Wafanyakazi wa Airtel mwaendekeza nJaa wateja tumewachoka!

NIMIMI

Senior Member
Apr 2, 2011
170
16
Wanajamvi poleni kwa majukumu! Kuna tabia wanazionesha na kufanywa na wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Mlimanicity hazitufurahishi wateja. Vocha zao hazina ubora ukikwangua namba zilizofichwa ili kuongeza salio zinachubuka na baadhi ya namba kutosomeka, Lakini cha ajabu tangu nianze kuwarudishia ili waniangalizie na kuongeza salio naambiwa niondoke watanitumia muda wa maongezi chakushangaza na kuudhi hadi sasa hakuna muda majibu yeyote.
Na nikifuatilia naambiwa bado, sasa hayo majibu ya bado hadi lini ama mmetumia pesa zangu, mbona mnapoteza uaminifu kwa kampuni iliyokuwa ikiaminika hivi aliyeko mlimanicity kufika makao makuu ya Airtel inamchukua siku ngapi? Kweli nimeudhika sana na zaidi naonekana sio mwaminifu ukizingatia kuna vocha ambazo niliagiziwa na watu wanadhani nimezitumia.
Hii haitoishia hapa jamvini lazima nipeleke mbali zaidi hata kwa waziri wa mawasiliano nitafika jamani uwizi mlo ufanya hamjatosheka hadi kuiba waziwazi? Wanajamvi kama wahusika wamo humu ujumbe huu uwafikie Tabia hizi zinakera mno na waufanyie kazi. Wanajamvi msaada wenu tafadhali.
 
Kuhusu vocha kuharibika zinapokwanguliwa hilo ni tatizo la nchi nzima.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom