wadau tutangaze mali zetu!!

Mimi ninamiliki vifuatavyo:-

1. Najimiliki mimi mwenyewe (Sourse.. niliumbwa na Mungu)
2. Nammiliki partner wangu wa maisha na mzazi mwenzangu (sourse.. tulikutana ujanani then married)
3. Namiliki mtoto mmoja wa kike(very beatful 1) na mwingine mtarajiwa (source... wote mnajua)

CAG nikague
Hizi ni mali pekee nilizonazo.
 
NAMILIKI SIMU YA MKONONI MCHINA 33,000, VIATU 10000,
mbuzi na kondoo 4 100,000
shuka,nguo na vinginevyo 130,000
jumla sijui plus goodwill yangu mwenyewe plus girlfriends plus vinginevyo, ntatoa idadi baadae
 
Mimi ninamiliki vifuatavyo:-

1. Najimiliki mimi mwenyewe (Sourse.. niliumbwa na Mungu)
2. Nammiliki partner wangu wa maisha na mzazi mwenzangu (sourse.. tulikutana ujanani then married)
3. Namiliki mtoto mmoja wa kike(very beatful 1) na mwingine mtarajiwa (source... wote mnajua)

CAG nikague
Hizi ni mali pekee nilizonazo.
mkuu hujasema huyo patner wako anathamani gani (mahari uliyotoa)
CAG nikague! i like it
 
Basikeli 1 ya swala,redio 1mbao ya national,jembe la mkono,panga,mashati mawili ya bahama,la kuchumpa,jinsi pensi,jumla 35000tsh.
 
watanzania huwa tunashabikia sana viongozi kutangaza mali zao sasa ili kuonyesha ni jambo jema na sisi wanajamvi tutangaze zetu, tuwe wakweli.
Naanza: Mi nnamiliki kalaptopu ya laki nane, redio ya laki tatu, feni ya elfu hamsini ,shelfu la vitabu kama hamsini nilinunua ubungo bukubuku na kwenye akaunti nina laki nane.

kwa ujumla ninamiliki mali za kama milioni mbili.

haya wanajamvi tiririkeni!

:decision::thinking::crazy:Mie nina miliki ka flash ka 2GB, ka moderm ka vodafone kalikochakachuliwa, line ya Zantel,Tigo, airtel na voda zote zikiwa na airtime ya bukubuku,ka simu ka Mchina aina ya pro tech,Radio ya KICHBO, ka screen ka inch 6 black and white baiskeli aina ya SWALA niliachiwa urithi na Mdingi pamoja na kakiwanja ka 20m x 10m actualy nikipata kaloan ka 80,000/= nilikoomba bay port nitaanza kujenga kagheto ka Room moja na Sebule, na nina ka akaunt ka mshahara ambako sikumbuki kama huwa kana zaidi ya buku tano kila mwisho wa mwezi, kwa ujumla mali zote zinaweza ku amount kama laki 2 unusu:thinking::thinking:
 
Vyote alivyokuwa navyo malima ni cha mtoto kwangu ninavyo ivyo mara 10 yake...Ila nina mabangaloo 6 pale masaki,alafu bughart 2 za mil.500,elikopta 3 mojawapo nilimuazimisha Slaa wakati wa uchaguzi na Jk mwaka juzi..Source urithi,magendo,madawa...Jamaa hata mkinishtaki serikali yote iko pale kwasababu mimi nipo.
 
Viatu:yebo yebo pea tatu nguo:kaunda suti pea mbili......kitanda cha kamba ingawa silalii kwani nalala chini sakafuni kwa kipande cha ngozi ya mbuzi majengo mawili ya ghorofa maeneo ya makete na kanyumba katofali za kuchoma kwetu matema bus mbili za kwenda mkoani.....hiace town kwa ajiri ya kusambaza mizigo kwenye maduka yangu mtaa wa congo.....hektari 50 za mashamba ya mbao mafinga na miliki misukule 6.....mali nyingine nitazitaja kesho nikienda kumuuliza babu njombe.
 
Namiliki jet fughter 2kwa ajili ya ulinzi hivi niliziteka kwa majeshi ya marehemu ghadafi kipindi wanamsaidia idd amin dada, vifaru 9 vinavyorusha mabomu ya masafa marefu (misile) hivi nimezawadiwa na jeshi la wananchi baada ya kustaafu jeshi, smg 1 hii nimeuziwa jana lakini nahisi itakuwa ya huyu waziri wetu aliyochopwa juzi pale mji kasoro bahari, zingine sitawatajia kwa sababu ni confidential mfano siwezi kukuambia nina wake wangapi, unashangaa! mke naye ni mali kama ulitoa mahari
 
Tunamsubiri yule anayemiliki Lake Oil na bangaloo pale kijijini msoga Chalinze ataje maali zake...
 
Namiliki bar ya pombe kali grocery ya mataputapu na kiwanda cha gongo,..Nami nafanya kazi tbl ninaishi guest house.Ni hayo tu.
 
Naishi kijijini kabisa :
> Namiliki shamba la ekari 50,niliuziwa na kijiji tsh 5m. Ekari 40 nimelima miti. Ekari 10 nimekodisha wakulima wa bhangi.
> viwanja 3 nimeuziwa na kijiji kwa tsh laki 3. Sijajenga naishi kwenye mjengo wa serikali.
> fenicha zangu zote zina thamani ya tsh 2m.
> simu aina nokia 6batani elfu 20 na nokia E61i ya tsh laki 5. Sina laptop na sijawahi kutumia kompyuta.
> mtambo wa umeme jua na standby generata 3 vyote tsh 3.5m.
>tv 3,subwoofers3, radio 3,receiver 1,satellite dishies 2 vyote tsh 1.7m.
> mke mmoja,superwhite,superbeauty,mzigua mwenye shahada ya uuguzi (MUCHS),anapiga mzigo Milembe. Nimemuoa kwa tsh elfu 40 mwaka 2008 bado nadaiwa elfu 20.
> kabinti ka miaka 2 nimezaa nje ya ndoa. Haka kakisoma na kukua nitakapiga bei kwa n'gombe 10 tu (tsh 5m ya sasa).
> baiskeli 15 nakodisha,thaman tsh 1.5m.
> mabegi 3 ya nguo za mitumba na za kushonesha na dukani,thamani tsh laki 4. Viatu vya kawaida pairs 5, yebo pairs 2,gumbuti pairs 2, vyote laki 1.
> benki sijui nina shs ngapi,ATM kadi anakaa nayo waifu.
KIFUPI NAMILIKI MALI ZENYE THAMANI YA TSHS MILLIONS 20.
PATO LANGU KWA MWAKA TSH 24 millions.
VYANZO VYA MAPATO,MSHAHARA WANGU + VITEGA UCHUMI.
... Acheni kiher*her* CAG aliishahakiki.
 
aisee ukitaka usikosee hesabu ya waifu chukua ( mahari +amaunti uliyotumia kwake+huduma ulizo mpa - huduma alizokupa=wife value). dawa ya sikio nasikia siyo fresh kumalizia mahari kwa wakwe! ntalipeleka kwenye mahusiano nisikie wenye ma experience wanasemaje.
 
aisee ukitaka usikosee hesabu ya waifu chukua ( mahari +amaunti uliyotumia kwake+huduma ulizo mpa - huduma alizokupa=wife value). dawa ya sikio nasikia siyo fresh kumalizia mahari kwa wakwe! ntalipeleka kwenye mahusiano nisikie wenye ma experience wanasemaje.
***

Hilo la hesabu za waifu inabidi nichukue muda wa kutosha. Nitatoa value yake thereafter.
Suala la mahari,wakwe walipanga elfu 60,nilitaka kulipa yote,wakaniambia kwa mila ya kwao MAHARI HUWA HAILIPWI YOTE. NI UDHALILISHAJI KWA MKE NA WAKWE.NIKALIPA ELFU 40.
Hebu Mkuu lipeleke hili MMU tusikie wanasemaje.
 
Magunia 8 ya mahindi, debe 21 za nyanya ila zinaweza kuharibika sio muda mrefu kwa kukosa soko,Kuku kama 100 wanaweza wakafa wote muda si mrefu kwa kuwa wanakideri,Maharage gunia 4 ila yamegongwa sana muda si mrefu ninawza nikayatupa,Alizeti gunia 9 ila panya wananisumbua sana wanaweza wakanibakizia 2 mpka mwezi ujao kwangu ndo mali zangu mkuu

Yaan kaka umenichekesha mpaka tumbo linaniuma. Nimeipenda sna hi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom