Nimejikuta nikijiuliza kwa nini waganda amekuwa wagumu sana kukikubali kiswahili? Ningetegemea wawe mbele zaidi hasa ukizingatia wamekuwemo Kwenye uanzilishi wa jumuia yetu na Vilevile kiswahili sio lugha ambayo Kabila moja linaweza likadai kuwa ni lugha yake peke yake.
Je, ni kwa sababu ya kasumba ya kuamini kuwa lugha ya waliokuwa watawala waingereza ndio bora? Je, ni kwa kuwa wanajiona wao ni Taifa kubwa kwa vile walikuwa na watawala wakubwa toka enzi yaani Kambaka Kingdom kwa hiyo wangependa wote tuzungumze kiganda?
Je, Kenya imekikubali kiswahili kirahisi zaidi kwa sababu kinazungumzwa sana mombasa? Nashangaa nchi kama Kongo na Rwanda kuonekana kukikubali kiswahili zaidi kuliko waganda,inaweza kuwa sababu gani?
Wajuzi tujuzeni.
Karibuni.