Wafanyakazi: JK Hahitaji kura zetu

Status
Not open for further replies.
Amesema hahitaji, mnampa za nini? Wapeni wanaozihitaji. Alidhani atawika peke yake hakujua Slaa ataingia kwenye mizani. Yuko kimya kamwe hataomba radhi, maana kuomba radhi kutamaanisha kukubaliana na madai ya wafanyakazi, naye alisema kwa mtaji huo hahitaji kura zenu. Mnadhani kura zenu ni almasi? Mashine za kuchapisha katatasi za kupigia kura wanazo, nia za kuzitumia mashine hizo wanayo, sababu wanayo na hata uwezo wa kufanya hivyo wanao. Tume ya kumsimamia kuchaguliwa si ipo? Wafanyakazi mlie tu. Kishindo chaja kwa wizi au vinginevyo. Ndipo mtajua Chukua chako mapema maaana yake nini.

CCM ina mikakati lukuki na imeanza kuwafyata mikia vidomodomo wote kama Lyatonga alivyofyatishwa mkia kwa kuingilia magendo ya wakubwa wake airport. Amelala njaa keshakumbuka asali na maziwa sasa ameanza kuimba nyimbo za Misri kwa kumsifu Farao kwa uongozi usiomithilika kwa utamu. Si alipelekwa India kutibiwa na Firauni?

Lakini Slaa kuja kwake kutamfanya Firauni asipate usingizi sawasawa. Wameanza kumzima kwa kuzuia TBC1 na Daily News wasiongelee habari za Padre wasije wakampa umaarufu zaidi. Lakini wapi bwana, Padre anapeta tuuuu utadhani hana akili nzuri vile, mpaka kieleweke. Watamtafutia viskendo, maana ccm hawajambo kwa hilo. Slaa anatakiwa kuwa macho kwa kila anachokisema na kufanya sasa hivi, maana ccm badala ya kujizatiti kutetea ilani yao ya uchaguzi wametibuliwa na wataanza kuzama katika kutafuta wapi padre atateleza, kama fisi anavyovizia mkobo wa mtu udondoke kwa kufuatilia kivuli.

Angalia TAKUKURU kinachowapata. Mkuu wa wilaya na Waziri wamevuliwa na nyavu za rushwa, dola inawazima midomo TAKUKURU kwa kudemote na kuhamisha wapiganaji. Wanasahau kwamba watanzania wa 2010 sio wale wa 2005. Wameelewa zaidi. Ndio maana hawadanganyiki kwa ahadi za kuletewa bahari Kalenga. Sasa Twaambiwa DSM kutapambwa na barabara za angani. Vituko nchi hii mwisho sana.
 
Jamani ehhh, kuna vijana walioifanya hiyo kazi. Itakuwa naiba ufundi na kazi ya mtu kuchukua hapa credit kwa kazi yao.

SIKONGE HAHUSIKI na UCHORAJI WA HIYO TSHIRT. Niliikumba tu sehemu kwenye Facebook na kuileta hapa.
 
Imependeza sana. Ni vizuri vitengenezwe vipeperushi vingi na visambazwe nchi nzima, na nyuma yake iandikwe - mbona sisi wazazi tunawategemea watoto wetu ambao ni wafanyakazi? AU kwa kutoongeza mshahara, sisi wategemezi wa wafanyakazi si tutaumia?-nasi kura zetu basi!
 
Hivi huyu jamaa alijua kama itamcost kiasi hiki? Au ulevi ulimpotosha...
 
Huyu bwana nadhani kaona watanzania kama vile vuvuzela unapuliza pale upatapo pumzi. LOL
 
He did a grave mistake! and, it will cost him a great deal..hayo ndiyo malipo ya usanii asilani.
 
Alipopandishwa mori na makada wa ccm aliowaita wazee wa DSM hakuzita. Wazee waliporudi makwao wakamwacha peke yake ndipo akili zake zinamrudia na kujua kwamba kura za wafanyakazi ni muhumu kwake. Jk imekula kwako mazima, yangu huipati!!!
 
Ameshawaambia kwamba hazitaki kura za Wafanyakazi, yaani hana shida nazo, hata msipompa atashinda tu,yaani hata mgome miaka nane Mishahara haitapanda, Je kutokana na kauli zake hizo JK anastahili Kura za Wafanyakazi na wale wote wanaowategemeza?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom