Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,148
Wafanyabiashara wahojiwa kwa magari ya wizi
Na Mwandishi wetu
27th May 2009
B-pepe
Chapa
Maoni
Magari 10 yanayosadikiwa kuibwa nchini Japan yanashikiliwa na polisi mkoani hapa.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Elias Kalinga alisema kuwa magari hayo ni kati ya 145 yaliyofanyiwa ukaguzi katika operesheni ya kukamata magari yaliyoibwa nchini humo kuanzia Juni 20, mwaka huu.
Kalinga alsiema kuwa idadi kubwa ya magari hayo yanamilikiwa na wafanyabiashara ambao wanahojiwa na polisi ili kujua jinsi walivyoyapata. Magari hayo yanayoshikiliwa ni aina ya Toyota Harrier, Mazda, Maecedez Benz na Toyota Landcruiser.
Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (Hujuma na Operesheni za Uchunguzi) alinukuliwa na vyombo vya habari akisema jeshi la polisi lingetangaza majina ya vigogo walionunua magari ya wizi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Japan jana, lakini hakufanya hivyo.