Wafuasi wa CHADEMA wafikishwa mahakamani - Arusha

Kwa ujumla walikamatwa watu 46 jana,22 wakaachiwa kutoka kituo cha polisi,na 24 wamefunguliwa mashtaka mawili,la kwanza Uharibifu wa mali,na kushusha watu kwenye daladala,kati ya 24 waliofikishwa mahakamani 22 tumeweza kuwadhamini na 2 ilishindikana baada ya hakimu kudai amechoka,ilikuwa majira ya saa kumi na moja kasoro,hivyo tunategemea kuwatoa kesho kwa remove order.Eneo ambalo wanadaiwa kuharibu daladala ni Sabena,wakati hakuna hata mmoja aliyekamatiwa sabena,wengi ni wa December tena wamekamatiwa kwenye maduka yao
Hiki ndicho tunachokipinga,kimsingi polisi wanafanya kazi ya siasa,na kwa maelekezo,pamoja na vitisho vyote bado umma wa Arusha umeendelea kuwa na mshikamano mkubwa,Nawapongeza sana kwa kuja mahakamani kwa wingi
Kamwe hatutarudi nyuma,wala hatutaogopa..

Wana JF,

Kwanza natanguliza shukrani zangu kza dhani kwa Kamanda wetu kutujuza yaliyo jili huko mahakamani hiyo Jana,

Hapo kwenye nyekundu ndipo panapo nipa wasi wasi sana na kupima uwezo Mahakimu wetu na ni jinsi gani kesi zinavyo endeshwa mahakamani je Ilikuwa ni kibabe au Hakimu alikuwa amechoka kweli? kwani walikuwa wamebaki ni wawili kuwekewa mdhamana ila hakimu akasema amechoka na muda umekwenda,

Si jajua kabisa au process ya kuwawekea mdhamana hao walio kuwa wamebaki wawili ni kuwa wadhamini walikuwa wako mbali kuja kuwadhamini au kulikuwa na pungufu lipi? kwa hizo dakika chache au kumdhamini mtu kuna kuwa na procedure ya more tha 45mins?

Mbali na maamuzi ya hakimu je hii leo hawa watu wawili wameshughulikiwa na kutoka?

Maaan Upelelezi wa kuwakamata watu zaidi ya 30 na kudai walikuwa kwa tukio fulani within 6hrs na kuwafikisha mahakamani kesho yake je huwa twapeleka kwanza ushahidi wa kuhisi then uchunguzi baadae au ni kumshitaki mtu kwanza then ndio ufate uchunguzi makinifu?

Kwa Police yetu hiii nadhani kama ni ingekuwa hivyo basi hata sukari bangi mirungi tungekuwa twisha pata wahusika kami ila poli e hapa ndipo wandhihirisha kwa mara nyingine tena mapungufu yao ya utendaji kazi zao hauendani na haki bali unatawala jazba fitna siasa na chuki baina ya raia na police


Twaomba ufafanuzi kwa wanao jui sheria tafadhari katika hili jambo.

 
Back
Top Bottom