Wadau: Dowans imechimbia kaburi CCM

Cha kupendaza kwenye habari hizo hapo juu ni kwamba kuna a lot of substance kwenye hotuba za hao jamaa na si propaganda kama za Tambwe Hiza. Jamaa wanazungumzia issues za kitaifa na sio ku-victimize raia at large at the expense ya wachache!
 
kumbe chriss mtikila yupo?

ila kwa hili amechemka sana...hawa vijana wa ccm baba zao ndo wale wale wanamilki dowans
 
He is begining to join them. Kwa jinsi walivyolewa madaraka, sitarajii kama kuna mwanasisiem anayeweza kuongea jambo la maana. Itakuwa ni maajabu ya dunia.
 
Kinachoanza kusikika sasa hivi ni kwamba CCM wamesha hakikishiwa mgao wao kutokana na malipo hayo.

Nchi haina uongozi. Inaongozwa na cartel. Ni mipango ya uovu ndo inaoongoza nchi. Maana kumbe hata halmashauri za miji na manispaa ni mifereji ya kupitishia pesa za chama. Ndo maana imewapa taabu sana kuachia majiji kama Mwanza na Arusha.
 
Hivi nyie Mnajua Mabango yaliyosambazwa Nchi nzima kipindi cha campaign yalikigharimu chama Bilioni Ngapi?
 
Kwani wana maslahi yao katika hayo madai ya wazee au ya walimu mnayosema??

Kwanza kura zao haziwatishi....za kuchakachua zinaweza kuziba kura zao so hawana haja ya kutishika nao.....
 
Hoja ya kutokuwa na imani na serikali yasukwa
*Utabiri wa CCM kufuata nyayo za Kanu watolewa
*Vijana CCM waendelea kuasi K'njaro na Moro
Kuna kila dalili kuwa suala la fidia ya Sh. bilioni 94 kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans ambayo ilishinda kesi dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC), litailipua nchi hasa baada ya chama tawala kuafiki uamuzi huo.

Mlipuko huo umeongezewa nguvu na uamuzi uliopitishwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wiki iliyopita kuwa fidia hiyo ni lazima ilipwe kwa kuwa mkataba wa Tanesco na Dowans ulivunjwa kinyume cha sheria.

Kutokana na tamko hilo, kundi la wabunge wa upinzani ambao si sehemu ya upinzani rasmi, limeibuka na kuazimia kwamba sasa wanakusudia kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Serikali kama kweli fedha hizo zitalipwa.

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, alisema kwamba ataliomba Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na Serikali iwapo kampuni hiyo italipwa fedha hizo kabla ya Mkutano ujao wa Bunge, unaotarajiwa kuanza Februari 8, mwaka huu.

Alitaka hoja ya Dowans iruhusiwe kwenda bungeni kabla malipo hayo hayajafanyika ili wabunge wakaihoji Serikali juu ya suala hilo.

Kafulila akitoa msimamo huo huku akiungwa mkono na wenzake. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho kinaunda upinzani rasmi bungeni tayari kimetahadharisha juu ya fidia hiyo, huku Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, akiwa amekwisha kuuibebesha serikali na CCM mzigo wa fidia hiyo kutokana na uzembe.

Akiwasha moto huu mpya, Kafulila alisema anataka Serikali iwaeleze Watanzania imekuwaje hadi kulazimishwa kuilipa kampuni ambayo mkataba wake una utata.

Kafulila, ambaye pia ni Katibu wa kamati ya kambi isiyo rasmi ya upinzani bungeni, alitoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa habari, ulioitishwa na kamati hiyo, katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, pamoja na Mbunge wa Mkanyageni (CUF), ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Teule ya Bunge la Tisa iliyochunguza mchakato wa zabuni iliyoipa ushindi Kampuni ya Richmond Development LLC, Mohammed Habib Mnyaa, waliunga mkono kauli ya Kafulila.

Uamuzi wa serikali wa kuilipa Dowans fedha hizo, ulitangazwa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Januari 6, mwaka huu akisema imekubaliana na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) iliyoliamuru Tanesco kuilipa kampuni hiyo Sh. Bilioni 94.

Kafulila alisema amefikia hatua hiyo kwa vile uamuzi wa kuilipa Dowans ni mbaya na kwamba, endapo Serikali itautekeleza itakuwa inajitia kitanzi.

Alisema Desemba 10, mwaka jana aliwasilisha ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam barua ya kusudio la kutaka kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhoji kwanini Serikali isiwajibike kwa kuliingiza taifa hasara kwenye sekta ya umeme.

Pia, kuliomba Bunge kuazimia kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini kwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa sera ya nishati na madini na mpango kabambe wa usambazaji umeme na hivyo kusimamia migawo mitatu ya umeme ndani ya miaka miwili ya uongozi wake.

Hata hivyo, alisema Desemba 14, mwaka huo, barua hiyo ilijibiwa kwa kuelezwa kwamba, maombi yake yanafanyiwa kazi.

Alisema wakati akisubiri kufanyiwa kazi maombi ya barua yake, Waziri wa Ngeleja akalitangazia taifa kuhusu uamuzi wa serikali wa kukubali kuilipa Dowans.


CCM ITAFUATA KANU
Kafulila alisema ubaya wa kuilipa Dowans, unatokana na kashfa ya kampuni hiyo kufanana na ile iliyoikumba Serikali ya Kenya, ya Goldenberg, ambayo ilipata kuuangusha utawala wa serikali ya nchi hiyo iliyokuwa chini ya Kanu mwaka 2007.

Kashfa ya Goldenberg ilijitokeza katika miaka ya 1990 wakati wa utawala wa Rais Mstaafu wa Kenya, Daniel arap Moi, ambayo ilisababisha serikali kupoteza dola milioni 600 kwa njia ya biashara ya kughushi ya kusafirisha almasi na dhahabu nje ya nchi.

“Kashfa ya Goldenburg, iliangusha utawala wa Kanu na kusababisha (Rais wa sasa wa Kenya, Mwai) Kibaki, aingie madarakani kupitia chama cha NARC. Sasa serikali ya Tanzania ikicheza na Dowans/Richmond mpaka 2015 wajue historia ya Kanu itatimia kwao,” alionya Kafulila.

Aliongeza kuwa: " Ni miaka tisa tu, 1993-2002 Goldenberg ikaondoa Kanu Kenya, 2006-2015 Dowans/Richmond itaondoa CCM Tanzania. Kwa hiyo miaka tisa (1993-2002) ya Goldenberg iliangusha Kanu mwaka 2002. Na miaka tisa (2006-2015) itaangusha utawala wa CCM uchaguzi wa 2015.”

Kafulila alisema ushahidi mwingine wa ubaya wa uamuzi wa kuilipa Dowans, ni namna ilivyozua mtafaruku hadi ndani ya serikali yenyewe, ambako mawaziri wa serikali moja wamekuwa wakitoa matamshi ya kupingana.

Alisema mbali na hayo, uamuzi wa kuilipa Dowans, unaipunguzia serikali uhalali wake wa kisiasa, ambapo inakuwa vigumu kuwahamasisha watu kuisikiliza, kuiamini na kuiunga mkono.

Alisema pia, kashfa ya Dowans, hadi sasa ukweli wake haujulikani, umefichwa.

"CCM wameshaiba na kufanya ufisadi mkubwa. Wizi huu wa Dowans hauna muafaka. Unakwenda kuiondoa CCM madarakani,” alisema Kafulila.

Aliitaka serikali kutocheza na Dowans, badala yake akataka suala hilo lifikishwe bungeni ili serikali ikalitolee ufafanuzi kwa kueleza kwanini ilishindwa kesi iliyofunguliwa na kampuni hiyo na kuwafikisha Watanzania hapa walipo.

"Hoja ya Dowans iruhusiwe, iende bungeni kabla malipo hayajafanyika. Huko ndiko ambako tutaulizana tumefikishanaje hapa? Wakilipa kabla haijapelekwa bungeni, hoja itapanuka.

Sasa sitaliomba Bunge kama nilivyokusudia awali limwajibishe Waziri wa Nishati na Madini tu, bali nitaliomba liazimie kutokuwa na imani na serikali yote. Kwa sababu hakuna haraka ya kulipa 'fasta fasta'," ” alisema na kuongeza kuwa:

"Watu wengi wanahitaji sheria, lakini mbona ilishafikia hadi walimu wanavua nguo katika kudai haki zao? Wazee wetu wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki karibu miaka 20 wanadai haki zao hadi wanalala barabarani.

Mbona haraka ya kuwalipa haikuwapo? Hivyo, nitamwomba Mheshimiwa Spika, hili jambo (la Dowans) lifikishwe mwisho na kuwawajibisha wote waliohusika."

Hamad Rashid Mohamed akiunga mkono kauli ya Kafulila, alisema wanataka hoja ya Dowans ipelekwe bungeni ili ifikie tamati.

Alisema hata mtu aliyefungwa gerezani, hukumu yake inaweza kurudishwa mahakamani ikapitiwa upya.

" Hata kama ni wabunge ndio walioamua kuhusu Richmond/Dowans nao ni binadamu vilevile," alisema Hamad akitilia msisitizo wa kutaka hoja ya Dowans ipelekwe bungeni kujadiliwa.

Alisema kwa sasa kanuni za Bunge haziruhusu suala lililokwishaamuliwa na Bunge kujadiliwa upya, lakini akasema kanuni ya 150 ya Bunge inawaruhusu wabunge kutengua kanuni hiyo iwapo jambo linalotaka kujadiliwa ni kwa maslahi ya taifa.

Naye Mnyaa, alisema wabunge wako tayari kuijadili upya hoja ya Richmond/Dowans iwapo itaruhusiwa kurejeshwa bungeni na kwamba, hilo haliwapi hofu yoyote.


SITTA, MWAKYEMBE NI MASHUJAA
Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameunga mkono tamko la Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM), kwa ujasiri na uzalendo wao wa kupinga Kampuni ya Dowans kulipwa Sh. bilioni 94 ambazo ni jasho la Watanzania wote.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam, Mtikila alisema kitendo cha UVCCM, kutoa tamko lenye uzalendo inadhihirisha kwamba wao ni daraja muhimu la kuunganisha na wananchi katika vita ya ukombozi wa nchi.

"Naunga mkono tamko la UVCCM la kupinga Dowans kulipwa mabilioni hayo ambayo awali zilitakiwa kukombwa Sh. bilioni 186, lakini baada ya wazalendo kupiga mayowe dhidi ya majambazi, hesabu ikapungua na kuwa Sh. bilioni 94," alisema Mchungaji Mtikila na kuongeza kuwa:

"Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ni viongozi pekee wanaotetea maslahi ya nchi dhidi ya majambazi wanaotegemea jasho la walalahoi."

Alisema Watanzania wakisimama kwa pamoja kuhusu Dowans haitatolewa hata senti moja na kwamba anaungana na wote wenye mawazo kama yaliyotolewa na UVCCM.


VIJANA MORO NAO WALIPUKA
UVCCM Morogoro wameunga mkono tamko la kamati ya utekelezaji Umoja huo taifa uliotolewa wiki iliyopita kuhusu sakata la Dowans kurejeshwa bungeni na kujadiliwa upya.

Umoja huo umeitaka Serikali na uongozi wa taifa wa CCM kuchukua hatua za haraka za kuwaweka kando baadhi ya mawaziri wanaopingana na misimamo ya Serikali kuhusiana na sakata hilobila kufuata taratibu.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wake, Jonas Nkya baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utekelezaji kilichoshirikisha pia viongozi wa matawi ya umoja huo kutoka vyuo vikuu.

" Tunaomba chama chetu kuwachukulia hatua haraka ili kuwaweka kando watu hao ili kukinusuru chama na serikali, lazima kuwe na msemaji mmoja. Iweje leo maelekezo na misimamo yake ipingane," alisema Nkya.

Aliiomba Serikali na CCM kutoa msimamo wa msemaji kwenye masuala nyeti na muhimu ili kutowapa nafasi viongozi waropokaji na wanaokurupuka.

Akitoa msimamo wa UVCCM kuhusu Dowans, Mjumbe wa Baraza hilo kutoka Chuo cha Ualimu (Motco), Said Sambala, alitaka Serikali itafakari kwa umakini kuhusu Dowans kwa kuwa linawagusa wananchi.

" Tunataka hoja ya Dowans irudishwe bungeni ili wahusika wajulikane na kama wapo walioishauri Serikali na wale wote wenye makosa wachukuliwe hatua za kisheria,” alisema Sambala.


KILIMANJARO NAKO MOTO
Nao UVCCM mkoani Kilimanjaro umeunga mkono tamko la Kamati ya Utekelezaji la Umoja huo Taifa na kueleza kuwa mabishano ya baadhi ya mawaziri hadharani juu ya Dowans kulipwa kulipwa fedha hizo kuwa ni ishara mbaya kwa Taifa.

Mwenyekiti wake, Godliving Moshi,alisema mabishano hayo yanahitaji utatuzi wa haraka kwani ni aibu kwa mawaziri kubishana hadharani wakati kauli zaozinapaswa kuwa moja.

Alisema sakata hilo limesababisha mawaziri kuwa na kauli tofauti, jambo ambalo alisema linashangaza na kutoa mfano mbaya.

Wiki iliyopita, Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM pamoja na mambo mengine, ilipinga mpango wa serikali kuilipa Dowans kiasi hicho cha fedha kama hukumu ya ICC ilivyoagiza.

Baraza hilo lilitoa tamko kwamba hoja hiyo irudishwe bungeni ili wananchi wajue ni nani aliyeifikisha hapo ilipo.




CHANZO: NIPASHE
 
Dowans yaiweka CCM njia panda Sunday, 23 January 2011 21:03

Na Waandishi Wetu
Mwananchi

MOTO wa malipo kwa Kampuni ya Dowans umezidi kusambaa baada ya Kambi ndogo ya Upinzani bungeni kuonya, kama Serikali ya CCM ikilipa fedha hizo ijiandae kujiuzulu huku Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, akisema tatizo jambo hilo halikupita kwenye Baraza la Mawaziri. Kambi hiyo ndogo ya upinzani ikitoa tamko ikifananisha Dowans na kashfa ya Goldenberg iliyochangia kuangusha Serikali ya KANU, Kenya, mwenyekiti wa DP Mchungaji Christopher Mtikila, ameibuka na kutoa tamko la kuitisha maandamano nchi nzima kupinga kile alichokiita, "Uporaji wa Nchi kwa Kutumia Bastola ya Dowans.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Sumaye ambaye hii ni mara yake ya kwanza kugusia sakata hilo, alisema tatizo lililopo ni Dowans haijapitia katika baraza la mawaziri na endapo lingeenda katika baraza hilo yasingetokea matatizo hayo.

"Tatizo la Dowans halijaenda kwenye cabinet, (Baraza la Mawaziri), lingeenda kwenye cabinet, nadhani lisingekuwa hivyo," alisema Sumaye.

Sumaye alitoa kauli hiyo nje ya Ukumbi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Lugalo ambako alikaribishwa kwenye tafrija ya kuukaribisha mwaka wa 2011 iliyoandaliwa na Umoja wa Maendeleo ya Wakazi wa Wilaya ya Mbulu, Karatu, Babati na Hanang (NORIVADA) waishio Dar es Salaam.

Hata hivyo, Sumaye ambaye hakutaka kabisa kuzungumzia suala la Dowans wala katiba mpya alijikuta akizungumza suala hilo kwa kifupi baada ya waandishi kumbana wakitaka kusikia msimamo wake. Kauli hiyo ya Sumaye iliwahi kutolewa pia na Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta, akihoji kutangazwa uamuzi huo bila kupita kwenye ngazi ya Baraza la Mawaziri.

Huku Sumaye akigusia kwa kifupi, kambi hiyo ndogo ya upinzani imetoa tamko katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam jana, ambalo Katibu wake David Kafulila, alisema kitendo cha Serikali kutaka kuilipa Dowans kabla suala hilo halijafikishwa bungeni ni sawa na kuchezea moto.

“Chimbuko la Dowans liliangusha Serikali madarakani, hivyo Serikali inatakiwa kutoa nafasi kwa sakata hili kwenda bungeni ili ieleze iweje kampuni ‘batili’ ilipwe kiasi hiki cha fedha,” alifafanua Kafulila, hatua ambayo itaiweka Serikali ya CCM katika ncha ya kisu.

Katibu huyo wa kambi hiyo ndogo, alifafanua kwamba ndani ya Serikali kila kiongozi ana mtazamo wake kuhusu malipo ya Dowans na kusisitiza, suala hilo linatakiwa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa.

“Sakata la Dowans Tanzania ni sawa na ‘Goldenberg scandal’ iliyoangusha utawala wa chama cha Kanu nchini Kenya, kashfa hii ilianza mwaka 1993 na kumalizika 2002, Richmond na Dowans ilidumu tangu 2006 hadi sasa hakuna majibu,”alisema Kafulila Kafulila ambaye amewasilisha kusudio lake la kutaka kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhoji sababu zinazoifanya Serikali isiwajibike kwa kuliingizia taifa hasara ya mabilioni ya fedha kwenye sekta ya nishati, alisema Serikali ikipuuza suala la Dowans itapunguza uhalali wake wa kisiasa.

“Pamoja na kuwa kambi hii si rasmi, lakini hatuwezi kukaa kimya katika mambo ya msingi, Dowans ni suala ambalo haliwezi kuzimwa hivi hivi tu wakati ukweli haujajulikana, na kwambia CCM itang’oka madarakani sababu ya Dowans kama ikifanya mchezo, historia ya Kanu itawahukumu,” alisema Kafulila. Aliongeza kwamba, kama CCM hakitang'oka madarakani basi kuna uwezekano nchi ikakumbwa na machafuko.

“Dowans isilipwe mpaka sakata hili lifike bungeni na kupitishwa katika mkaa wa moto wa wabunge, wakilipuuza hili la malipo ya Sh94 bilioni basi wanaweza kupuuza hata malipo feki ya Sh100 bilioni,” alisema Kafulila.

Alifafanua, Dowans ikilipwa kabla ya kujadiliwa bungeni maana yake ni kwamba suala hilo litapanuka na kuongeza kuwa ikiwa hivyo, atawaomba wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na Serikali.

“Hivi hii nguvu na mbio kubwa za kuilipa Dowans zimetoka wapi, mbona malipo ya wastaafu wa EAC na walimu hayapewi kipaumbele, mimi hoja yangu imelenga zaidi hukumu ya ICC kuhusu kulipa Dowans kiasi hiki cha fedha,”alisisitiza Kafulila.

Alipoulizwa kwamba haoni kurudisha sakata la Dowans bungeni linaweza kuibua mengine kuhusu sakata la Richmond ambalo lilisababisha mawaziri kujiuzulu, Kafulila alisema; ...ninachokwenda kuhoji bungeni ni suala la hukumu ya ICC kuilipa Dowans, nataka maelezo katika hilo, najua kuna ambayo hayakusemwa katika ripoti ya Richmond iliyotolewa bungeni na ile kamati ya akina Mwakyembe, inawezekana yakaamka tena, hilo sijui, lakini likiwa hivyo atakayevuliwa nguo chafu na kuvalishwa safi ataonekana.”

Naye Hamad Rashid wakati akizungumzia mwelekeo wa bunge la kumi, alisema kuhusu vurugu zilizotokea Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu, Serikali inatakiwa kuboresha mawasiliano kati yake na wananchi ili kuepuka kutokea tukio jingine kama hilo.

“CUF waliwahi kuzuiwa kuandamana, ila taarifa zilikuja usiku, sasa hapo unaweza kuwazuia watu wasiandamane kesho yake, “alihoji Rashid. Akizungumzia uwajibikaji, alisema umefikia wakati wa viongozi wa Serikali kuwajibika na kuongeza kuwa kitendo cha viongozi hao kutowajibika ndio kunakofanya nchi isitulie.

“Kuhusu ushirikiano tumemuandikia Mbowe (Freeman Mbowe) barua Januari 21 mwaka huu kwa kuwa tuliwahi kumweleza kuwa tuko tayari kushirikiana nao ambapo alitujibu kuwa hawezi kuamua suala hilo pekee mpaka maamuzi ya vikao vya chama chake,”alisema Hamad.


Aliongeza, “Tumempa muda wa kutosha na vikao vya chama chake vimeshakaa na kwa kuwa tunaelekea katika vikao vya kumi vya bunge vinaanza Februari 8, tumemtaka atueleze kama jambo la kushirikiana kati yetu na wao litawezekana na hatimaye tufanye kazi kwa pamoja tukiamini kuwa umoja ni agenda ya umma,”alisema Hamad.

Kuhusu mtizamo wa kamati hiyo kuhusu katiba, Hamad alisema umefikia wakati wa Watanzania kuwa na katiba yao ambao wameshiriki kuitunga. “Watanzania waulizwe wanataka mfumo gani wa Serikali, mfumo lazima uwekwe na wananchi kwa kuwa hata tukiwa na rais mwizi basi ashindwe kuiba kwa kuwa atabanwa na mfumo uliopo,”alisema Hamad.

Mtikila aishangaa CC kutaka Dowans ilipwe Kwa upande wake Mtikila alisema, "hii si siasa. Kama CCM ingekuwa inazungumzia kulipa pesa zake tungeruhusu wakae kwenye Nec au CC na kuvaa nguo zao za kijani, lakini hizi ni pesa za umma." Mtikila alisema kulipa fedha hizo ni kuhujumu nchi. Kiongozi huyo ambaye pia huongoza Kanisa la Uokovu Kamili, alisema katika kuonyesha hasira za umma, chama chake kwa kushirikiana na wanaharakati, vyama vingine vya siasa, viongozi wa dini zote kitafanya mandamano makubwa kupinga malipo hayo.

"Hili halitakuwa jambo la kusubiri hata hukumu..., moto huu utawaka wakati wowote. Namtahadharisha Jakaya Kikwete (Rais), asichezee kabisa na moto huu mimi mwenyewe ambaye sifi kwa risasi nitakuwa mbele," alionya Mtikila ambaye ameibuka baada ya kimya cha muda mrefu.

Alifafanua kwamba, pesa hizo za kuilipa Dowans zilitajwa ni Sh 186 bilioni na kuongeza, "Lakini baada ya mayowe dhidi ya majambazi hesabu ikapungua na kuwa sh 94 bilioni." Mwanasiasa huyo mwenye historia ya misukosuko ya kutumikia kifungo jela na anayeoongoza kwa kufungua kesi nyingi mahakamani, aliwataka wananchi kutumia Ibara za 27 na 28 za Katiba na kusisitiza, " hata senti moja hatutaporwa na jambazi lolote."

Aliongeza kwamba, Ibara ya 27 (2) inataka raia wazalendo kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndiyo waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa na kuhoji, "Taifa linauziwa bidhaa gani na Dowans kwa mabilioni ya fedha zetu hizi adimu?" Kwa msisitizo alisema, "Maandalizi ya kile tulicho nacho ni uboreshaji wa maisha yetu sisi sote milioni 44.

Maandalizi ya watoto wetu wote kwa maisha yao ya baadaye, ujenzi wa miundombinu na misingi imara ya uchumi wetu n.k." Akizungumzia msimamo wa Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi Dk Harrison Mwakyembe, kupinga malipo hayo, Mtikla aliwaunga mkono akisema wako sahihi.

Tangu kutangazwa uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC Court) hapo Novemba mwaka jana ukiagiza Tanesco kuilipa Dowans, taifa limeingia kwenye mjadala mzito huku baraza la mawaziri nalo likigawanyika. Habari hii imeandkwa na Ramadhan Semtawa na Fidelis Butahe na Felix Mwagara
 
Halipwi mtu hapa mpaka kieleweke. Tumechoka nchi yetu kufanywa shamba la bibi kila kukicha.
 
"Hili halitakuwa jambo la kusubiri hata hukumu..., moto huu utawaka wakati wowote. Namtahadharisha Jakaya Kikwete (Rais), asichezee kabisa na moto huu mimi mwenyewe ambaye sifi kwa risasi nitakuwa mbele," alionya Mtikila ambaye ameibuka baada ya kimya cha muda mrefu.

Mtikila kiboko aiseee!
 
Kutokana na tamko hilo, kundi la wabunge wa upinzani ambao si sehemu ya upinzani rasmi, limeibuka na kuazimia kwamba sasa wanakusudia kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Serikali kama kweli fedha hizo zitalipwa.
Khaaa! Inatakiwa hii hoja iende walipwe wasilipwe. Huyu JMK nchi imeshamshinda wamwondoe tuu
 
Hii hoja inapswa iende bungeni whether they like it or not otherwise kutofikishwa kwa hoja hii Bungeni kutaendeleza mpasuko mkubwa ambao tayari umeishaanza kuonekana
 
Back
Top Bottom