Wafadhili mmeidekeza Tanzania, bado tunataka nyonyo!

Mwanakijiji uliyosemaq ni sahihi kabisa ila kwanza kabla ya kuifukuza hii misaada tuwapige mateke hawa viongozi wabovu( CCM). Chama cha CCM tukiweke kando ili nchi hii iweze kusukwa upya. Hatuwezi kuwa na chama ambacho kinajiendesha kwa kuibiibia serikali/ watanzania.
Tanzania ni nchi yenye pesa na ushahidi uko wazi kwenye matumizi ya serikali na Bunge. Kwa sababu tuna pesa za kutosha ndo maana tunanunua magari ya milion 100 hadi 200. Wafanyakazi wanapeana posho za vikao hadi 500,000 kwa kikao cha masaa tu.
Turekebishe kwanza uongozi ili tuweze kupata watu bora na wenye uwezo wa ku-manage pesa zetu.
 
Ni kweli misaada inadumaza. Lakini ninakataa kukubali kuwa misaada ya kigeni ndiyo imepelekea nchi yetu kuwa maskini. Misaada ni chachu ya maendeleo kama wanaopewa misaada hiyo wamejiandaa kuitumia ipasavyo. Ninafikiri tatizo liko kwetu sisi tunaopewa misaada hiyo na sio kwa wanaotoa misaada na aina misaada wanayotoa. Ukiachana na misaada, Fedha za ndani pekee tumeshindwa kuzitumia kikamilifu. It's like we don't know what we want. And if we know, nobody is commited to pursue our objectives. Kwa kujua udhaifu wetu, kila mfadhili ana utaratibu wake wa kuhakikisha pesa yake inatumika kadiri anavyoona inafaa. Historia ya matumizi yetu ya misaada imetufikisha hapa tulipo.

Na hata wakisema, utegemezi wa bajeti yetu ni asilimia 0, what difference will it make? Unafikiri kutakuwa na jitihada za kuziba hilo pengo? Kitakachotokea ni kuwa baadhi ya miradi itakuwa - underfunded. Nothing else! Probably, wataongeza kodi na kuendelea kuwakandamiza walalahoi. Na hili la kupungua kwa utegemezi wa bajeti na kauli za kisiasa tu. The problem lies on the lack of prioritization and not on the share of the budget that comes from outside. Foreign aid is supposed to compliments efforts rather than prohibit the recipient from making effort to achieve the desired condition.

Trade rather than aid is a good idea. Je tuko tayari kunufaika na fursa za kibiashara? Take an example of AGOA. Did we do our best?

And why are we waiting for the cut off of foreign aid to start acting responsibly? To me, blaming the foreign aid for our mess is simply aiming at a wrong target.
 
...mwenye nyonyo tamu zaidi ni sisi au wao?

...maziwa kutoka kwenye nyonyo zetu ni pure organic, je yao yakoje?

... conversely, in the same capacity, since wafadhili are already addicted to our organic milk (liquid and powder), the challenge is how to wean them from, bearing in mind that it is hard to deal with addicts and addiction by itself!!
 
Last edited:
Azimio.. yawezekana hatujiamini kuwa tunaweza kusimama! Nyie subirini tu muone jinsi nchi zote zilizokumbwa na majanga na zinatuzunguka zikitupita kwa kasi kama tumesimama!

Mwanakijiji:

Matatizo makubwa ya kufanya nchi kuendelea kuwepo kwenye misaada ni nyinyi MA-ELITE. Misaada ikikatwa misaada taabu na misukosuko inayoambatana na kukatwa misaada hamtaweza kuvumilia.
 
Mwanakijiji:

Matatizo makubwa ya kufanya nchi kuendelea kuwepo kwenye misaada ni nyinyi MA-ELITE. Misaada ikikatwa misaada taabu na misukosuko inayoambatana na kukatwa misaada hamtaweza kuvumilia.

ah.. kwenye kundi la elite miye simo! wakikata misaada angalia picha yangu nimebeba nini!
 
ah.. kwenye kundi la elite miye simo! wakikata misaada angalia picha yangu nimebeba nini!

Hilo jembe ulilobeba ni usanii tu wa JF. Kumbuka hata baadhi ya wanaIsrael walikuwa wanamlalamikia Musa kuwa warudi Misri kwani walichoshwa na manner na walitamani mboga mboga za mto Nile. Hao ni watu waliokombolewa kutoka utumwani.

Je nyie watu huo mnaopewa misaada na mkiwa huru si mtaanzisha hata vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kutaka misaada irudi.
 
hahahahaha.. haya bwana..
 
Mwanakijiji
Hii misaada wanayotupa si kwamba wanatuangushia ttunaililia vibaya sana,Waziri ama Raisi anafunga safari ya gharama just kwenda kuomba msaada tu na si zaidi.Na akirudi bila msaada anona ziara yake haikuwa na mafanikio.Sasa tizama hiyo ziara yenyewe hilo kundi linaloondoka na Rais kiasi hata hao wanaoombwa hiyo misaada wanashangaa na huo msafara.Tunasema wanatudekeza wao wanatuonea huruma vibaya sana kwa sababu wametustudy sana na wanajua udhaifu wetu.wanajua hadi kiasi gani tutakifuja kabla hawajatupa.Wanatucheka na kutukebehi masikini sisi.Na tukiimagine waafrica bila misaada ni aibu.muhimu tukaze buti new generation is needed.
THINK TWICE.

SAHIBA.
 
hahahahaha.. haya bwana..

Mwanakijiji:

Nilikuwa na-genaralize tu. Misaada inalinda serikali zilizokuwepo madarakani. Pamoja na mapenzi yako makubwa kwa Mwalimu, kama angakataa misaada 1981, nadhani hilo jembe lako lingemfikia kichwani.

Ni vyepesi sana kwa sisi tulio nje kusema tunaweza kuwa na program ya kuondokana na misaada. Lakini ukipewa urais na kukawa na watu wenye kukusubiri kulipwa mishahara na wewe mwenyewe kutaka kubaki madarakani, basi njia nyepesi ni kubakisha misaada.

Misaada inaweza kuachwa lakini tupo tayari kufanya programs za kupunguza misaada :confused: Kwa maana fiscal displine kwa miaka kama mitano hivi.
 
Zakumi, leo hii imetangazwakuwa serikali ya Japani itatoa msaada wa karibu Shilingi bilioni 20 kusaidia usambazaji wa Maji Zanzibar ikiwa ni sehemu ya pili ya mradi wa maji. Tutatia sahihi msaada huo na tutaupokea kwa furaha.

Wakati huo huo serikali ya Tanzania imeshindwa kukusanya shilingi bilioni 40 toka Kagoda na hadi hivi sasa wanasema hawajui Kagoda ni nani? Unafikiri wanaharaka ya kumjua Kagoda ili wapate zile bilioni 40 zetu? Of course not!

Kwa kadiri wajomba zetu wanatupatia fedha za kufanya mambo mbalimbali ndivyo hivyo hivyo watawala wetu hawaoni uharaka, ulazima wala haja ya kuhakikisha fedha zetu zinakuwa accounted to the last penny.

Kuna mabilioni yaliyoenda Mwananchi Gold, Tangold na wengine, unafikiri wana haraka ya kuyatafuta wakati wajomba wamekuja na mapakacha ya misaada?
 
Last edited:
Kupata msaada ni jambo moja na kujitahidi ili Bajeti isiwe tegemezi ni jambo jingine. Kweli CCM kwa kipindi chote ilichoongoza imeshindwa katika hili la kuweka mazingira angalau tuweze kupunguza kwa hali ya juu kutegemea misaada. Rasilimali tunazo ila jinsi ya kufaidika nazo ndio imekuwa tatizo. Hatuna vipaumbele, tunakulupuka linapotokea tatizo. Mfano ni umeme, hatuna sera kamilifu ya kuangalia kuwa watu wanaongezeka na viwanda pia, hivyo nishati hii ni muhimu siku hadi siku, umeme ulipoleta tatizo ndio pale tukasikia wengine wakitafuta mvua za kemikali kule Thailand na kuingia katika matatizo kama ya Richmond. Ikija njaa, wakati TZ kuna maeneo yakiwekwa sawa yanalisha TZ nzima na tukauza nje, lakini wapi?.

Kwa sasa na hata baadae yoyote ama chama chochote kitakachoongoza serikali bado misaada itatakiwa tu. Hatujafika sehemu hatuhitaji msaada, ila tunatakiwa jua jee hii misaada inapelekwa wapi. Sekta muhimu kama maji, afya, shule, miundombinu nk. Vipaumbele vyetu si kukarabati viwanja ama semina na makongamano ya jinsi ya kumuondolea mTZ umasikini. Afrika ya Kusini na Misri ni nchi zina Uchumi mzuri kuliko wetu, lakini bado zinapokea misaasa kibao toka nje. Ni kuamua tu tunaomba misaada kwa kuifanyia nini?, na jee inatumika kwa lengo?.
 
Zakumi, leo hii imetangazwakuwa serikali ya Japani itatoa msaada wa karibu Shilingi bilioni 20 kusaidia usambazaji wa Maji Zanzibar ikiwa ni sehemu ya pili ya mradi wa maji. Tutatia sahihi msaada huo na tutaupokea kwa furaha.

Wakati huo huo serikali ya Tanzania imeshindwa kukusanya dola bilioni 40 toka Kagoda na hadi hivi sasa wanasema hawajui Kagoda ni nani? Unafikiri wanaharaka ya kumjua Kagoda ili wapate zile bilioni 40 zetu? Of course not!

Kwa kadiri wajomba zetu wanatupatia fedha za kufanya mambo mbalimbali ndivyo hivyo hivyo watawala wetu hawaoni uharaka, ulazima wala haja ya kuhakikisha fedha zetu zinakuwa accounted to the last penny.

Kuna mabilioni yaliyoenda Mwananchi Gold, Tangold na wengine, unafikiri wana haraka ya kuyatafuta wakati wajomba wamekuja na mapakacha ya misaada?

Mwanakijiji:

Nakusikia. Na mradi ukimalizika atakwenda Rais wa Zanzibar na kufungua akisema tumetimiza manifesto.

Misaada inadumaza innovation na vilevile inapunguza mzunguko wa pesa iwapo itatumika kwa muda mrefu.

WaJapan watakapo leta mradi wataleta na wataalamu wao, kitu ambacho kitafanya wataalamu wetu wasipate uzoefu.

Vilevile kazi zingefanyika na watanzania basi, watanzania hao wangeweza kuziweka pesa katika mabenki ya Tanzania na ku-diversify biashara yao.

Inabidi waangalie program za sasa za Marekani za kufufua uchumi. Zote zimelenga kuwapa watu miradi hii pesa izunguke na baadaye uchumi ukue. Misaada haizungushi pesa.
 
Kupata msaada ni jambo moja na kujitahidi ili Bajeti isiwe tegemezi ni jambo jingine. Kweli CCM kwa kipindi chote ilichoongoza imeshindwa katika hili la kuweka mazingira angalau tuweze kupunguza kwa hali ya juu kutegemea misaada. Rasilimali tunazo ila jinsi ya kufaidika nazo ndio imekuwa tatizo. Hatuna vipaumbele, tunakulupuka linapotokea tatizo. Mfano ni umeme, hatuna sera kamilifu ya kuangalia kuwa watu wanaongezeka na viwanda pia, hivyo nishati hii ni muhimu siku hadi siku, umeme ulipoleta tatizo ndio pale tukasikia wengine wakitafuta mvua za kemikali kule Thailand na kuingia katika matatizo kama ya Richmond. Ikija njaa, wakati TZ kuna maeneo yakiwekwa sawa yanalisha TZ nzima na tukauza nje, lakini wapi?.

Kwa sasa na hata baadae yoyote ama chama chochote kitakachoongoza serikali bado misaada itatakiwa tu. Hatujafika sehemu hatuhitaji msaada, ila tunatakiwa jua jee hii misaada inapelekwa wapi. Sekta muhimu kama maji, afya, shule, miundombinu nk. Vipaumbele vyetu si kukarabati viwanja ama semina na makongamano ya jinsi ya kumuondolea mTZ umasikini. Afrika ya Kusini na Misri ni nchi zina Uchumi mzuri kuliko wetu, lakini bado zinapokea misaasa kibao toka nje. Ni kuamua tu tunaomba misaada kwa kuifanyia nini?, na jee inatumika kwa lengo?.

Mfumwa, my argument ni kuwa hatuhitaji misaada ili tuendelee!! Misri na Afrika ya Kusini kama wanapokea misaada hilo lao. Labda na wenyewe wana mentality kama ya kwetu?

a. Je Tanzania ina uwezo wa kupata pato la kiasi gani kutoka kwa shughuli zake za ndani na mauzo ya nje?

b. Je, katika miradi yetu tunapanga vipi vipaumbele vya nini tunaweza kufanya? Kwa mfano kuna miradi mitatu ambayo inakuja Mradi wa Flyovers, mradi wa Vitambulisho, mradi wa mabasi yaendayo kasi n.k Je ni kipi tufanye kwanza, je ni lazima tufanye vyote kwa wakati mmoja?

c. Bila kuwa na good domestic consumer base ni vigumu kuzalisha kwa faida kwa sababu hatuwezi kutegemea soko la nje kama ndani watu hawali! So, how do we empower and stimulate internal consumption of our own products?

d. Je ni kwa jinsi gani tunatengeneza vitu ambavyo vina ubora wa hali ya juu na kwa gharama afueni zaidi kuliko vitu hivyo hivyo toka nje? Kama kununua tenga la nyanya toka Lushoto ni bei ghali kuliko kuagiza tenga hilo toka Afrika ya Kusini, kwanini watu wanunue nyanya toka Lushoto?

e. Kama wafadhili wanataka kusaidia basi wasaidie vitu ambavyo wao wenyewe watasimamia, wataviendesha na viwe chini yao, wasiwaachie Watanzania!!!! Watanzania wakitaka waanzishe vya kwao!!!
 
Right. Na katika miradi uliyoiorodhesha, hakuna hata mmoja ambao ni kipaumbele, ukizingatia matatizo tuliyonayo. Ni mfano tu.
 
Mfumwa, my argument ni kuwa hatuhitaji misaada ili tuendelee!! Misri na Afrika ya Kusini kama wanapokea misaada hilo lao. Labda na wenyewe wana mentality kama ya kwetu?

a. Je Tanzania ina uwezo wa kupata pato la kiasi gani kutoka kwa shughuli zake za ndani na mauzo ya nje?

b. Je, katika miradi yetu tunapanga vipi vipaumbele vya nini tunaweza kufanya? Kwa mfano kuna miradi mitatu ambayo inakuja Mradi wa Flyovers, mradi wa Vitambulisho, mradi wa mabasi yaendayo kasi n.k Je ni kipi tufanye kwanza, je ni lazima tufanye vyote kwa wakati mmoja?

c. Bila kuwa na good domestic consumer base ni vigumu kuzalisha kwa faida kwa sababu hatuwezi kutegemea soko la nje kama ndani watu hawali! So, how do we empower and stimulate internal consumption of our own products?

d. Je ni kwa jinsi gani tunatengeneza vitu ambavyo vina ubora wa hali ya juu na kwa gharama afueni zaidi kuliko vitu hivyo hivyo toka nje? Kama kununua tenga la nyanya toka Lushoto ni bei ghali kuliko kuagiza tenga hilo toka Afrika ya Kusini, kwanini watu wanunue nyanya toka Lushoto?

e. Kama wafadhili wanataka kusaidia basi wasaidie vitu ambavyo wao wenyewe watasimamia, wataviendesha na viwe chini yao, wasiwaachie Watanzania!!!! Watanzania wakitaka waanzishe vya kwao!!!

Hakuna nilikosema tunahitaji misaada ili tuendelee, lakini vilevile yaweza kuwa vichocheo vya maendeleo. Na msaada waweza kuwa madaktari toka Cuba ama waalimu wanaoletwa kuja kufundisha Kiingereza na Physics ktk shule zetu. Kwa hiyo msaada ni kichocheo cha maendeleo.

Kuzungumzia kuwa TZ inaweza kupata kiasi gani kwa shughuli za ndani na mauzo ya nje inategemea tunaangalia wapi?. Mfano leo hii watu wanaweza lima Pamba, korosho nk, ukifika kwa soko la dunia unakuta kuna watu wakulima wao walipewa ruzuku, bei yao iko chini, sisi hatukuwapa ruzuku, bei iko juu. Hivyo inatubidi kuuza kwa bei ya hasara. Hivyo ni bora kuweka mkakati wa kutengeneza viwanda ambavyo hatutatuza malighafi nje, na hata kama tutauza iwe kidogo. Hilo la miradi “post” yangu iliyopita nimelieleza, kuna mambo muhimu ya kuwekeza kwanza, ila kama fedha zipo mradi kama flying over na mabasi yaendayo kasi ni muhimu sana kuanza mapema. Ila iratibiwe tu vizuri ili isije baada ya miaka 20, tatizo linaanza tena. Na hili la barabara za juu, yawezekana bado hatujafika huko, twaweza vifanya hata vichochoro njia mbadala pamoja na kutumia eneo la bahari pia. Manake maendeleo hayaji kwa watu kuchelewa kazini, bidhaa kuchelewa njiani. Hili tatizo linatakiwa kushughulikiwa haraka kuliko la vitambulisho vya Taifa japo nalo ni muhimu.

Kuwa na soko la ndani hili ni tatizo la TZ, tunaweza kujiuliza kuna watu wako Mara, Mwanza nk, lini walitembelea Mbuga ya Serengeti. Kuna watu wako Mlima Kilianjaro, wanauona tu kwa mbali, lini waliupanda. Hili linaanzia mbali, hatuna muda wa kuwekeza kwa watoto wetu, na wala hatukuwekezwa kukua ili tutembelee vivutio vya utalii, kwa kufanya hivyo tunakuza uelewa wetu na kuzidisha pato la Taifa. Hawa jamaa huwa wanapendelea kuwakaribisha watoto wanaosoma “International Schools”, lakini sisi wa Mihayo, Msinjahili, Mkuyuni hatupati hizi huduma. Hawa wa kwenye vivutio vya utalii kama wangekuwa wanatangaza punguzo kwa wanafunzi, Waalimu wangewapeleka na kwa kufanya hilo, utalii wa ndani ungekuwa mkubwa. Hapo acha mazao ya chakula pia.

Kuweza kuvishindanisha vitu vyetu na vya nje inatakiwa mkakati wa kudumu kusaidia wakulima wetu. Bila hawa kusaidiwa kupata pembejeo za kilimo kwa bei nafuu ni kazi, ruzuku ni muhimu kwa serikali yetu. Lakini kama nivyogusia juu, hatuwajengi watoto wetu wathamini kilicho chetu. Pilipili za Dabaga nani ananunua, kila mtu atataka nunua kitu cha nje. Hii inaanzia mbali watu kuwekezwa kuthamini vitu vyao. Kama hatutapigana wenyewe kuweka nchi safi, basi tutaona hata karanga zitatoka Afrika ya Kusini kama sio China.
 
Mfumwa una mawazo mazuri. Lakini siku zote napata shida sana kuelewa tatizo liko wapi. Ukimuliza Rais au Waziri, atatoa maelezo kama uliyoyatoa. Then, unabaki kujiuliza, what is the problem? Hakuna utekelezaji. Kila mtu anajitahidi kuwa hodari wa kutumia lugha na kusubiri watu wamsifie. That's all! Ninaangalia documentary hapa by Soledad of CNN. Inaitwa "Blacks in America". Dude, blacks tunamatatizo kila mahali. Si Tanzania peke yake. I think we need more research to figure out our problem. is it genetical or something?
 
Hakuna nilikosema tunahitaji misaada ili tuendelee, lakini vilevile yaweza kuwa vichocheo vya maendeleo. Na msaada waweza kuwa madaktari toka Cuba ama waalimu wanaoletwa kuja kufundisha Kiingereza na Physics ktk shule zetu. Kwa hiyo msaada ni kichocheo cha maendeleo.

Mifano hiyo ya misaada uliyoitoa ndiyo ninayoikataa. NI misaada isiyo ya lazima. Tanzania haiitaji walimu wa kigeni kufundisha masomo ambayo tunauwezo wa kuyafundisha!

Lakini pia ninachokataa ni hii dhana kuwa misaada ni kichocheo cha maendeleo. Si kweli, kwa sababu kama ingekuwa kweli Tanzania lingekuwa Taifa lililoendelea kweli ukilinganisha na kiwango cha misaada iliyopokea.
 
KWa kweli ndiyo maana nikasema domestic industries ni za muhimu na miundo mbinu nyingine kwa ujumla.ni bora hata misaada tunayopokea tuiwekeze huko.huwezi ku-stimulate domestic consumers without purchasing power.So,the gvnt has to increase the expenditure na kuwekeza ktk miradi mikubwa ya jamii itakayotoa ajira kwa wananchi wengi.

Kufanya hivyo serikali itakua imeua ndege wawaili kwa jiwe moja.Kwanza maendeleo kutokana na mradi wenyewe na pili,ajira itokanayo na mradi itaongeza living standard na watu watakua na purchasing power kitu kitakachowafanya wawe na demand ya bidhaa,sasa kama tuna domestic products zitauzwa

Pia serikali iweke restriction ktk import tukiwa na hivyo viwanda ili kuvilinda,na hiyo ni kwa kutumia ushuru na kodi kubwa kubwa.Wale matajiri jeuri watakaokaidi na kuagiza nje basi serikli itapata kodi kubwa na kuvipa viwanda vyetu ruzuku kutokana na kodi hizo ili kuviimarasha
 
Mifano hiyo ya misaada uliyoitoa ndiyo ninayoikataa. NI misaada isiyo ya lazima. Tanzania haiitaji walimu wa kigeni kufundisha masomo ambayo tunauwezo wa kuyafundisha!

I am not getting it. Ni nini tatizo la kuwa na mwalimu wa Kiingereza au Physics kutoka Marekani ambaye huingii gharama yoyote kumleta? If anything, tunanufaika na ujuzi alionao. Don't you see the added value from having a foreign teacher imparting knowledge to our young fellows? Actually, hii ndio misaada tunaihitaji: Afya, elimu. We don't need cash. We need to build a healthier and skilled society. Na hawa wenzetu wana ujuzi ambao hatuna. Mwl. wa Shule ya Msingi Katerero, Bukoba si sawa na Mwl. wa Shule ya Msingi kule Hamden, Connecticut. Interaction kati ya hawa walimu wawili itawanufaisha wote na jamii kwa ujumla. Mwl. wa Bukoba atajifunza jinsi mwenzake alivyopiga hatua wakati yule wa CT atajifunza ni jinsi gani mwenzake yuko nyuma katika kila kitu.

We have a lot of weaknesses and blaming the foreign for our poverty is by itself a weakness.
 
This is a serious issue....misaada ni kilema kibaya......tatizo ya rinchi hiri ni kuwa kila kitu kinapelekwa kiCCM na Makambalians ndio wanaoamua destiny ya nchi.....
....hakuna maoni ya kitalaam yanayokuwa considered au kusikilizwa......inakera sana....

Hapo ndipo kumekaa kitaaluma zaidi kwingine siasa nyingi.....unajua mamabo haya ukiweka siasa nyingi haki ya nani tutaishia kupiga mayowe mpaka vidole viote sugu....

hao wafadhili mie huwa napigwa butwaa sana kuna sekta nyeti huwa hawagusi hasa sekta ya elimu.....mara nyingi hata misaada wanayotoa utasikia madawati sijui chaki na vidudu vya ovyoo ovyo..

huyo raisi wenu juzi nimemuona akipokea wanafunzi sijui wa majuu nao yeye kashindwa kuweka na hajakutana na uongozi wa wanafunzi tanzania.....kuna kazi kubwa sana kufika......

.........kuna mambo yanatia aibu sana yaani na huyo raisi sijui hamnazo au namna gani sijui.....ati bush alitoa vyandarau ambavyo sisi tunaweza kuchangishana na kutoa......

contribution za kitaaluma wanaJF zinahitajika baada ya blah blah za kisiasa sasa ifikie na sisi tujiangalie jamani huyu mkwere hatabiliki hapaswi kutegemewa.....yaaani anatoka magogoni kwenda misungwi kufungua kisima cha mil 20!

Mkuu hii imenikumbusha pia PM Pinda juzi juzi alikuwa Moshi eti kikubwa mno alicho kisema wananchi waondoe nyasi zinazoziba mfereji wa umwagiliaji! Nilipigwa na butwaa kwamba hivi nalo hilo linasubiri waziri mkuu aje kulisemea?
 
Back
Top Bottom