"Wafanyakazi Wa Wilaya ya LONGIDO,Wafunga Ofis wote na Kwenda Kwenye MAANDAMANO"

mjunguonline

Member
Mar 10, 2011
73
5
Hakika nchi yetu sijui inakwenda wapi ndugu zangu.Huku "LONGIDO",wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya.Wameamuliwa na MKURUGENZI MTENDAJI kufunga Ofisi na kwenda kwenye MAANDAMANO Mkoani "Arusha" ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Tz

Hivi navyowapa taarifa,Ofisi zote za Halmashauri,zimefungwa,na hakuna Huduma yoyote inayopatikana

Hivi,watanzania tunakwenda wapi?Inaingia akilini kweli,watu mfunge Ofisi,na kuondoka wote na kwenda kwenye maandamano?

Mi nadhani,ingekuwa ni busara,kama wangeenda baadhi,na wengine wabaki,kufanya kazi,kwa niaba ya wenzao!Kinachouma zaidi ni kwamba!Kutoka LONGIDO hadi ARUSHA ni Km 86.Mkurugenzi kajaza mafuta,ya kwenda na kurudi Kwa Gari km 7 aina ya Landcruser.Ivi huu si ufujaji wa Mali za Umma.

Hii ndio Tanzania,inayoazimisha miaka 50 ya uhuru!
 
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni kwa hiyo watendaji imekuwa nafasi nzuri ya kujipatia posho,kweli Tanzania shamba la Bibi wakikuta ofisi zimewashwa moto watasemaje
 
Kwanini wasiende wakati watavuna maposho na hakuna atakayewauliza nchi hii inatawaliwa kishikaji na kisela sasa ni wakati wa kusema sasa imetosha kwani kwa mtindo huu ndio unasorotesha maendeleo na ndio maana unakuta halmashauri imepangiwa mabilioni kwa ajili ya miradi mbali mbali lakini hakuna kinachofanyika si shangai mkurugenzi wa longido kwenda huko na msururu mrefu kwani longido ipo kwenye top ten ya wilaya zilizoongoza tanzania kwa upotevu wa nyaraka za ukaguzi hadi kukwamisha ukaguzi hii according to CAG ripot hasa hasa wilaya zinazokaliwa na wafugaji kwani ngorongoro ndiyo iliyoongoza kwa upotevu au kwa kuficha nyaraka kwani jumla ya nyaraka 164 hazikuonekana hivyo kukwamisha ukaguzi na bado mkurugenzi anapeta sasa kwanini wasiende wakati hakuna wa kumuuliza wilaya zilizopo kwenye kumi bora kwa upotevu wa nyaraka ni kiteto,simanjiro,longido,kilindi,pamoja na zingine nyingi achana zile tatu zilizopata hati chafu hivyo hawajapewa chochote kwenye budget ya mwaka huu sasa kama hali ni kwanini wasiende
 
huyo mkurugenzi anajua kabisa ndo mbinu ya kumtoroka mkewe na kwenda kutafuna vimada A town ndo maana yukoo mbele mbele kufunga ofisi ili iwe ni kisingizio
 
Hakika nchi yetu sijui inakwenda wapi ndugu zangu.Huku "LONGIDO",wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya.Wameamuliwa na MKURUGENZI MTENDAJI kufunga Ofisi na kwenda kwenye MAANDAMANO Mkoani "Arusha" ya maadhimisho ya Miaka 50 ya TzHivi navyowapa taarifa,Ofisi zote za Halmashauri,zimefungwa,na hakuna Huduma yoyote inayopatikanaHivi,watanzania tunakwenda wapi?Inaingia akilini kweli,watu mfunge Ofisi,na kuondoka wote na kwenda kwenye maandamano?Mi nadhani,ingekuwa ni busara,kama wangeenda baadhi,na wengine wabaki,kufanya kazi,kwa niaba ya wenzao!Kinachouma zaidi ni kwamba!Kutoka LONGIDO hadi ARUSHA ni Km 86.Mkurugenzi kajaza mafuta,ya kwenda na kurudi Kwa Gari km 7 aina ya Landcruser.Ivi huu si ufujaji wa Mali za Umma.Hii ndio Tanzania,inayoazimisha miaka 50 ya uhuru!
POSHO MKUU! Penye maandamano ujue Maandaziyamo na kila kikao na kikalio. Unauliza upweke Kaburini?
 
watapata posho ya hotel,chakula,nauli,t-shirt,usumbufu nk.kila mtu si chini ya laki
 
Back
Top Bottom