Waganda ni noma...!

Wa mmoja

Member
Aug 4, 2009
99
0
Wazazi wamemcharaza bakora mwalimu wa shule huko Uganda baada ya kufika ofisini akiwa amelewa chakari!

Sasa alienda kufanya nini shuleni huku amelewa?

Hivi Watanzania kama hawa wapo kweli wanaoenda maofisini wakiwa wamelewa...?!

Na kama wapo wachukuliwe hatua gani?
 
Hii stori inanikumbusha mkuu wa wilaya Bukoba aliyewachapa walimu wa shule za msingi za wilaya hiyo ikiwemo shule maarufu ya KATERERO.
 
Hii stori inanikumbusha mkuu wa wilaya Bukoba aliyewachapa walimu wa shule za msingi za wilaya hiyo ikiwemo shule maarufu ya KATERERO.

Sasa Babuyao,huyo mkuu wa wilaya si aliwachapa walimu kwa sababu ya kufeli kwa wanafunzi katika shule hiyo?

Huyo wa Uganda ni mlevi..! Na ndio mana nikauliza, je watu kama hao Tz wapo? Na kama wapo wachukuliwe hatua gani?
 
Kwa kweli wanapaswa kuchukuliwa hatua maana mwalimu ambaye anakuja amelewa siamini kama atafundisha inavyopaswa under the influence of alcohol. Na mara nyingi hata mitaala anakuwa hakuiandaa. Kumbe yafaa washughulikiwe kwa sababu wanatupa hasara wazazi na watoto wetu tuwapendao na taifa letu.
 
Mboko Tu!! Sasa mtu mzima anakuja kazini amelewa--tiba yake sii mboko tu???

Sasa mkubwa ina mana wakipewa mboko ndo watashika adbu au inakuwaje...?
Ukiachilia shule,kwenye maofisi mengine ina mana Boss inabidi achonge fimbo yake ya ukweli,mtu akikatiza tu na harufu ya pombe anakula stick,au inakuwaje hapo?!
 
Kwa kweli wanapaswa kuchukuliwa hatua maana mwalimu ambaye anakuja amelewa siamini kama atafundisha inavyopaswa under the influence of alcohol. Na mara nyingi hata mitaala anakuwa hakuiandaa. Kumbe yafaa washughulikiwe kwa sababu wanatupa hasara wazazi na watoto wetu tuwapendao na taifa letu.

Kwani walimu pekee ndo watumishi?Je na madaktari, polisi, mawazi, mbona ni wote tu. Sasa nani amchape nani
 
Kwani walimu pekee ndo watumishi?Je na madaktari, polisi, mawazi, mbona ni wote tu. Sasa nani amchape nani

Ndio mana nikauliza Zhule,ina mana kama mboko ndio fundisho,kwa hiyo inabidi Boss nayeye achonge fimbo yake ili kuwaadhibu wale wanaolewa...Hapa ina maanisha ni sekta zote not only the teachers!
Fundisho gani linawafaa hawa walevi wanaolewa maofisini wakati wa kazi?
 
Hata maofisini walevi ni wengi tu, labda "IUNDWE TUME" kuchunguza walevi
 
Kwani walimu pekee ndo watumishi?Je na madaktari, polisi, mawazi, mbona ni wote tu. Sasa nani amchape nani
Hakika wale wote wanaoenda maofini wamelewa wanapaswa KUADHIBIWA ikibidi wachapwe viboko ndiyo! kwani viboko ni moja ya adhabu lukuki zilizopo kwenye system zetu za mahakama. Kama njia nyingine hazisaidii, mi naona wachapwe mboko. Wakumbushwe ya Kanali Mnali kule BK.
 
Kuchapa siyo suluhisho na watu wanafanya starehe zao baada ya kazi sema asubuhi ndo vile vipato vyetu vidogo badala ya kupata hata supu kupunguza pombe utakuta mkubwa anakomelea mnazi/ulanzi/mbege/comon/kibuku na n.k hapo ndo anaibuka job akiwa safi!
Suluhisho labda viwango vya mishahara viongezwe ili tuone mabadiliko, -ve/+ve?
 
Alcoholism ni ugonjwa. Walevi wengi wanahitaji msaada ili waweze kuachana na tabia ya ulevi. Kutoa adhabu iwe ya viboko au ingine sio suluhisho la ulevi. Kwanza kwa machungu ya kuchapwa anaweza enda utwika zaidi. La muhimu hapa ni kuangalia kiini cha mhusika kuwa mlevi nakujaribu kutatua tatizo na sio kuadhibu matokeo ya ulevi. Viko vitengo vyakuwasaidia watu kama hawa ndani ya ustawi wa jamii. Ni muda vikakuza wigo wake nakufika kila mahala. Tutibu ulevi sio kuuadhibu.
 
Thanks much to you all,i think hili wazo la mzeeba likifanyiwa kazi litasaidia kwa kiwango kikubwa ingawa Tanzania yetu utekelezaji wa vitu vingi ni sifuri...!
 
Back
Top Bottom