Wafanyakazi: JK Hahitaji kura zetu

Status
Not open for further replies.

Recta

JF-Expert Member
Dec 8, 2006
855
38
Nimesubiri kwa muda mrefu kusikia kama JK atabadi kauli yake kuwa kura za wafanyakazi hana shida nazo. Kinachonijia akilini ni kimoja tu kadiri tunavyokaribia uchaguzi mkuu. Nacho ni kuwa labda anajua jinsi ya kuzipata kura anazozihitaji au ana uhakika kuwa kura nyingine zote, zinamtosha au hana haja ya ushindi.

oub6n9.jpg

Kha huyu jamaa unadhani atakuja kusahihisha kauli yake ...kishaona wafanyakazi hawamfahi
 
JK anuhakika kabisa, yaani hizo kura za wafanyakazi zimeshachongwa duplicate !!! Hizo kura halisi za wafanyakazi hazihitaji tena hata kama zote mkimpa Dr.Slaa !!!! " Kijani bila w*zi hakifiki "
 
JK anuhakika kabisa, yaani hizo kura za wafanyakazi zimeshachongwa duplicate !!! Hizo kura halisi za wafanyakazi hazihitaji tena hata kama zote mkimpa Dr.Slaa !!!! " Kijani bila w*zi hakifiki "
Mkuu umenikumbusha. Kuna sehemu nimesikia, wameanza kutengeneza wapiga kura vivuli (idadi sawa na wapiga kura halisi) ili kujihakikishia ushindi wa kura za maoni. Ikitokea hivyo kwenye uchaguzi mkuu wa vyama vingi, nadhani kuna hali mbaya inayoweza kutokea.

Unajua, si rahisi kuiba kura za wengi wapendao mabadilko kwa imani thabiti. Kufanya hivyo kunaweza kuanzisha vita ya ajabu.
 
Hivi mkuu, hata wewe kama huhitaji kura ya mtu je, unaweza ku-apologize kwake wakati huhitaji msaada wake?

JK ni SHABABI kwelikweli kwenye kupata kura za WIZI. Na CCM kwa kuiba kura hawawezekani na ndo maana ANAJEURI!!!
 
JK anuhakika kabisa, yaani hizo kura za wafanyakazi zimeshachongwa duplicate !!! Hizo kura halisi za wafanyakazi hazihitaji tena hata kama zote mkimpa Dr.Slaa !!!! " Kijani bila w*zi hakifiki "
Huu ni mwaka 2010 na sio 2005 au 2000. Hilo walitambue. Wajifunze kutoka Kenya kuwa wizi wa kura unachochea nini kwa watu waliofumbuka macho na kuzijua haki zao. Ukondoo wa miaka ya nyuma hata kama haujaisha kabisa lakini umepungua kwa kiasi kikubwa ndio maana tuliyaona ya Tarime,Busanda na Biharamuro. Huko kote zilipelekwa nguvu za ziada(kitaifa) jee sasa watatawanyika nchi nzima kuhimili? Wafikiri njia nyingine na si wizi, vinginevyo historia itawahukumu kwa yatakayo tokea. Kimbunga kitokeapo hakichagui nyumba,
 
Mimi nitashangaa mfanyakazi yoyote atakayejipendekeza kumpigia jk ili hali hana haja na kura zao. Alaaniwe jk, ilaaniwe ccm ,ilaaniwe tume ya uchaguzi, ilaaniwe TISS,
 
Kimsingi anazihitaji kura hizo lakini hana jinsi alishatukana wakunga na uzazi ungalipo. Si rahisi kurudisha nyuma kauli yake. Anaona aibu.
 
Mimi ni mfanyakazi siwezi kumpa kura Muungwana kwasababu tayari katamka haradhani haitaji kura yangu.Mfanyakazi yoyote atakaempa kura Kikwetu atakuwa hana akili nzuri au tunaweza kumwita mwehu.Wafanyakzi tuungane kumwangusaha Kikwete na genge lake la mafisadi.
 
Ah, lakini si anatakiwa ajue kuwa kura hizo ni nyingi sana. Itabidi kufungua ofisi za kuiba kura nyingi kiasi cha kumuwezesha kushinda. Labda kama ameshaanza kuzi-tick sasa hivi.

Ila uungwana ni kukiri kosa na kuomba msamaha. Si kawaida ni kuwa kipindi kama hiki (cha uchaguzi) alie juu anajishusha?
Ama sio waku.
 
Mimi nitashangaa mfanyakazi yoyote atakayejipendekeza kumpigia jk ili hali hana haja na kura zao. Alaaniwe jk, ilaaniwe ccm ,ilaaniwe tume ya uchaguzi, ilaaniwe TISS,

Inaonekana wewe huzijui akili za watanzania. Pamoja na matusi yote aliyowatukana JK wafanyakazi, pamoja na kazi mbovu aliyoifanya katika kiopindi hiki cha miaka mitano nenda kaanagalie wanaomuunga mkono JK ni akina nani?

Kaangalie wale wanaojipanga njiani kumpokea au kumpa mkono, ni akina nani? Waliomchangia pesa za kuchukulia form kule Dodoma ni akina nani? Yaani utakuta wasomi na watu wenye nafasi zao ndiyo wako busy na JK kuwashinda hata wakulima ambao hawakuwahi kwenda shule.

Fanya kautafiti kadogo one day uone ni nini kinachoendelea. Tuna shida sana hii nchi, sasa kaa kijiweni uwaone wanavyolalamika, huwezi amini kama hao ndiyo walewale waliokuwa wapambe wa CCM na ndiyo waliompa kura JK. Kaazi kwelikweli!!
 
JK ataijutia sana kauri yake, I think that is the rise and fall of Kikwete, Kalewa madaraka hadi anachangua wakumchagua. Masikini hata hajui mchango wa wafankazi wake. Watanzania tubadilike tufanye mapinduzi, ccm kweli wametuchoka kabisa wapiga kura wao..
 
Msijipotezee muda kufikiri mambo rejareja. Hawa jamaa wana mtandao wa kimafia - state mafia - kuhakikisha kura zinatimia kwa hesabu wanayoitaka wao. Ndio maana harakati zao za uchaguzi zinawasumbua zaidi ndani ya chama na sio nje yake. Wakimaliza kupangana ndani huko nje kila kitu kimeshakuwa set ukiachia kwa baadhi ya wagombea wao wanyonge wasiothaminiwa sana.

Hata vyombo vyote vya dola na usalama wa taifa tayari vinajua wajibu wao kwa chama kwenye kuhakikisha ushindi.
 
Ndiyo maana nimetoa tamko la kuilaani Tume ya uchaguzi na TISS kwani vyombo hivi ni mwiba mkali kwa demokrasia ya kweli kwa nchi hii.
 
Kwa taarifa ya tetesi JK kawaongezea walimu na secta nyingine kimya kimya walimu wanachekelea na kula zote watampa.Wadanganyika tutaendelea kudanganyika mpaka hapo CCM itakapogawanyika kwani kwa mtindo huu wa chadema na cuf kila mtu kivyake itachukua muda mrefu kuiondoa CCM madarakani
 
Kufuatia ile kauli ya mkuu aliyoitoa kwa moyo wa dhati
kwamba haitaji kula za wafanyakazi mwaka huu. Najiuliza,
Je ni kweli kwamba wafanyakazi hawatampigia kula?:A S confused:
 
sasa kama mwenyewe alisema hana haja na kura zetu tumpigie za nini? au ndo kujipendekeza?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom