Wafadhili ktk mradi wa kujenga shule

gvyagusa

Member
Aug 25, 2010
11
8
Wana JF

Mkoa wa Kigoma ni moja ya mikoa ambayo maendeleo ya kielimu bado yako chini sana (kuna vyuo viwili tu vya ualimu na hakuna shule nyingi - hata zilizopo ufanisi wake ni mdogo ukilinganisha na mikoa mingine).

Mwaka juzi nilikuwa likizo kijijini kwetu huko Kigoma, wanakijiji wakanieleza kuwa watoto wao wengi wanasoma shule za kata na hazina walimu wala vitabu - wakaniuliza mimi nikiwa nimesomea ualimu nitawasaidiaje ili watoto wao nao wasome hadi kufikia elimu niliyonayo?

Kwa kuguswa na suala la hilo na nikiwa pia ni mwenyeji wa huko nimeazimia kutoa huduma hiyo mimi mwenyewe (japo vijisenti havitoshi kuwekeza katika mradi huo), hivyo najipanga ili nianzishe shule yangu itakayokuwa na 3-WINGS: Shule ya Msingi (English Medium), High School (Sayansi na Biashara) na Chuo cha Ualimu (kwa ajili ya Diploma na Grade A) hususani katika maeneo ya vijijini.

Kwa hivi sasa nimeomba kuuziwa ardhi kijijini kwetu mkoani Kigoma na serikali ya kijiji na wananchi wenyewe wameafiki sana mradi huo na wako tayari kuniuzia sehemu ya ardhi kijijini hapo (eka 150) na wangependa ujenzi wa shule hizo ukamilike mapema ili watoto wao wasome.

Pamoja na kufanya biashara, malengo yangu ni kuanzisha mfumo wa kipekee katika katika kutoa elimu, mfumo ambao utawawezesha wazazi/wanafunzi kulipa ada nafuu na hivyo kuwa msaada wa maana sana kwa watoto kutoka familia maskini kwani wengi hawasomi shule nzuri za private kutokana na kukosa uwezo kifedha. Hivyo nikifanikiwa kujenga shule hizo nakusudia kuanzisha mfumo wa Learning by Doing and Earning.

Katika mfumo huo pamoja na kusoma masomo ya kawaida kwa ajili ya kufanya mitihani ya kitaifa wanafunzi watafundishwa pia stadi za ujasiriamali na kuanza kuzalisha bidhaa (kilimo, ufugaji, ufundi nk) wakiwa bado ni wanafunzi na kuuza bidhaa hizo hapo hapo shuleni na hata nje ya shule. Kwa hiyo mwanafunzi ataweza hata kujilipia ada yeye mwenyewe bila msaada wa mzazi - na inawezekana.

Wana JF, naombeni mnipe habari kuhusu mashirika au hata watu binafsi wanaoweza KUFADHILI mradi wangu kwa hatua za awali ili kukamilisha walau madarasa 3-5 ya kuanzia. Nimeulizia maswala ya mikopo naona suala hilo linawezekana kama tayari mradi unafanya kazi (operational) na siyo kuanzisha.

Kwa kutegemea hela yangu mwenyewe inaweza kuchukua muda mrefu kidogo kukamilisha ujenzi huo.

Nawasilisha...


==================================
…..”Those who receive this privilege therefore, have a duty to repay the sacrifice which others have made. They are like the man who has been given all the food available in a starving village in order that he might have strength to bring supplies back from a distant place. If he takes this food and does not bring help to his brothers, he is a traitor. Similarly, if any of the young men and women who are given an education by the people of this republic adopt attitudes of superiority, or fail to use their knowledge to help the development of this country, then they are betraying our nation" - JULIUS KAMBARAGE NYERERE
 
Ndugu, wazo lako ni zuri sana.Ni bora ungejitahidi uanze na hata darasa moja kwa pesa yako,then hapo utakua na njia nzuri ya kuwashawishi wafadhili.Ni bora kupata mawazo kutoka kwa watu wanaoendesha shule binafsi,hasa shule za mission watakupa mwanga jinsi ya kupata wafadhili.Kila la Kheri.
 
hizo n habari njema kwa wakazi wa kigoma na vijiji vyake. ni wazo zuri sana, kilichobaki asa, jitaidi sana angalau ujenge hata madarasa mawili na ofisi za walimu t...
 
Back
Top Bottom