Wafanyacho CLOUDS ni Uzalendo ama kuna Chembechembe za SIASA....

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
412
90
May it please wakuu wangu;

Kwa wale wapenzi wa mpira wanafahamu kuwa kesho ndio ule mtanange kati ya Yanga na Zamalak ambayo hii haiwezi kuwa hoja hata kidogo.

Hoja yangu ni kwamba Mechi hii kati ya hizi timu mbili imekuwa ikitangazwa na kufanyiwa Promo ya hali ya juu na Clouds Fm hasa katika kipindi cha Jahazi, Promo ambayo binafsi sikuwahi pata sikia hata wakati timu ya Taifa inapokuwa na Mechi ama za ndani au za nje. Promo ambayo naamini ingekuwa inafanywa kama inavyofanywa leo hii kwa namna moja ama nyingine inaweza kuwapa moyo si Wachezaji tu bali Mashabiki na Watanzania kwa ujumla na kukuta tunajumuika pamoja kwa mambo yahusuyo Taifa letu na wachezaji wetu.

Hili limenipelekea kuuliza Clouds na hata kulileta hapa kwenu waungwana ili pawepo na tafakuri juu ya mambo mawili;

1. Je hayo matangazo ni Uzalendo + Uclouds?? ama
2. Ni Uridhi1 + Uclouds

Kama jibu litakuwa ni Uzalendo + Uclouds

1. Je tutegemee promo ya namna hiyo pindi panapokuwa na Mechi zingine mathalan Taifa Stars, Simba, Maji Maji n.k???
2. Na kama jibu litakuwa Uridhi1 + Uclouds je hawaoni kuwa kwa kufanya hivyo ni kudhoofisha au kukatisha wengine tamaa kwa ubaguzi huo wa wazi??
 
Napendekeza neno Clouds lipigwe marufuku kama yalivyopigwa marufuku maneno mengine humu!
 
WAFU FM! I hATE WAFU FM! I HATE RADIO YA WAFU! I hate wAFU FM!
 
labda yanga wamelipia kama makampuni mengine ya biashara yanavolipia
 
Napendekeza neno Clouds lipigwe marufuku kama yalivyopigwa marufuku maneno mengine humu!

Mkuu Bwa'Nchuchu pendelezo lako laweza kuwa sawa lakini kama tukilikimbia hili hatutakuwa tumetatua tatizo bali tutakuwa tumewaonea Watz kwa kuuficha ukweli ama utata uliopo....... Ina kera ila kubwa ni kutafuta suluhu
 
Unaishi wapi ndugu? Clouds FM kupitia Prime Time Promotions wameinunua hiyo mechi na hivyo wana kibali cha kusimamia mazzndalizi hadi mauzo ya tiketi.
 
Clouds wamepewa tenda na Yanga ya kusimamia hiyo mechi kwa kupitia kampuni yao ya Primetime Promotion, ndo maana hata tiketi wanasimamia wao kuanzia kuzitengeneza hadi kuziuza!
 
labda yanga wamelipia kama makampuni mengine ya biashara yanavolipia

TODO japo siwezi kukubalina na wewe moja kwa moja na ni kutokana na kuto ipitia sheria inayolinda vyombo vya habari ila hili lako pia laweza kuwa neno lakini ni kweli kwamba TFF huwa wanashindwa kuilipia Taifa Stars kufanya Promo ya namna hiyo?? Lakini kwa nini isiwe Radio One, ama RTD, ama Magic Fm na zinginezo why Clouds??
 
Clouds wamepewa tenda na Yanga ya kusimamia hiyo mechi kwa kupitia kampuni yao ya Primetime Promotion, ndo maana hata tiketi wanasimamia wao kuanzia kuzitengeneza hadi kuziuza!

Shukrani kwa jibu Mzalendo wa kweli manake hiyo +255 iko pahala pake mkuu
 
Grate thinkers think twice please!!! Clouds ni institution ya kibiashra, wako kikazi zaidi sio kufurahisha umma tu. Yeyote anayewliupia matangazo yake atatangazwa kulingana na thamani ya malipo. Kipi cha ajabu yanga kupewa shavu clouds? Maajabu yatakuwa chadema kurushwa hewani na uhuru radio tu; na wala si clous na yanga! Nawasilisha.
 
Wameinunua mechi kwa bei chee ( ufisadi mtupu ) c unajua wamejiweka karibu na wakuu. Siku watu wakishtuka watakuwa wameshanyonywa sana.
 
Wanachofanya Clouds ni kutumia umbumbu wa wanachama wa simba na yanga pamoja na viongozi wao namna wanavyoweza kutumia rasilimari watu kuendeleza vilabu vyao
hivi simba ba yanga zinashindwa nini kuwa na vitengo vya masoko tunaona Barcelona na Realmadrid ambazo ni vilabu vinavyoongoza duniani kuwa na mapato makubwa pamoja na kumilikiwa na wanachama
Nawalaumu wanachama wa vilabu hivyo kwa kuchagua viongozi kwa kudanganywa na pilau na ahadi za kuwekwa milangoni pindi timu hizo zinapocheza
Cloud hawana uzalendo kama uzalendo wangesaidia Twiga ambayo inawakilisha Taifa badala ya vilabu au michezo mingine kama ngumi wanaojiandaa kwa olympics
 
Mmh wale hawajasaidia yanga ndugu ni kibiashara zaidi na hata hiyo twiga waliipigia promo japo sio kiviile, na walichangia millioni moja
 
Hivi Clouds bado ipo mi nilidhani imeshakufa aisee...wezi wakubwa hao. Ndala watalia kuhusu mapato yao we subiri tu.
 
Watu bwana!!!!clouds wapo kibiashara kama na wewe unataka promo peleka pakee urushwe kila wakati uone kama watakataa!!!
 
Hawana uzalendo,wapo kwa ajili ya biashara...!!wameinunua mech kupitia Prime Time promotion,lengo lao s kuinua kiwango cha soka na uzalendo,bali kujitengeneza pesa ambazo viongozi wa Yangu wamekuwa wavivu kujua!mpaka nakwambia wachezaji wa Yanga wamechukia sana,mana kuna m2 kawambia Clouds itakusanya hela nyng sana,lakin wao watapewa mgao kidogo!mpaka sasa kambini moral hakuna kabisa...kwa ukubwa wa Timu ya Yanga ni aibu sana kukosa kitengo cha Masoko...NA SIJUI LEO YEBOYEBO WAKITIWA MAGOLI CLOUDS WATAWEKA WAP MBWEMBWE ZAO
 
Watanzania wenzangu mimi naitwa Ruge Mutahaba...mimi ni meneja wa WAFU FM!mi nimecover kila sehemu mpaka kwa mamu fresh!!sasa hivi nimeanza kuingilia mpaka soka mi ndo Ruge bwana...mi mjanja ntapiga bao tu mi mjanja bwana!!halafu watz wenzangu msichonge sana mi nataka nijiimarishe ili nitawale kila k2 hapa bongo!==Hellooo WAFU FM!Mmeshaingilia mpaka soko la soka?mnatupeleka wapi?
 
Back
Top Bottom