wadada wenzangu naombeni msaada

Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,347
11,610
hivi utamwamini mwanaume kwa vipi?
i mean nijiachie vipi na niridhike niwe na confidence niseme kabisa huyu flani huyu ni mpenzi wangu......
kiukweli naogopa aibu ... unamtambulisha mtu ,siku mbili tatu si mtu ni kiatu......
kiukweli uoga uliopo moyoni mwangu ni zaidi ya upendo naoweza kuoffer kwa mwanaume
mimi nawaona waongo tu .....
hivi kuna wa ukweli? nashangaa tu wenzangu wanaolewa .... i wish niwe na confidence kama wao ila nashindwa...wananiambia eti mwanamke hadi unaolewa lazima uwe ma.....l...ya.... try wanaume wengi as much as u can eti ndo ipo siku utapata wa ukweli eti ni kweli?

nawasilisha from real@smile
 
Jiamini alafu muamini na yeye kama hajakupa sababu ya kufanya vinginevyo.

Binafsi sijawahi kuwa na mwanaume aliyenipa wasiwasi (anacheat/hanipendi/ananichezea tu) ila bado sijawahi kumtambulisha mwanaume kama mpenzi wangu kwa ndugu au rafiki. Kwahiyo wewe ukishaweza kujiambia mwenyewe kwamba "huyu ni mpenzi wangu" huna haja ya kufikiria ohhh sijui nikiwaambia wengine ntaishia kupata aibu and such. . .wa muhimu ni wewe ukubali/uamini/ujieleze na uelewe basi.

Na hao unaosema wanaolewa tu kwasababu wana confidence jaribu kuzungumza nao ujue kama wanayo kweli au la, usidanganyike na unayoyaona. Waweza kuta wenzio wameamua kujilipua tu.
 
hata sielewi kwa kweli acha tu nikaombewe....au na mimi nijilipue?
 
mbona smile unaonyesha unajiamini sana?hiyo confidence yako ki ukweli mimi sina.na kuhusu hao viumbe,jipe muda nae kwanza,and then unaweza kumtambulisha kwa marafiki.ikila kwako,wewe hautokuwa wa kwanza na wala hautokuwa wa mwisho.nina amini wapo wanaume wengine wanaokuwa na wasiwasi na kutowaamini wanawake.mimi naamini kwa asilimia zote,wapo watu faithfull.ukiwa na mtu enjoy relationship yako na penda kama anavyokupenda
 
Hawa watu hua hawaeleweki Smile the best way to live with them is just to play your part and enjoy the moment when its there...
Mambo ya wewe kumtambulisha yaweke pembeni mwache yeye akutambulishe kama anapenda, kama yupo serious time will tell..
 
Last edited by a moderator:
hivi utamwamini mwanaume kwa vipi?
i mean nijiachie vipi na niridhike niwe na confidence niseme kabisa huyu flani huyu ni mpenzi wangu......
kiukweli naogopa aibu ... unamtambulisha mtu ,siku mbili tatu si mtu ni kiatu......
kiukweli uoga uliopo moyoni mwangu ni zaidi ya upendo naoweza kuoffer kwa mwanaume
mimi nawaona waongo tu .....
hivi kuna wa ukweli? nashangaa tu wenzangu wanaolewa .... i wish niwe na confidence kama wao ila nashindwa...wananiambia eti mwanamke hadi unaolewa lazima uwe ma.....l...ya.... try wanaume wengi as much as u can eti ndo ipo siku utapata wa ukweli eti ni kweli?

nawasilisha from real@smile

Japo kuwa umewauliza akina dada mi naweza kukushauri kuwa msingi wa ndoa ni Mungu. Kwa hiyo huna hata haja ya kujaribu wanaume maana waweza kuishia kubaya au kuumizwa zaidi na kujikuta umekosa kabisa hii sehemu nzuri kabisa ya maisha yako ualiyobaki. Mwombe Mungu na ujiamini kuwa kwa namna ulivyoumbwa lazima pia yuko mtu aliumbwa kwa ajili yako ili kufanya complete pair.
 
uliposema unashangaa wenzio wanaolewa
hapo ndo point muhimu

cha kufanya mwambie mtu wako yeyote anaekufuata
kuwa ungependa kuolewa
so hutakuwa tayari kwa sex wala mahusiano marefu bila ndoa kwanza

inasaidia
 
Wapo wanaume ambao they are for real smile, the first thing ni kujiamini wewe mwenyewe kwanza!! Coz most of the times wanawake wana tatizo la kutojiamini wao wenyewe, usipojiamini utaona kila mwanamke ni mzuri kukuzidi na nu tishio kwako; so jiamini kwanza before thinking about trusting ur man......... There z no shortcut. Anzia hapo kwanza.
 
hivi utamwamini mwanaume kwa vipi?
i mean nijiachie vipi na niridhike niwe na confidence niseme kabisa huyu flani huyu ni mpenzi wangu......
kiukweli naogopa aibu ... unamtambulisha mtu ,siku mbili tatu si mtu ni kiatu......
kiukweli uoga uliopo moyoni mwangu ni zaidi ya upendo naoweza kuoffer kwa mwanaume
mimi nawaona waongo tu .....
hivi kuna wa ukweli? nashangaa tu wenzangu wanaolewa .... i wish niwe na confidence kama wao ila nashindwa...wananiambia eti mwanamke hadi unaolewa lazima uwe ma.....l...ya.... try wanaume wengi as much as u can eti ndo ipo siku utapata wa ukweli eti ni kweli?

nawasilisha from real@smile

tupo wakweli smile
 
Pamoja na kuwa umelenga kupata mawazo ya wadada, naomba tu na mimi usome mawazo yangu juu yako. Ila samahani kama nitakukwaza kwa namna yo yote ile. Nilitamani nikwambia ktk private mail, lakini sijui naona kana sina jinsi, but also given the relevance of your mada
Mimi nimejiunga hivi karibuni hapa jamvini, lakini ktk uzoefu wangu wa muda mfupi hapa -of course kupita comments na mada zako mbalimbali nimegundua mambo mawili matatu juu yako ambayo binafsi naamini yana ukweli ndani yake. Nitayasema moja baada ya jingine:

Kwanza kabisa, kama baadhi ya watu walivyosema, unaonekana una confidence ya hali ya juu.

Pili, unajua ku-analyze issues mbalimbali zinazohusu relationship - binafsi nakukubali. Hii inanipa picha kuwa unauzoefu mkubwa ktk mambo haya aidha kwa kufanya, kusoma, kuona au kuishi na watu mbalimbali walio kwenye relationship

Tatu, uko makini sana ktk mambo yako -sijui nitumie maneno gani unielewe ninachotaka kueleza ktk point hii. Yaani wewe uko very perfect, ni TBS kwa maneno mengine. Mtu wa aina hii ni rahisi sana kuwa disappointed, maana unakuwa unategemea mwenzio naye awe kama wewe.

Nne, unaonekana siyo wanamke unayempenda mwanaume kwa kupasi time tu. Kwa maana nyingine unaonekana huwezi kumkubalia mwanaume eti kwa vile ana pesa, mali, kazi, madaraka sijui nini. Yaani, kwako ungetamani umpate mmoja unayempenda kwa vigezo vyako, na awe huyo huyo mmoja ktk maisha yako!

Tano na mwisho, nakuona kama ni mwanamke ambaye alishawahi kutendwa, tena mara nyingi tu. Matokeo yake ume-develop negativity kwa wanaume karibia wote.

Ila samahani kama nimeku-judge vibaya, ni mawazo yangu tu. Kama hayo niliyoyasema juu yako ni sahihi, basi haya ndo yanaweza kuwa chanzo cha tatizo lako. Kiukweli huwa natamani kama kungekuwa na uwezekano tukutane tuongee ana kwa ana (sounds private, lakini sina maana hiyo kabisa au najihisi, aaaha!). Nahisi ningeweza kukushauri zaidi na zaidi. Bahati mbaya hatuwezi kuonana due to geographical location.
 
..wananiambia eti mwanamke hadi unaolewa lazima uwe ma.....l...ya.... try wanaume wengi as much as u can eti ndo ipo siku utapata wa ukweli eti ni kweli?

point ipo hapo.....ni ukweli kabisa na hakuna kona kona kwa hili.....amini nakwambia....
 
Dunia imebadilika sana na maadili kushuka saana. Hilo swali Smile mdogo wangu unalouliza kua umwamini vipi mwanume…. Ni hilo hilo wanaume wanauliza kua amwamini vipi mwanamke na kama hata amtambulishe kwa wakaribu wake ambao ni wa maana (acha hawa wa kukuita shemeji njiani). Yastahili uvumilivu, kujua nini wataka na kujipanga…. Kwa mtazamo wangu ni kua Men treat you the way you want them to treat you…. Kama upo tayari kuolewa na unataka kuolewa kuna utofauti na matendo/mawazo na focus zako ukiwa huna mpango huo.

Mahusiano mara ya kwanza mara nyingi msingi wake ni Sex…. Ila mkivuka huo mpaka wa kuenda beyond, mkawa marafiki na partners, mwazungumzia maendeleo, mwapeana ushauri wa kujenga na kuboresha maisha… taratibu bond inakua na mwajikuta mwataka kua partners na kuoana for life. Kumtambulisha Mpenzi wako siku za mwanzo kwa mrafikizo sio muhimu wala msingi sana, inakiwa kue na kitime Fulani cha kusomana ili kujua mpenzi wako kama kuna kichembe cha hope kua ni the rite person. Huo mtihani haupo kwa wadada tu Smiles, saizi ni tatizo la wote. Wadada wa kuoa hawapo na akina kaka wakuoa hawapo. Smile naamini wewe ni mzima wa afya….
 
Last edited by a moderator:
uliposema unashangaa wenzio wanaolewa
hapo ndo point muhimu

cha kufanya mwambie mtu wako yeyote anaekufuata
kuwa ungependa kuolewa
so hutakuwa tayari kwa sex wala mahusiano marefu bila ndoa kwanza

inasaidia
Hawa wanao jidai hawagawi, ndo wakuwaogopa :bounce:
 
Smile ishu kwako ni moja tu, nayo ni hujampata mwenye vigezo vyako vyote au kwa asilimia kubwa. hili huwakuta mabinti ambao ni wazuri wajuzi na wenye utash mpana ila tu wanaweka vigezo vingi sana ambavyo huwa wanakosa anayefit kwa asilimia kubwa. ushauri wangu kwako ni angalia vile vigezo vya lazima sana kwamba lazima mume awe navyo vipe kipaumbele but vile subsidary visikuwazishe sana. i believe utapata confidence kwa staili hii. usiweke vigezo vyote kuwa muhimu but pia usividharu vile vya muhimu.
nisamehe kama nimekuudhi
 
mbona smile unaonyesha unajiamini sana?hiyo confidence yako ki ukweli mimi sina.na kuhusu hao viumbe,jipe muda nae kwanza,and then unaweza kumtambulisha kwa marafiki.ikila kwako,wewe hautokuwa wa kwanza na wala hautokuwa wa mwisho.nina amini wapo wanaume wengine wanaokuwa na wasiwasi na kutowaamini wanawake.mimi naamini kwa asilimia zote,wapo watu faithfull.ukiwa na mtu enjoy relationship yako na penda kama anavyokupenda
Mkuu konfidensi anayo kny kiibodi tu naona (just a joke!) Nacho kiona huyu binti ametulia kutokana na malezi na kanidham nakaona pia kapo, tatizo anaanza kukata tamaa, jambo litakalo mfanya kuchukua maamuzi hatarishi. afikirie kabla ya kuamua yeye ni wa pekee!. Nb. Ninaweza siyo Mdada ingawa amechangia kinyume na msisitizo wa mleta mada na anaomba samahani kwa hilo.
 
Back
Top Bottom