Wafanyakazi wa Kampuni Kwa Kujiua Hawajambo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
3102154.jpg

Kampuni ya simu ya Ufaransa, France Telecom imekumbwa na wimbi la wafanyakazi wake kujiua Wednesday, September 16, 2009 5:13 AM
Kampuni ya simu ya Ufaransa, France Telecom imekumbwa na wimbi la wafanyakazi wake kujiua, wiki iliyopita walijiua wawili, katika mwaka mmoja na nusu jumla ya wafanyakazi 23 wa kampuni hiyo wameishajiua. Alhamisi iliyopita katika kukomesha wimbi la wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Ufaransam France Telecom kujiua, mkuu wa kampuni hiyo alitoa risala ndefu kwa wafanyakazi wake ili kuwafanya wasiwe na mawazo ya kujiua.

Lakini siku moja baada ya mkuu huyo wa kampuni kuongea na wafanyakazi wake, mfanyakazi mwanamke wa kampuni hiyo mwenye umri wa miaka 32 alijirusha toka ghorofa ya nne ya jengo la kampuni hiyo lililopo jijini Paris na kufariki dunia.

Kifo cha mwanamke hiyo kilikuja ikiwa ni wiki chache baada ya mfanyakazi mwingine wa kampuni hiyo mwenye umri wa miaka 57 kujiua nyumbani kwake na kuacha barua akiilamu kazi yake kwa kumfanya aingie kwenye dipresheni.

Wiki hiyo hiyo, fundi mitambo wa kampuni hiyo alijichoma kisu tumboni kwenye mkutano wa wafanyakazi akilalamikia mazingira ya kufanya kazi.

Kama hiyo haitoshi jana pia meneja masoko wa kampuni hiyo katika mji wa Metz alikutwa akiwa amezidiwa ofisini kwake baada ya kumeza vidonge kwa nia ya kujiua baada ya kupewa taarifa ya kuhamishwa kikazi mji mwingine kwa mara ya tatu ndani ya mwaka mmoja.

Hali hiyo ilisababisha serikali ya Ufaransa kumtaka mkuu wa kampuni hiyo kujaribu kuongea na wafanyakazi wake kupunguza wimbi hilo la kujiua.

Kampuni hiyo ambayo awali ilikuwa ya serikali, ilibinafsishwa mwaka 1998 na ndipo wamiliki wake wapya walipoamua kufanya mabadiliko kwenye kampuni hiyo kuongeza ufanisi na kupunguza gharama.

Mwaka 2000 walijiua wafanyakazi 28 wakati mwaka 2002 wafanyakazi 29 waliamua kujitoa roho zao wenyewe.

Kampuni hiyo yenye wafanyakazi laki moja nchi nzima imelaumiwa na umoja wa wafanyakazi kuwa hatua yake ya kuwahamisha hamisha wafanyakazi na kuwapunguza kazi wengine katika hatua zake za kupunguza gharama ni miongoni mwa sababu zinazochangia wafanyakazi wake kujiua.

Wamiliki wa kampuni hiyo wameamua kusimamisha mipango yote ya mabadiliko waliyoipanga awali ili kuongeza ufanisi na kupunguza gharama katika kampuni hiyo. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3102154&&Cat=2
 
Hizi ni bangi tu, kwa hizo sababu walizotoa bongo tungeshajiua wote.
 
Back
Top Bottom