Wafanyabiashara ndogondogo wa ubungo zaidi ya mia tano wavamia manispaa ya kinondoni.

Lua

JF-Expert Member
May 19, 2011
704
305
wafanyabiashara ndogo ndogo wa ubungo waliondolewa leo wamevamia manispaa ya kinondoni, kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa eneo la mbadala. hiyo imetokea baada ya mbunge wa ubungo john mnyika kuwaarika kuja kwani kutakuwa na kikao fedha na uongozi cha manispaa ambacho mbunge ni mjumbe wa kamati hiyo. hatimaye mara baada ya kumaliza kikao mbunge alifanikiwa kuwatoa ofisini meya na timu yake kuja kuwasikiliza wafanyabiashara hao. na ndipo kamati iliundwa hapo na mwekiti wa kamati naibu meya, na zoezi hilo la kutafuta eneo ndani ya ubungo linaanza leo.
 
Attachments

  • DSC00724.JPG
    DSC00724.JPG
    1.1 MB · Views: 88
  • DSC00714.JPG
    DSC00714.JPG
    1.1 MB · Views: 77
  • Thanks
Reactions: FJM
kwa kweli kwa staili hii tutafika kweli? wanasubiri mpaka tatizo litokee then wachukue hatua? siku zote hizi walikua wapi?
 
haya! Kila kona kuna vuguvugu la vurugu kati ya wananch na serikali, yangu macho
 
Wakati mwingine ni sahihi kabisa kuwaondoa katika maeneo yale ya ubungo kwani ni sehemu hatarishi hasa mitambo ile ya tanesco, pia kwa sisi wapita njia wakati wa asubuhi tukielekea katika kutafuta liziki za kila siku na wakati tukitoka kutafuta liziki upitaji hasa kwa zile sehemu za watembea kwa miguu huwa shida sana,. Lakini tangu waanze kuondolewa yapita leo siku kama ya tatu kwanza pamekuwa pasafi.mtu unapita kwa kujinafasi (wasemavyo watoto wa sikuizi) pia nikaja kungudua sababu ya biashara unaona watu ni wengi kwa sasabu wanasimama kununua bidhaa lakini sasa unaona watu ni wachache kwa kuwa wanatembea amna kusimama simama mara uyu anataka ichi mara mwingine hichi ni wito wangu tu watafutiwe maeneo mbadara ili nao waweze kujiingizia kipato pogezi pia kwa mbunge kuingilia kati swala hilo
 
unaonekana kuwa una asili ya uchoyo, yani mtu asitafute riziki yake eti kisa ww upite barabarani kwa kujinafasi? Chunga sana usichezee maisha ya watu danadana utaumia siku moja´
 
Hakuna mtu yoyote anayependa kwenda Ubungo mataa (chini ya nyaya za umeme) kuuza nguo, maji, viberiti, sahani n.k. Watu wanafanya hivyo kwa sababu that's only way wanaweza kulisha familia zao. Kila kukicha idadi ya hawa wafanyabiashara inazidi kuongezeka. Lakini wafanyeje? Utamwacha mwanao afe njaa au utauza maji chini ya nyaya za umeme? This is what you get Serikali inapotelekeza watu.

Pamoja na kwamba eneo hilo sio maalum kwa biashara lakini serikali makini ingetakiwa ijipange ili kuhakikisha wale wanaofanya biashara wanapata maeoneo -yanayofaa. Tuna mkuu wa mkoa, tuna mayor wa jiji, tuna mkuu wa wilaya, tuna mayor wa mahali husika kwanini haya yote yatokee? Kwa nini hawakukaa na hawa machinga kabla? Mbunge amekuwa ndio mkuu wa mkoa, mayor (expect hana bajeti) kwa nini iwe hivyo?

Utaratibu huu alioutumia Mnyika ni mzuri sana. Huwezi kutatua tatizo la machinga bila ya kuwashirikisha wamchinga wenyewe. Lazima wahusika wake chini na hawa wamachinga ndio solution itapatikana.

CHADEMA ina wabunge wapato 49 tu, lakini wanaonekana kama ndio wanaongoza hii nchi kwa sasa. Serikali ya ccm wako busy kufungua kesi za uchaguzi. Wanapenda madaraka lakini hawataki responsibilities!
 
wafanyabiashara ndogo ndogo wa ubungo waliondolewa leo wamevamia manispaa ya kinondoni, kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa eneo la mbadala. hiyo imetokea baada ya mbunge wa ubungo john mnyika kuwaarika kuja kwani kutakuwa na kikao fedha na uongozi cha manispaa ambacho mbunge ni mjumbe wa kamati hiyo. hatimaye mara baada ya kumaliza kikao mbunge alifanikiwa kuwatoa ofisini meya na timu yake kuja kuwasikiliza wafanyabiashara hao. na ndipo kamati iliundwa hapo na mwekiti wa kamati naibu meya, na zoezi hilo la kutafuta eneo ndani ya ubungo linaanza leo.

Ubungo hakuna soko, Kimara hakuna soko, Mbezi hakuna soko, acha hayo masoko madogodogo. Hili ni bomu kaatika mipango miji. Ile idara ya maji ingepewa manispaa wakajenga soko kubwa la kisasa na hata maji wakapata ofisi humo. Nani aamue. Masoko ni vizuri yawe karibu na standi kubwa za daladala. hivi Tanesco wenyewe wanaona hilo eneo ni muafaka kwao? Wana mipango gani ya muda mrefu? Hili suala linaumiza pande zote, yaani wauzaji na wanunuzi wa bidhaa. Halafu manispaa ikijipanga vizuri itapata mapato mazuri tu.
 
Na likianguka pale pakaripuka basi lawama itakwenda serikalini au tanesco.

Lakini naomba kuuliza, hivi kwa kila anaekuja mjini ni wajibu wa manispaa kumtafutia eneo la kufanyia kazi kwa ajili ya survival yake?
 
Mkongwe, afadhali uwaambie wewe. Hawa CHADEMA wachochezi kila mahali, DSM wanaichonganisha serikali na wamachinga. Huko Arusha wanachonganisha mahakama na serikali. Wanataka nchi isitawalike
 
Hebu acha siasa kwenye mambo yanayohusu mustakabali wa nchi na watu wake! Hivi umeshindwa hata kufikiria jambo dogo kama hilo?! Kweli Tz tunasafari ndefu kuyafikia maendeleo yetu! Ukitoka Kariakoo hadi Kibamba kilometa kama 30 hivi, ni wapi kwenye soko unaloweza kuliita soko kwa ajili ya bidhaa ndogondogo ambalo lina miundombinu ya kueleweka kama mabanda yaliyojengwa kimpangilio, huduma ya vyoo, maji, umeme na sehemu za kutupa taka? Je hiyo serikali unayoitetea kuacha mambo yanajiendea holela holela ndio uwajibikaji kwa wananchi?

Hongera Mnyika kwa kuchukua hatua ya kuwapeleka Machinga kukutana na watesi wao (wakuu wa manispaa) ili waweze kutatua matatizo ya wananchi, kazi waliyoiomba kwa kutoa rushwa ili waipate!
 
JOHN MNYIKA: Matokeo ya Mkutano wa Mbunge na Wafanyabiashara Ndogondogo
Msome hapa utapata ukweli kuwa yeye ndiye aliyewachochea:

Kwanini hakuwapa ufumbuzi mpaka awaambie waende Manispaa? Kwanini hakushughulikia matatizo yao bila kumtaja Rais Kikwete? Rais Kikwete anahusika vipi na zoezi lililofanywa na Polisi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa?

....ndiyohiyo
 
Na likianguka pale pakaripuka basi lawama itakwenda serikalini au tanesco.

Lakini naomba kuuliza, hivi kwa kila anaekuja mjini ni wajibu wa manispaa kumtafutia eneo la kufanyia kazi kwa ajili ya survival yake?

ndiyo maana tuna wataalamu wa mipango miji.
 
Mnyika anatatua tatizo,wewe unataka vijana warudie kazi ya kukwapua!kwa nini mitambo hatarishi isijengwe pembezoni?
 
Na likianguka pale pakaripuka basi lawama itakwenda serikalini au tanesco.

Lakini naomba kuuliza, hivi kwa kila anaekuja mjini ni wajibu wa manispaa kumtafutia eneo la kufanyia kazi kwa ajili ya survival yake?
Binti mkongwe, serikali inajukumu la kuandaa miundo mbinu ili wananchi waweze kundesha maisha yao bila hatari yoyote.
Ni jukumu la serikali kuandaa plan za miji, kama viwanja vya michezo, hospitali, masoko nk. Yaani hilo ni jukumu lisilokwepeka, sasa niambie wewe, serikali yako inafanya hivyo? Je haikusanyi kodi? Wewe unaishi kulikopimwa?, kwanini hakuna mipango miji almost 80per cent ya maeneo wanayoishi watu hapa Dar hayajapimwa, sasa hilo ndio chanzo cha matatizo yote haya, ni hiyo serikali yako!
 
Na likianguka pale pakaripuka basi lawama itakwenda serikalini au tanesco.

Lakini naomba kuuliza, hivi kwa kila anaekuja mjini ni wajibu wa manispaa kumtafutia eneo la kufanyia kazi kwa ajili ya survival yake?

iwe wazi kwamba sababu ya kuwafukuza machinga ubungo ni sehemu ambayo siyo rasmi kwa biashara hiyo na sio kuendelea kumung'unyamung'unya maneno hapa.

kuwepo kwa plant ubungo c vyanzo vya kuwatimua wamachinga hawa eti ni sehemu hatarishi, serikali imeshindwa kuona hatari hiyo hata ikaamua kuweka plant hizo za gas hapa ubungo, serikli haijui athari watakazo pata wananchi wa ubungo kutokana na mlipuko wa gas ya umeme, serikali haijui jinsi gn moto wa gas inavyosafiri kwa haraka pamoja na hewa?

Binafsi siungi mkono wamachinga kufanya biashara sehemu isiyo rasmi ila pia siungi mkono kwa serikali badala ya kutoa sababu ya msingi inamuyamunya maneno,...inamaana kusingekuwa na vyanzo vya umeme ubungo mngewaacha wamachinga hao?
 
JOHN MNYIKA: Matokeo ya Mkutano wa Mbunge na Wafanyabiashara Ndogondogo
Msome hapa utapata ukweli kuwa yeye ndiye aliyewachochea:
JOHN MNYIKA: Matokeo ya Mkutano wa Mbunge na Wafanyabiashara Ndogondogo

Kwanini hakuwapa ufumbuzi mpaka awaambie waende Manispaa? Kwanini hakushughulikia matatizo yao bila kumtaja Rais Kikwete? Rais Kikwete anahusika vipi na zoezi lililofanywa na Polisi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa?

....ndiyohiyo

wewe umeambiwa manispaa inashughulila na masuala ya nani kama si hao waliokwenda. usipende kula kundi utakosa haja kuu uadhirike!
 
Kama tatizo ni hatari, vipi jengi la TANESCO liko salama? wananchi wenye nyumba kuzunguka eneo lile vipi wako salama? Nakubaliana na waliounga mkono kuondolewa kwa machinga pale, TATIZO ni kwamba wanapelekwa wapi? machinga anunue ndizi toka pale mahakama ya ndizi halafu unasema umemtafutia eneo sehemu hiyohiyo alipo nunua tena?, Vipi ahadi ya baba lizi kuhusu machinga complex kila manispaa ya kinondoni iko wapi? Kwa nini kila kona ya nchi kunakuwa na matatizo ninyi wenye dhamana ya kuongoza hamuoni tu kwamba mambo yanawashinda au ndo kila kitu mnasingizia CDM wanataka nchi isitawalike, kweli mkitatua matatizo ya wananchi hata hao CDM watasema nini? NAAMINI MAGAMBA HAMUWEZI KUONGOZA NCHI HII TENA
 
Back
Top Bottom