Wadau nani basi anayeaminika tena kushika hatamu ya uongozi wa Tanzania?

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
3,142
5,634
Wadau nimekuwa na matumaini makubwa sana na vyama vya upinzani haswa CHADEMA kwa muda mrefu nikiamini huyu ndiye mkombozi ajaye kwa wananchi wa Tanzania. Katika siku za hivi karibuni zimeibuka kashfa za rushwa katika kamati za Bunge, na mbaya zaidi kinachonisikitisha hata wale tunaowaamini sana wa upinzani kumbe nao wamo. Je, kama makucha wameanza kuyatoa mapema namna hii hata kabla ya kushika hatamu kuongoza nchi, wakishikilia nchi itakuwaje?

Ni nani wakumwamini tena basi? Au ndo ule msemo wa "HERI ZIMWI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKWISHA KULIKO ZIMWI LISILOKUJUA" unaanza kujidhihirisha?

Kwa kweli Mbunge yeyote yule wa upinzani aliyekubali kupokea rushwa mmetuangusha mno, hatukutegemea hayo kutoka kwenu.
 
Back
Top Bottom