Waghushi waraka kuhusisha CHADEMA na migomo

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, ameeleza kuwa wapinzani wa kisiasa wa chama hicho wameghushi waraka wenye sahihi yake ambao unakihusisha chama hicho na migomo inayoendelea nchini.

Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu, Dk. Slaa alisema inashangaza watu kughushi waraka wa namna hiyo wakati ambao nchi inakabiliwa na changamoto nyingi hususani za kuwakwamua wananchi na lindi la umaskini.

Alisema chama hicho kitaendelea kutekeleza wajibu na majukumu yake kama chama cha siasa ikiwemo kuuelimisha umma juu ya haki za msingi pamoja na umuhimu wa kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ya nchi.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa shirikisho la Chama Cha Mapinduzi katika Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Dar es Salaam, Asenga Abubakar, alisambaza waraka unaodaiwa kutolewa na Dk. Slaa kwa viongozi wa Chadema kuwataka washinikize migomo nchini hususani wa walimu.

Akizungumza na NIPASHE jana, Asenga alisema waraka huo umesambazwa kwenye mitandano ya kijamii na kwamba yeye (Asenga), alitoa nakala na kuzisambaza kwa vyombo vya habari kwa nia njema ya kukemea maelekezo hayo.
 
Kweli ccm wameshikwa pabaya. hiyo kwa wale wapenda mpira tunaiita total football , yaani mpaka kipa anaenda kushambulia. mashambulizi kila kona. kwanini wasichanganyikiwe hawa magamba.
Jamani tukaze buti hawa wagamba watatoka tu 2015
 
Atuambie ni mitandao gani uliwekwa huo waraka?Na kwanini haukupatikana humu JF?Hao si ndio wale walioandamana kupinga mgomo wa madr?wanaacha kusoma wanakubali kutumiwa na wakina Nape.Nimeanza kuelewa kwa nini CCM walianzisha hii mitandao mavyuoni.
 
siasa za Mwigulu hizo ndiyo iko kwenye chat kwa sasa " Hat cuf ilikutana na mtihani huu! Kumbukeni makontena ya mapanga na na igp. Mahita; cuf ikasambaratishwa sasa imefunga ndoa na ccm" nafikiri cdm ndiyo wako uchumba siku wakilegea tu mahari italipwa.na.mwiglu
 
CCM wanadhani watatuhadaa km walivyowapoteza Cuf enzi za ngunguri aka mahita walipoleta contena la majambia wakawabambikia ngangari aka CUF kuwa wameleta ili wawachinje wa bongo wakati wa uchaguzi. Sisi na chadema ni km inzi na kidonda, tutafia Chadema!! Peoples power!
 
Waraka huo si umo humu? Lakini kama mnapinga kuwa hakuna waraka huo mbona nyaraka za Serikali mnazikubali hata kama mmeghushi wenyewe? cdm bwana! Limewaganda kooni hilo,halimezeki wala halitemeki! Mnaloo!
 
Tutaona na kusikia mengi kipindi hiki 'CDM' hakuna kusikiliza hawa jamaa dhaifu kabisa tena hafifu sana. Wanashindwa kujenga hoja wanaleta viroja hapa.
 
Kutapatapa kwa magamba kunazidi kuongezeka kwa kasi ya kutisha na tutaona na kusikia mengi kati ya sasa na 2015. Nchi inazidi kuporomoka kutokana na udhaifu wa DHAIFU.
 
Kama wameanza kuwatumia mpaka Vichaa wa Mungu, na kuwavika kesi ya kumtekanyara Dr. Ulimboka, kweli Chama cha Mabwepande kinaelekea ukingoni.
 
haka kajamaa ni kapuuzi sana huwa nakaona itv kwenye kipimajoto kanavaa matambara shingoni kama mgulu yule mzinzi.
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, ameeleza kuwa wapinzani wa kisiasa wa chama hicho wameghushi waraka wenye sahihi yake ambao unakihusisha chama hicho na migomo inayoendelea nchini.

Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu, Dk. Slaa alisema inashangaza watu kughushi waraka wa namna hiyo wakati ambao nchi inakabiliwa na changamoto nyingi hususani za kuwakwamua wananchi na lindi la umaskini.

Alisema chama hicho kitaendelea kutekeleza wajibu na majukumu yake kama chama cha siasa ikiwemo kuuelimisha umma juu ya haki za msingi pamoja na umuhimu wa kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ya nchi.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa shirikisho la Chama Cha Mapinduzi katika Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Dar es Salaam, Asenga Abubakar, alisambaza waraka unaodaiwa kutolewa na Dk. Slaa kwa viongozi wa Chadema kuwataka washinikize migomo nchini hususani wa walimu.

Akizungumza na NIPASHE jana, Asenga alisema waraka huo umesambazwa kwenye mitandano ya kijamii na kwamba yeye (Asenga), alitoa nakala na kuzisambaza kwa vyombo vya habari kwa nia njema ya kukemea maelekezo hayo.

hivi hawa watu wa ccm wamelogwa? Serikali yao yenyewe imekiri kuwa kuna mgogoro kati ya serikali na walimu na upo kwa msuluhishi alfu wanaojiita ccm vyuo vikuu wanaleta matamshi ya kijinga,tena walimu wanaasira kila wakidai haki wanapuuzwa nawaambia ccm walimu wengi hivi sasa ni wa level ya diploma na degree na jinsi usoteaji wa elimu ya tanzania ulivyo ccm wasidhani km wanaweza kuzuia mgomo kwa mbinu za kipuuzi km hizo,dhaifu
 
Atuambie ni mitandao gani uliwekwa huo waraka?Na kwanini haukupatikana humu JF?Hao si ndio wale walioandamana kupinga mgomo wa madr?wanaacha kusoma wanakubali kutumiwa na wakina Nape.Nimeanza kuelewa kwa nini CCM walianzisha hii mitandao mavyuoni.

huyu dogo asenga alidai kasimamishwa masomo chuon mwl. nyerere kwa kudai refund ya fi za matibabu.kumbe hata yeye anasimamishwa
 
Back
Top Bottom