Wageni kujaa kwenye ngo's watasaidia nchi hii?

Babu Ubwete

Senior Member
Jan 26, 2008
169
29
KUna wingi wa wageni katika NGO's za hapa Tanzania ukianza na volunteers,wakenya,wazimbabwe,wadosi, waghana,na wapopo. Hivi kweli hakuna reguratory body yoyote inayoangalia hawa wageni maana wengi wao wamekuja kutafuta riziki na wanalipwa dola nyingi kwa kazi ambazo watanzania wanaweza kuzifanya. Umefika wakati Tanzania ibaki kwa watanzania mambo yanayoendelea Ivory coast kiini chake ni wageni wengi kukimbilia nchini mwao. Serikali ijaribu kuangalia upya ni kwanini tuna wageni wengi kwa njia ya NGO's , investment ambao wanakuja kufaidi nchini mwetu kwani hili ni sawa na Time bomb, Tuna Universities nyingi zinazalisha graduates lakini ukiangalia top management ya Foreign banks,insurance & accounting firms, Telecom companies ni wageni hili tuliondoe haraka. Na kwenye Katiba liwepo.
 
Naunga mkono hoja hilo ni tatizo kubwa sana hapa nchini; na linatokana na ''ufala'' wa serikali yetu na sisi wananchi. Huwezi kuwa na wageni katika sekta ambayo siyo adimu kwa maana kwamba hakuna mtz anayeweza kufanya.

Hata hao ma CEO wageni wanapewa vibali labda miaka 2 kuwa wahakikishe wanajenga uwezo wa watz ili wachukue hixo nafasi, lakini kinachotokea ni rushwa, na ushamba tu vibali vina kuwa renewed hata miaka kumi.

Jaribu kwenda Zambia, Ethiopia, au Lesotho, hata Malawai uombe kibali cha kufanya kazi huko utaona wanavuokuhoji kuona kama umeleta ujuzi wa tofauti na walio nao wao
 
NGO moja inaitwa Imma world health inahusika na health capacity building whteva au engedderhealth, actionaid,helpage kweli wakenya na wazungu watakuwa na uchungu wa kusaidia watanzania kweli? Iliwahi kuibuliwa na current president wa African development Bank. kwamba haiwezekani AFDB imejaa wacanada, waeuropa na americans,asians halafu walete mabadiliko Africa lakini wakubwa wanaiblock hoja hiyo kwamba non mebers wanacontribute much kwenye peas ya Afdb. cijui wakenya hapa kwetu kwenye vi ngo wanaolipwa dola wanachangi utumbo gani zaidi ya kutudharau
 
:yield:

Lakini nadhani iko sheeria inayo-regulate hayo mambo...kama sikosei ni National Employment Promotion Service Act ya 1999 kama sikosei kuanzia section 24 mpaka 27 ili kulinda ajira za wazawa

Lakini pia ili kuwa na uhakika kama wanaibia au vipi na ukawa na uthibitisho ni volunteers walioingia kwa term za ku-volunteer na wanalipwa sana peleka case Uhamiaji....

Nakumbuka iliwahi tokea mtu kaja kama volunteer kwa 3 months then wakawa wanamlipa mipesa kwa wingi waungwana wakachomea yule dada akapigwa dola 700 kama adhabu na watu wa Immigration
 
Ni kweli kabisa wa TZ tumekuwa makondoo sana wageni wanakuja pamoja kuchukua posts ambazo ziko ndani ya uwezo wa TZ jamaa ni wanyanyasi,waulize waTz wanaofanya kazi na Africare Tz ni mashuhuda.
 
Kuna wataalamu wengi sana wa Kitanzania waishio nje ambao wangwewza kuanzisha NGO za kuendeleza nchi, na kuja Tanzania kama wataalam wa kigeni, lakini wakati huo huo ni wazawa. Nimeshawahi kusikia kuwepo kwa NGO hizo. Kitu muhimu ni NGO hizo upewa nafasi ya kuja kutoa huduma.
 
Shida ipo kwa serekali yetu hasa
uhamiaji kwani hutoa vibali bila
Kufikiria.Nina ushaidi kabisa pale
Uhamiaji wametumia wageni kama mtaji
Wao kwani wanahonga hela nyingi ku
Pata hivi vibali.Je tutafika?unakuta mtu
Anadiploma na wanampa udirector!je hatuna
Mtanzania anayeweza?
 
Back
Top Bottom