini hajawa wazi ni mbinu zipi zitakazotumika. Ukichukuliwa ufinyu wa mtandao wa CHADEMA huko vijijini (hata baadhi ya maeneo mijini) na ukweli kwamba vyombo vya mabavu vya dola vimeishatangaza nia ya kuingilia kati kwa niaba ya CCM, kuna kigiza kinatanda.
 
uteuzi makini wa mawakala ambao wametosheka ndiyo mwisho wa JK na ngome yake ya wezi na wabadhirifu wa CCM
 
Back
Top Bottom