Wafanyabiashara Watahadharishwa na Matapeli Wanaojifanya Watendaji wa Bodi

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Na Fatma Kassim, Maelezo,

BODI ya Chakula Dawa na Vipodozi, imetoa tahadhari kwa wafanyabiashara kwamba kumejitokeza baadhi ya watu wanaojifanya ni wafanyakzi wa bodi ambao hupita madukani kuchukua vyakula kama mchele na mafuta, kwa madai ya kwenda kuzifanyia uchunguzi.

Mrajis wa Bodi hiyo, Dk. Burhan Othman Simai alisema wafanyakazi wa bodi hiyo wanapokwenda kufanya ukaguzi katika maduka au maghala wanakuwa na vitambulisho vinavyoonesha kuwa yeye ni mfanyakazi wa bodi pamoja na kuwajazisha fomu maalum wafanyabiashara kwa kuepuka usumbufu.

Aidha aliwataka wafanyabishara wanapofika wakaguzi ni vyema wakawauliza vitambulisho ili kuondoa usumbufu katika bidhaa zao.

Aliwataka wafanyabishara kujenga ushirikiano na bodi yake na wale ambao hawajasajili wafanye hivyo ili kupunguza matatizo kwa walaji.

Katika hatua nyengine Dk. Burhan alisema kutokana na kumaliza mfungo mtukufu wa Ramadhan bidhaa nyingi za chakula zinatolewa na baadhi ya wafanyabishara ambao si waaminifu kwa kuuzwa kwa bei nafuu katika miji mbali mbali ya Zanzibar.

Alisema bodi imejipanga kukabiliana na wafanyabiashara hao na watakaobainika wanauza bidhaa zisizofaa watachukuliwa hatua ikiwemo kuangamizwa.

Aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa bodi endapo watagundua bidhaa ambazo zimepitwa na muda.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom