Wafuta vioo kwenye foleni Dar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Kero
Mhariri
MIMI ni dereva, nimekuwa nikitumia muda mwingi barabarani na nimeshuhudia vijana wanaofuta vioo wakati magari yakiwa kwenye foleni na wananikera mno.
Wao wanachukua maji machafu, wanaloweka tambala, badala ya kukisafisha kioo, wanakichafua. Hili linatukera sana.

Baya zaidi wakimaliza kuchafua hicho kioo, wanadai fedha. Wakati mwingine, usipowapa fedha wanakutukana au kukurushia maji machafu, Je huu ni uungawana?

Tabia hii inakera mno, hasa sisi tunaofanya kazi za barabarani kila mara.

Tunaomba askari wa usalama barabarani na wengineo watusaidie kuwafukuza watu hawa, ambao wanatishia amani na usalama wa kazi

zetu na zaidi wanakera mno.
Juma Mnandi,
Dar es Salaam.
BARUA HIZI

Tunachajiwa 10,000 za ulinzi shirikishi,kila mwezi, hii ni haki?

Mhariri

NINASHUKURU kupata nafasi ya kueleza malalamiko yangu katika chombo hiki bora.
Sisi ni wakazi wa Tabata, Mawenzi hapa Dar es Salaam, tunasikitishwa na kitendo cha viongozi wetu ambao hatupendi kuwataja kwa majina, kutuchaji kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili tu ya ulinzi shirikishi.

Viongozi hao wanapita kila nyumba wakitulazimisha tulipe Sh 10,000 kwa ajili ya kuwalipa wanaolinda usiku.

Tunakubali kufanya hivyo kwa kuwa, ulinzi shirikishi ni jambo la muhimu mno kwa usalama wetu. Lakini kiasi hicho cha fedha ni kikubwa mno.

Baadhi yetu kwa siku tunaingiza kipato ambacho hakifiki hata robo ya hicho, inakuwaje leo tutoe elfu kumi kwa ajili ya ulinzi.
Mbona maeneo mengine ya Dar es Salaam, wanatoa Sh 1000 kutwa?
Huu ni unyonyaji na unadhihirisha tabia za ubadhirifu wa fedha kwa viongozi wetu.
Noeli Mkweree,
Tabata-DSM.

Madereva wanaotumia simu wakiendesha wadhibitiwe

Mhariri

MADEREVA wa magari wa siku hizi wanashangaza, wengi wameshazoea na kufanya kuwa ni kawaida kwao, kuzungumza na simu wakati wakiendesha vyombo vya usafiri.

Tabia hii hivi karibuni imesababisha ajali mbaya mno.
Madereva wa aina zote, kuanzia wa bajaj, bodaboda(pikipiki), baiskeli na magari wanavunja sheria, jambo ambalo linatishia usalama wa maisha yao na ya raia.

Serikali iwachukulie hatua kali wanaofanya vitendo hivi, bila hivyo, ajali hazitapungua Tanzania.
Lakini, si hivyo tu, bali madereva hawa wadhibitiwe pia hata katika kuiheshimu mistari ya barabarani (zebra crossing).
Wamekuwa hawazingatii mistari hii na wanapita bila kuwajali wavuka barabara hivyo kuwafanya raia kusubiri kwa muda mrefu kuvuka barabara.
Mwikali Nyembo,

Wafuta vioo kwenye foleni Dar
 
Hizo ndio ajira alizo ahidi baba mwanaasha? ****** jk
 
Tz ina mambo hakuna sheria inayoongoza nchi hii. Zote zimebaki kuwa kwenye makabrasha yaliyo rudufishwa kwa gharama kubwa na sasa ni chakula cha panya na mende. kama siyo katratasi za kufungia vitafunwa maofisini lol............ wapi ustawi wa jamii na sera zao? polosi je? haya na tume ya jiji inafanya nni? meya wa jiji hivi gari lako huwa linafutwa vioo na hawa vijana?
 
Hii ya wafuta vioo ni KEROOOO kubwaaaa!
Huwa najiuliza mara zote hivi hawa viongozi wetu hawakerwi na hao vijana wanaolazimisha kusafisha vioo na mimaji yao michafu????!!!!na ukikataa wanakutukana na kukumwagia maji machafu halafu wanaondoka.
 
Back
Top Bottom