Wafipa bado wanakula panya, symbilis na maduduwasha?

M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
151
panya a.k.a koyo....panya buku, symbils a.k.a ndezi panya na maduduwasha a.k.a viwavi ni chakula cha enzi kwa jamii ya wafipa. Niliwahi tembelea kijiji kimoja kilichopo mpakani mwa zambia na TZ kinaitwa matai na kushuhudia kwa macho yangu vyakula tajwa vikiliwa
 
Watu wengine!! Nilidhani utasema wanakula sumu.
 
Sasa umeshuhudia mbona kuna alama ya kuuliza?

Huna uhakika na ulichokishuhudia au?
 
hao simbilisi ni watamu sana , duh sijawala siku nyingi.
duh huyu jamaa kanikumbusha mbaaaali sana!!! hao simbilisi ni watamu sanaaa nilikuwa nawala huko Iringa kwa mabibi lloh I miss those old days, bibi yetu alikuwa anatupeleka kwao Iringa kutembelea ndugu zake... ilikuwa ni utalii wa kutosha
 
Bado baadhi ya sehemu wanakula lakini zaidi Simbilis a.k.a ndezi, viwavi jeshi siku hizi sidhani kama vinaliwa sana kama zamani, panya(tunko) wanaliwa bado ila pia baadhi ya sehemu.......!!
Unatushangaa wafipa kula viwavi jeshi, huko kusini niliwahi ona wanakula konokono.
Karibu sana m-pesa Matai nikuandalie ugali kwa koyo na uuchi(asali)
 
Hivyo ulivyovitaja ni vyanzo vya protein. Something may be a resource to one communty, and may not be to another community. Hivyo usishangae ndugu. Kwanza jamii za panya zaliwa sehemu nyingi Tz, mfano Mtwara na wanamwita samaki nchanga. Tanga wanamwita ntoke vipi.
 
pamoja mkuu, binafsi nimewahi kula konokono (spanish food) ni watamu usipimie. Mwanzoni nili resist sana, kuna mzungu mmoja alinishawishi sana ni test ....then ndipo nikagundua uhondo wanaofaidi.
Bado baadhi ya sehemu wanakula lakini zaidi Simbilis a.k.a ndezi, viwavi jeshi siku hizi sidhani kama vinaliwa sana kama zamani, panya(tunko) wanaliwa bado ila pia baadhi ya sehemu.......!!
Unatushangaa wafipa kula viwavi jeshi, huko kusini niliwahi ona wanakula konokono.
Karibu sana m-pesa Matai nikuandalie ugali kwa koyo na uuchi(asali)
 
Viwavi jeshi, guinea pigs na panya vinaongeza nini mwilini? Vitamin Q au Z??

ah? Wewe umekariri kuwa piza na burger ndo vyenye virutubisho eh? Katika vyanzo vya protini, wadudu nao wanahusika, nadhani viwavi ni wamojawapo.
 
Ni kweli mkuu lakini kula viwavi jeshi mmmmh
ah? Wewe umekariri kuwa piza na burger ndo vyenye virutubisho eh? Katika vyanzo vya protini, wadudu nao wanahusika, nadhani viwavi ni wamojawapo.
 
Tukubaliane kuwa tamaduni zetu zinatofautiana hata vyakula tunavyokula pia vinatofautiana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom