Wafuatao waliwahi kukutana uso kwa uso na busara na hasira za Mwalimu Nyerere!..

Nasikia alikuwa na tabia ya kuchana vyeti vya watu vya taaluma! mfano umesoma nje umepata Phd, kama ukileta longolongo anakwambia leta cheti chako hapa anakichana mbele yako! pia ukizidi kujifanya mjuaji unaweka kizuizini
Ilitakiwa kufanya hivyo, watu wanasomeshwa na Serikali waisaidie nchi halafu wanaleta longolongo.
 
Hii ndo leo nasikia, kama kweli huyu jamaa hafai kuwa kiongozi maana alidanganya ufaulu. kimsingi ana cheti feki kamanda Siro aanzie hapo.
Sio feki kwa kuwa alisamehewa akaendelea na masomo na hatimaye alihitimu, cheti chake ni halali
 
Umewasahau Mwalimu Kazibure na Tuntemeke Sanga.

8. Mwalimu Kazibure, kwa kuamua kuondoka akiwa engineer wa Radio Tanzania pale ambapo Nyerere alipochelewa kwenye sehemu Radio Tanzania walipotakiwa kurusha matangazo moja kwa moja, na akaondolewa kazi na kuzuiwa eneo la Kibaha kama mwalimu tu

9. Tuntemeke Sanga, kwa kujiona yeye ni msomi sana luliko Nyerere na hata kutoa matamshi kwamba hakuna kazi iliyoendana na usomi wake Tanzania labda uraisi, Nyerere ampishe, na Nyerere kuamua asingeajiriwa popote pale nchini na ikibidi azuiliwe kijijini kwao akalime pamoja na usomi wake
 
Wakati huo mwenyekiti CCM taifa alikuwa Mkapa mwaka 1997 na ndipo alipoaanguka ghafla akiwa katika vikao vya chama na baadae kukimbizwa hospital na baadae kufariki dunia.
.
 
1. Idd Amini - Alipoivamia Tz.... Mwalimu alitamka tutampiga nduli!.. Na kweli Idd Amini alipigwa hadi akaikimbia Uganda....

2. Kolimba - Alipotamka CCM imepoteza Dira na Mwelekeo... Mwalimu alimwita Dodoma akamuuliza nani kakutuma useme hivyo?!.. Ndio ukawa mwisho wa Kolimba!..

3. Samweli Sitta - Alipokuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi UDSM aliongoza mgomo wa wanafunzi wenzake kudai siagi na maziwa!... Mwalimu aliibuka pale chuoni akamuuliza Samweli Samweli kwenu mnakunywa maziwa kweli?!.. Akamwambia lala chini, akamcharaza bakora na mgomo ukaishia hapo hapo!...

4. Abdul Jumbe! - Alipotaka serikali tatu!.. Nyerere alimuuliza moja kujumlisha moja ni ngapi?!.. Jumbe akajibu ni mbili!.. Nyerere akamwambia kama ni mbili mbona unataka serikali tatu?!.. Huo ndio ukawa mwisho wa Abdul Jumbe kuwa Rais wa Zanzibar!..

5. John Samwel Malecela - Ni baada ya taarifa kuzagaa kuwa amebadili dini na jina ili apate kuungwa mkono na nchi za kiislamu kugombea Urais mwaka 1995!.. Nyerere alimwambia wee John wewe umeenda Arabuni mara moja umebadilisha jina sasa unaitwa Jumanne!. Ukienda mara ya pili si utabadilisha kabila?!... Huo ukawa mwisho wa ndoto zake kuwa Rais wa Tz !...

6. Edward Lowassa - Alipokodi ndege binafsi ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 alimpa lift JK!.. Nyerere alimuuliza mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!...

Natamani Nyerere angekuwepo sasa na mwaka 2015!!......
huyu mzee alikuwa hataki utani wa kijinga
 
Hilo la sita kulilia siagi na maziwa ni kiboko..kwahiyo mzee akala viboko na mgomo ukaisha..haha...
 
6. Edward Lowassa - Alipokodi ndege binafsi ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka 1995 alimpa lift JK!.. Nyerere alimuuliza mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao vya mchujo!...
Kwenye hiyo ndege si walikuwa na Kikwete ..... ilikuwaje akakatwa peke yake!!
 
Baba Ritz walimuuliza una wake na vimada wangapi?akajibu 14,akatikisa kichwa akasema ukipata Urais utaoa wabunge wooteee na kuwapa viti maalum mamis wote na kila anayekusifia

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Baba Ritz walimuuliza una wake na vimada wangapi?akajibu 14,akatikisa kichwa akasema ukipata Urais utaoa wabunge wooteee na kuwapa viti maalum mamis wote na kila anayekusifia

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
duuh... teh Noma sana
 
Back
Top Bottom