wadada wa kizazi kipya DRC nani zaidi?

Mkuu Thanks a lot kwa hii info...hiyo clip ya kwanza ninayo na baadhi za live show za Ferre akiwa na Wenge musica.........Msela ana sauti nzuri sana na haswa anapopiga rhumba na nyimbo zake nyingi hazina sebene kama zilivyo za kina Fally ipupa ni Full rhumba.Hivi kuna Band kweli za Kikongo zilizodumu toka enzi hizo mpaka sasa bila kuvugika.kama ulivyosema huyu SIPE ni hatari sana wa kuvuruga maband alivyochakachua hilo jina la inaonyesha ni jinsi gani alivyo wa sound..........Naona Extra Musica nao wamerudi kivingine nimepata baadhi ya Video zao mpya

Ntamuelezea kidogo SIMON SIPE watu wamjue ni mtu wa aina gani.Huyu jamaa anajulikana kama SERIAL BANDS BREAKER katika ulimwengu wa wapenda muziki wa lingala.Jamaa amezisababishia sintofahamu bendi nyingi sana kwa kuzigawa na yeye ama kubaki na bendi original au kuchukua rebels wa bendi na kufanya nao kazi.Tabia hii alianza nayo kwa ZAIKO LANGA LANGA mwaka 1988 baada ya kusababisha mgwanyiko katika bendi hiyo uliozaa Zaiko familia de zaiko langa langa ambayo baadae ikaja kujulikana kama ZAIKO NKOLO MBOKA iki release album yake " jettez l'eponge" huku simon sipe akiwa producer na meneja wake,Baadae nadhani 1990 akaichukua WENGE MUSICA kwa mkataba na mpango wa kutoa album tano za bendi pamoja na solo album za viongozi wa bendi hiyo kwa zamu.Wenge musica chini yake ikafanikiwa kutoa album ya Pentagone ambayo ailikua album ya bendi,then mpango unaofuata ulikua ni SIPE kuandaa na kuisimamia album solo ya kwanza chini yake lakini ya pili baada ya ile solo album ya Prince Alain Makaba ambayo aliifanya chini ya SONODISC,album hiyo ya kwanza solo chini yake ilikua ni album Feux De l'amour(ndombolo ya solo) ya JB Mpiana album ambayo ilipata mafanikio makubwa sana kuliko album zote za wenge toka ianzishwe.Sasa baada ya mafanikio hayo ya jb na solo album yake chini ya SIPE,jamaa SIPE inasemekana akaingia tamaa na kunogewa na jb,hapo haraka haraka badala ya kuanza kuishughulikia album ya bendi na baadae werrason atoe album yake solo kama ilivyokuwa imepengwa SIPE akataka Jb mpiana arekodi second solo album badala ya album ya kundi ikifuatiwa na hiyo ya werrason,hali iliyoanza kuleta joto la mfarakano ndani ya kundi,baada ya jaribio la SIPE kumbeba Jb kukwama ikabidi bendi ianze kuandaa album ya bendi lakini huku tension na hali ya kutoaminiana miongoni mwa member ikizidi kusambaa kimya kimya,hali hiyo ilendelea samba samba na maandalizi ya album lakini baadae zikazaliwa kambi mbili ndani ya bendi,moja ikiwa ya Mpiana na nyingine ya werrason hali iliyofanya kazi ya kurekodi album ya bendi kuwa ngumu na baadae Jb mpiana kwa ushawishi wa SIMON SIPE akaamua kujiondoa kundini akifuatwa na wanamuziki wote waliokuwa wakimuunga mkono,ambao ni swahiba wake wa damu wakati huo Alain makaba,Blaize Bulla,Alain mpela,Aimelia Lyase Demingongo,marepa Roberto Ekokota na chipukizi wakati huo Tutu Caludji na wengine kibao wakaenda kuanzisha wenge bcbg wakikwepa kutumia MUSICA kwa kuwa Wenge Musica ni jina lililobuniwa na Didier Masela ambae alibaki na Werrason na Adolphe Dominguez.....ambao wakaiendeleza wenge musica wakiongeza neno Maison Mere lenye maana ya Makao makuu(yani wenge yao ndio makao makuu nyingine zote ni branches)!

Huyo ndio SIPE ambae haraka haraka akiwa meneja na jb mpiana rais akaitafutia bendi safari ya kwenda ufaransa na kutumbuiza kwenye ukumbi wa BATACLAN ambapo pia waliitumioa ziara hiyo kurekodi fasta album ambayo wakaipa jina la TITANIC likiwa ni dongo kwa waliobaki na wenge musica yani kina werrason kwamba wamezama katika ajali ya meli ya TITANIC wao kina Jb wameokoka,ikumbukwe kuwa nyimbo karibu zote za kwenye album hiyo pia kina werrason walishiriki maandalizi yake na tayari ilikua imekamilika na walikua wameshaifanyia sana mazoezi na baadhi ya mapigo walishayatumia kwenye concert local na ile hapo juu ya abidjan ukiisikiliza utasikia mapigo ambayo yapo kwenye album ya TITANIC,na kudhihirisha kuwa kina werrason walishiriki kwenye kuiandaa album hiyo ukisikiliza album ya kwanza ya kina werrason ile FORCE DE INTERVENTION RAPIDE hasa huo wimbo uliobeba jina la album utaona unavyoanza amapigo yake ni kama ya wimbo wa TITANIC wa bcbg,wasiojua huwa wanadhani kina werrason waliiga,hapana,walishiriki hivyo wote walikua na haki ya kutumia.

Umafia mwingine wa SIPE aliufanya kwa Extra Musica ya congo brazzaville alipoisambaratisha vipande vipande kwa kuwashawishi baadhi ya member waasi na kuanzisha Extra Musica International ambako nako baada ya kutoa album mmoja akawagawa tena na kuzaa kundi lingine alilolichukua na kuliwezesha kutoa album,then umafia wa mwisho ndio ule niliouleza pale juu ambapo aliigawa vipande viwili wenge musica maison mere na kuzaa le marquis de maison mere ambayo haikudumu sana

Nadhani angalau mtakua mmemjua SERIAL BANDS BREAKER SIMON SIPE ambae ni raia wa IVORY COAST!
 
Haya ndio mambo ya Ferre Gola...taratibu..

 
Last edited by a moderator:
The Romantic we mkalii aisee.................Nimekubali mkubwa.HAPA SILAHA ZOTE NIMEWEKA CHINI
Hilo Song la Vita Imana nalikubali sana haswa ile remix yake aliyoifanya na kijana mdogo Shikito.......WE NOMA
 
Muziki ya congo now iko chini kisoko ,nigerians took over ,but koffi mbishi anapambana kibishi kwa kujibadilisha badilisha
 
Diamond platnumz kuna ngoma kafanya na fally ipupa iko store tu for almost 2 years,anaona upepo wa wacongo hauwezi kumvumisha kiviiile
 
Back
Top Bottom