Wadau mmesikia haya ya Zanzibar... CUF imepigwa chenga ama ?


Lakini Shamhuna, ambaye pia ni Waziri wa Habari wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ), alisema Zanzibar haihitaji Serikali ya Mseto wala Serikali ya Umoja wa Kitaifa, bali kinachotakiwa ni kujenga utamaduni wa kukubali matokeo ya uchaguzi ya kushinda na kushindwa.

Shamhuna kamaliza kazi. Hivi Seif kwanini ameogopa uchaguzi mapema hivyo?? Nadhani alijua tiyari kisha shindwa wacha aombe vyeo vya bure.
 
Nd. Masatu,
Tafadhali zihurumie mbavu zetu!!!
Hayo aliyoyasema Shamhuna ndio msimamo wa SMZ na yale ya Karume ilikuwa babaisha ***** tu! Kwa kweli inatia uchungu, Maalim Seif baada ya miaka zaidi ya 10 ndio sasa anajua maslahi ya Wa-zanzibari? Sasa zogo lote lile lilikuwa la nini? Kwa mimi Seif ndio awe wa mwanzo kupandishwa mahakamani kwa kuwarejesha nyuma Wa-zanzibari kwa ugomvi ambao kumbe sio wa kweli.
Mh!!! Ngida1. Nafikiri una point hapo ya kueleza. Hebu fafanua . Unajua sisi wengine si watu wa Zenj, lakini tuna shauku ya kuyajua yale ya ndani ya huko.
 
Uzuri wa Shamhuna huwa ni mkweli na haumi maneno! Karume anapodai kuwa suala la serikali ya mseto anawaachia Wazanzibari wenyewe ni kuuma maneno bila kuelezea ukweli wa mambo! Seif na Libumba mmeliwa mchana kweupeee!
-Shamhuna anaongea nadharia tu kama vile Mhadhiri anayetaka kuwababaisha wanafunzi wake tena wale Undergraduates walio katika mwaka wao wa kwanza.
 
Maalim na Profesa wametugeuka lakini mwisho wao hauko mbali. Yote ambayo tumekuwa tunayapigania hakuna hata moja lililotekelezwa na SMZ hivo kitendo chao cha kujikomba kwa SMZ ni usaliti wa hali ya juu. Mlioko bara mwachekelea kwani hilo ndo mlilotaka lakini CUF twasema hatutokata tamaa mpaka kieleweke hiyo ndoa ya mkeka haitadumu!
 
Kwani Karume akiamua Shamhuna ataweza kupinga? Na ndio maana kikao chao kikawa cha siri ili watu kama kina shamhuna wasivuruge mambo na kama kuna mambo ya serikali ya umoja atashangaa hivyo hivyo. Ujue serikali ya mseto ikija baadhi ya mawaziri wa sasa watapoteza kazi kwa hiyo hawataki kusikia hicho.

Binafsi naona kuheshimiana na kutendeana haki bila kujali idiology ya mzanzibar ndicho muhimu zaidi kuliko hiyo serikali ya mseto.
 
Shamhuna kamaliza kazi. Hivi Seif kwanini ameogopa uchaguzi mapema hivyo?? Nadhani alijua tiyari kisha shindwa wacha aombe vyeo vya bure.

Seif alichofanya ni kutafuta fair play kwenye uchaguzi ujao na sio serikali ya mseto kama wengi mnavyofikiri. Unajua Pemba na Unguja wakielewana hata huo muungano wa bara hauhitajiki. Na hilo Karume na Seif wameliona na wamechoka na malumbano yasiyojenga nchi. Kwa hiyo usishangae Karume akakubali kuiachia CUF washinde uraisi mwakani japo ccm hawatapendezwa na hilo.
 
Naona watu wote munapiga kelele tuu, wengine kuonesha kuwa wao wanaogopa wazanzibari wasiungane kwa kulinda muungano...n.k

Jambo la msingi ambalo hapa limekosekana ni NIDHAMU, Shamhuna na Khatibu na Sophia ni watovu wa nidhamu.Hawa hawastahiki kutoa maoni ambayo yanapingana na kiongozi wa nchi (regardless of Pindas perspective ofcoz).

Serekali na vyama vina utaratibu wao wa kutoa msimamo, sio tuu huyu kasema vile ...nahisi kama Karume angelimchukulia hatua za nidhamu huyu Shamhuna kwa kutoa kauli zinazokwenda kinyume na uongozi wake.Otherwise wanatunganya wananchi!
 
kwani shamhuna ni nani hata mumpe sifa zote hizo ungekuwa unamjua shamhuna wala usingesema kitu huyu jamaa ni msaka tonge tu na mpenda ulwa wewe huoni hata katika kamati kuu hayumo amekataliwa kwao kwenye jimbo lake amashindwa kaikosa nafasi na sasa ataikosa tena nafasi hiyo ya uakilishi shamhuna hana tofauti na huyo asha ngedere na alipokuwa hana uaziri alikuwa analia tu lakini mambo ni kangaja huwenda yakaja mtakuja ona haya
 
Back
Top Bottom