Wafanyabiashara wasaidiwe

MIUNDOMBINU

JF-Expert Member
Apr 14, 2010
465
96
Wafanyabiashara wasaidiwe
Friday, 06 May 2011 20:36
Happy Lazaro,
Arusha
SERIKALI imeshauriwa kuweka utaratibu maalumu ili kuwasaidia wadau mbalimbali wa biashara wanaotaka kuanzisha biashara zao kuwa na mahali maalumu pa kupata muongozo wa jinsi ya kuanzisha biashara.

Kukosekana kwa utaratibu huo umesababisha biashara nyingi kufa kutokana na kutokuwa na muongozo maalumu wa kibiashara.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Experience Tanzania Ltd wakati akizungumza katika warsha iliyowashirikisha wanawake wajasiriamali, iliyofanyika mjini hapa.

Alisema serikali inatakiwa ifike mahali sasa iweke utaratibu maalumu utakaowasaidia wafanyabiashara kuanzisha baishara zenye tija na ambazo zitawaletea faida kwa ujumla.

Ester alisema endapo kutakuwao na utaratibu huo utahamasisha kwa kiasi kikubwa wafanyabiasha kuanzisha biashara zao kwa uhakika na kufikia malengo waliokusudia.

“Mimi nilipotaka kuanzisha biashara yangu nilikaa chini na kufikiria kwanza nianze kufanyaje ili niweze kufikia malengo yangu wakati kama kungekuwa na muongozo maalumu wa kuonyesha cha kufanya kabla ya kuanzisha biashara nisingepata tatizo lolote,”alisema Ester.

Aliwataka wanawake wanajitokeza kwa wingi kuanzisha baishara zenye tija ili kupata kipato badala ya kukaa na kuwa tegemezi katika familia zao.

Alisema umefika wakati sasa wa wanawake kuchangamka na kujiunga katika vikundi ili kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha.

Source:Wafanyabiashara wasaidiwe
 
Biashara zinakatisha tamaa hasa unapokosa support.
Vizuri kama utaratibu huo utapitishwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom