Wafanyakazi wa Migodi Kanda ya Ziwa watangaza Vita na Serikali

Kwa hakika hii Nchi inaudhi kibaya zaidi wapo wachache wanajaribu kucheza na maisha ya watanzania walala hoi wakidiriki hata kutumia dola inauma inaudhi this time WASIJARIBU
 
Wametangaza kutokuwa na imani na waziri wa kazi Bi.Gaudencia Kabaka pamoja na mkurugenzi mkuu wa SSRA Bi. Irene Kisaka.
Ni katika muendelezo wa kupinga utekelezaji wa sheria mpya ya mafao ya kujitoa inayowalazimu wanacahama wa mifuko ya pensheni ya NSSF na PPF kutochukua mafao yao hadi watakapotimiza umri wa miaka 55. Pia wamedai waziri aliudanganya umma kupitia bunge alipokuwa akitolea ufafanuzi madai yao ya kupinga sheria hiyo.

Walikuwa wakizungumza katika mkutano uliowakutanisha wawakilishi wa Jumuiya za wafanyakazi wa migodi ya kanda ya ziwa.
Wameitaka serikali kuandaa risasi za kutosha, mabomu ya kutosha, makaburi ya kutosha na magereza ya kutosha kwakuwa katika bunge lijalo la mwezi wa 11 kama sheria hiyo haitasitishwa nao hawatakubali kamwe kunyimwa mafao yao kwa kutumia sheria kandamizi.

Source ITV.
wadai na maslahi mengine sio mafao tu
 
Kwa hakika hii Nchi inaudhi kibaya zaidi wapo wachache wanajaribu kucheza na maisha ya watanzania walala hoi wakidiriki hata kutumia dola inauma inaudhi this time WASIJARIBU

Kama wafanyakazi wa Tanzania wataondokana na uoga pamoja na unafiki kwa hakika wataweza kupata maslahi mazuri ya kazi zao.
Walimu hapo jirani zetu Kenya walipoamua kupigania maslahi yao wakaunganisha nguvu bila kuruhusu itikadi za kisiasa kuwatenganisha hatimaye wamefanikiwa madai yao na serikali ya Kenya imekubali kutekeleza madai yao.
Hapa kwetu Tanzania wafanyakazi wanachojua ni kulialia na kulalamika bila kuchukua hatua madhubuti zaidi ya kuwategemea viongozi wa Tucta watangaze mgomo kisha waandamane wao wenyewe.
 
Kweli ndugu yangu......waamke wapaze sauti zao kwa pamoja manake wakizubaa watajaachwa......afu watakosa pa kulalamikia manake na sisi tutawauliza walikuwa wapi siku zote?

PPF na NSSF wamewekeza katika miradi mikubwa kadhaa ikiwa ni pamoja na kuikopesha serikali mabilioni ya shilingi. Na bado serikali inaendelea kuikopa mifuko hiyo ya pensheni bila kuwepo na repayment plan kwa mikopo ya awali.
Mifuko hiyohiyo kwa upande wa pili inaliwa sana na management zao kwa kujilipa mafao yasyoeleweka mathalani mamilioni wanayojilipa wakurugenzi wa PPF kwa kile kinachoitwa endowment scheme kila baada ya miaka mitano.
Inawezekana kabisa mifuko hii ya PPF na NSSF imeishiwa fedha za kuwalipa wanachama wake sasa serikali imeamua kutunga sheria ya kuinusuru na aibu ya kushindwa kulipa mafao na pensheni kwa wanachama wao.
 
Back
Top Bottom