Wafaransa, waswisi vinara kuvaa soksi zinazonuka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,079
GENEVA

UTAFITI uliofanywa na kampuni ya Uswisi ya Blacksocks umeonesha kuwa asilimia 66 ya wanaume wa kifaransa hubadili soksi zao kila siku, huku kila watu saba kati ya 10 wenye asili ya Uswisi ndiyo huvaa pea ya soksi safi kila siku.Inabanishwapia kuwa wanaume wa Kijerumani na Waingereza asilimia 78 huvaa soksi safi kila siku, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa watu 3000 katika nchi sita.
Hiyo ina maana kuwa wanaume wa kifaransa au kiswisi ndiyo wanaoongoza kwa kuvaa soksi zinazonuka kuliko wajerumani au waingereza.
Kwa ujumla, asilimia 77 ya wanawake na wanaume waliofanyiwa utafiti walibadili soksi kila siku, wakati asilimia 11 walisema hubadili baada ya siku moja au mbili.

Asilimia nne huvaa soksi safi kila baada ya siku tatu, asilimia moja hubadili mata moja tu katika wiki.
Uwiano wa kubadili soksi ulikuwa ukilingana na idadi ya soksi ambayo muhusika anamiliki.

Wanaume wa kijerumani wameonekana kupenda kuwa na soksi, ambapo kwa wastani mtu humiliki hadi pea 24. Wanaume wa Austria huwa na pea 23, wakifuatiwa na Waswisi kwa pea 22

Spoti Starehe | www.spoti.co.tz

Kumbe hata Wazungu wananuka miguu Fangasi hahahahahahahahh
 
Back
Top Bottom