Moja ya matatizo makubwa kwa watz ni umasikini wa akili.
Wafanyakazi walio wengi ni masikini wa akili na hii ndiyo sababu tosha ya kuamini kwamba wataendelea kumpigia kura pamoja na kwamba hazihitaji.
Wafanyakazi na wakulima wamenyang'anywa chama chao (CCM) lakini hakuna anayeweza kuhoji na hawajui kwamba chama kimeporwa.
Sasa hivi mafisadi, wezi, wafanyabiashara wenye tamaa, viongozi wa dini wenye tamaa na wanaofanana na hao ndiyo wanaopigana vikumbo kusaka uongozi wa kuchaguliwa kupitia chama cha wakulima na wafanyakazi.
JK amesahau kwamba chama chake ni cha wakulima na wafanyakazi na wafanyakazi hawajui kwamba wao wamemuajiri.
Sasa tutegemee nini kwa watu wa aina hiyo?