Wafanyabiashara karibu wote wagoma,Hali ni tete nchini.

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,837
Wananchi wa Tanzania wamekuwa katika wakati mgumu wa kununua bidhaa mbali mbali baada ya wafanyabiashara wa maduka karibu yote kufanya mgomo wa kushitukiza wakiishinikiza serikali kwa mambo matatu, ya kumpa dhamana mwenyekiti wao kitaifa,Bw.Johnson Minja,kuongezeka kwa kodi asilimia mia moja,na matumizi ya mashine za EFDS.


Akizungumzia mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea nchini waziri mwenye dhamana mkuya amesema serikali inaangalia hatua za kisheria dhidi ya wafanyabiashara wanaoendelea na mgomo huo kwani wamekuwa wakisababisha usumbufu mkubwa siyo tu kwa wananchi bali hata kwa wafanyabiashara kutoka nje.
 
Serikali ya Tanzania ni km MAMBA mwenye kichaa. Inakusanya kodi kwa fujo bila kujali mahitaji ya walipa Kodi.

Yaani Hii serikali yetu Sijui inaweka watu wenye Nazi kichwani?
Vipi upende mayai ya Kuku hali ya kuwa Kuku humjali?
Mnalazimisha Wafanyabiashara Watumie mashine ambazo Zinafanya kazi zao kuwa Ngumu siku hadi siku, wakilalamika mnajifanya VIZIWI!
Sasa Mtakula Jeuri yenu. Mapato sasa hampati, Ajira zinapungua! Wezi wataongezeka! Ujambazi ndio huo tena hata Askari hawako salama.

Yote haya yanatokana na Kuweka Wachumia Tumbo ktk Idara Nyeti km TRA. Badala ya Kuwapa Wenye Elimu zao kazi hii mnawapa Watoto wa Shangazi zenu na Mashemeji zenu.

Msipochunga Mtaiingiza hii nchi ktk balaa km za hao majirani zetu.
Kumbuka Binaadamu mwenye njaa yuko tayari kufanya lolote apate Kula.
 
Hii nchi viongozi wanajua kuvaa suti tu na kunywa bia,wakiwa na pesa kazi nyingine umalaya kuchukua wake za watu na mabint wa watu tu,
Hakuna kwenye afadhali nchi mbovu hovyo imeoza, viongozi wetu wameziba masikio na pamba hawashauriki wala hawana future, hakuna hata kimoja tunachofanya kwa uhakika,mradi tu tuna nchi na serikali,
Mpango wangu wa kuomba uraia Somalia sijasitisha kabisa, bora nikaishi na wanaume wa kazi ukileta ujuaji tunakuondoa tu ndio heshima inakuja
 
Back
Top Bottom