Wadaiwa kujaza maji kwenye chupa na kuyauza kwa abiria

ishuguy

Member
Nov 3, 2007
76
10
SERIKALI ya Mji Mdogo wa Same mkoani Kilinajaro imebaini baadhi ya wafanyabiashara wadogo katika kituo cha mabasi cha Same mjini, wanaouza maji ya kunywa abiria ambayo, hayana viwango vinavyotakiwa na Shirika la Viwango nchini (TBS).

Watendaji wa mji huo, walisema kuwa baada ya kufanya utafiti wamebaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu, wamekuwa wakifanya biashara hiyo chafu na waliwatahadharisha wananchi kuwa makini kabla ya kunywa maji hayo.

Maji hayo, licha ya kuhofiwa kutoandaliwa kwa kuzingatia kanuni za afya, yalikuwa yamewekwa kwenye chupa zenye nembo bandia za makampuni mbalimbali yanayozalisha maji ya kunywa.

Miongoni mwa chupa za maji zilizojazwa maji ambayo yanahofiwa kutokuwa salama ni chupa zenye nembo ya Kilimanjaro, Iceberg na Uhai na abiria wa waliokuwa wakisafiri kuelekea vijijini wilayani humo na yanayosafiri safari ndefu nje ya wilaya hiyo .

Wafanyabiashara hao wasiowaaminifu wanasadikiwa kukusanya chupa zilizotumika na kuweka maji ya bomba na kuwauzia watu mbalimbali, wakiwemo abiria.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia jana maafisa watendaji wa Mamlaka ya Mji huo wakiwa na askari katika kituo hicho cha mabasi kuwathibiti wafanyabiashara waliokuwa wanakwepa kulipa ushuru na kodi mbalimbali za serikali na kwamba wakati wakiendelea na shughuli hiyo,walitia shaka wafanyabiashara waliokuwa wakiuza maji.

Mtendaji Kata ya Same, Destina Azaliwa alisema Kampeni ya kudhibiti wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi una lengo la kuongeza mapato ya serikali wakati udhibiti wa usafi una lengo la kudhibiti magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.

Aliwataka abiria na watumiaji wa maji ya kunywa wakiwa safarini, kuwa makini dhidi ya wafanyabiashara wadanganyifu ili kuepuka maradhi na madhara mengine yanayohusiana na ,atumizi ya maji ambayo si salama.

Ugonjwa wa kipindupindu upo katika kata ya Ruvu jirani na Mji wa Same na endapo wakazi wa mji huo, wasipokuwa makini katika kuzingatia kanuni za usafi, ugonjwa huo huenda ukapiga ahodi katika mjini huo mdogo wa Same.
source: MWANANCHI 5/12/09





Hii imegundulika same inamaana hata sehemu nyingi utakuwa unafanyika mchezo huu.
Sasa bongo tuwe na imani na kitu gani?. watu wanachezea afya za watu.
 
Hii issue ya kujaza maji yasiyo chemshwa na kuwauzia watu hasa abiria mbona ni ya zamani kabisa? Nakumbuka wakati tunasafiri na TRC miaka ya 90 tulikuwa tunakumbana na hili balaa hasa pale saranda na manyoni, itigi.
 
Back
Top Bottom