Wafanyakazi TRL wawazomea maofisa Sumatra

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
na Betty Kangonga




WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Reli (TRL) jana waliwazomea maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) na viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU baada ya kutoa maelekezo ya kufanyika majaribio ya mabehewa na injini vyote vilivyozuiliwa na RITES mwezi uliopita.

Wafanyakazi hao waliwazomea maofisa na viongozi hao baada ya kutoka kuangalia karakana ya reli na kujadili jambo kwa dakika zisizozidi 15.

Baada ya viongozi hao kutoka ndipo wafanyakazi hao walipolipuka kwa kelele za kuzomea na kuwaita viongozi hao ni wala rushwa na vigeugeu kwa kukosa msimamo katika suala hilo linalohusu uhai wa watu.

Hata hivyo akiombwa afafanue lile walilojadili kwenye kikao hicho mkurugenzi wa huduma za reli kutoka Sumatra, Eliyona Simbo, aligoma kuzungumza na kuwataka waandishi wamtafute wakati mwingine.

“Kwa sasa siwezi kuongea, naomba mje ofisini kwangu au mnitafute kwenye simu, sina lolote la kueleza hapa,” alisema.

Aidha, akizungumza na Tanzania Daima Mwenyekiti wa TRAWU, Emanuel Jomalema, alisema katika kikao hicho kilichofanyika Wizara ya Miundombinu waliombwa kujaribu kuwaelimisha wafanyakazi hao ili wakubaliane na matakwa husika.

Hata hivyo walipokutana na wafanyakazi na kuwapa ushauri ili kukubali azma ya Sumatra, hawakuwa tayari kwa lolote na kusisitiza kuondoa mabehewa na injini hizo kuzirudisha India.

“Kwa kweli katika kikao kile tumeombwa kuwaelimisha wafanyakazi wote wa nchi nzima, lakini kwa hao wachache waliopo hapa wamekataa kabisa ambapo wameomba mbia kuchukua miundombinu yake,” alieleza mwenyekiti huyo.

Mabehewa na injini hizo zilikuwa zifanyiwe majaribio kuelekea mkoani Morogoro na kurudi Dar es Salaam kabla ya kuanza safari zake.

Akielezea zaidi William Ngaja ambaye ni mfanyakazi wa TRL alisema wameshangazwa na kitendo kilichofanywa na SUMATRA cha kutaka kufanyia majaribio mabehewa 20 ili kuweza kuanza safari huku wakielewa kuwa hayana ubora.

“Hivi kweli unaweza kukubali vipi ufanyie majaribio mabehewa ambayo yapo chini ya kiwango na hayana ubora wowote, hapo si kutaka kuwateketeza Watanzania wenzetu ambao hawana hatia yoyote?” alihoji Ngaja.

Sumatra imefikia hatua hiyo huku ikiwa ni mwezi mmoja (septemba 10) RITES alipoamua kuchukuwa miundombinu yake baada ya TRL kushindwa kulipa deni la kiasi cha sh milioni 436.
 
Back
Top Bottom